THE DEVIL’S BIBLE
(CODEX GIGAS)
CODEX GIGAS
au kwa kiswahili (kitabu kikubwa),ndio kitabu kikubwa Zaidi kuwahi kuandikwa
duniani tangu medieval periods ( karne za kumi kumi).The codex Gigas kina
ukubwa wa (urefu sm 92,upana sm 22) na uzito wa kilogramu 75.Kitabu hichi pia kinaitwa
“Devil’s bible” au
biblia ya shetani kutokana na historia yake ,Pia katikati mwa kitabu hiki cha
maajabu kuna picha kubwa ya malaika wa zamani aliyetupwa yaani ibilisi na
shetani ambayo inaongeza utata juu ya kitabu hichi kikongwe.
Kitabu hiki
kiliundwa mwaka (karne ya 13) mwanzoni huko monastery of podlacize ndani ya mji
ambao kwa sasa unaitwa CZECH
REPUBLIC.
Ndani ya
kitabu hichi kuna biblia ya kiitaliano (latino) inayoitwa VULGATE BIBLE ikiwa ndiyo
biblia ya kwanza kwa lugha ya kiitaliano mwishoni mwa karne ya 4 ambayo baadae
ndiyo ilikuwa kuwa biblia halisi ya kikatoliki.Vitabu vingine mashuhuri
vilivyomo katika codex gigas ni pamoja na baadhi ya maandishi ya agano jipya na
agano la kale la biblia ya wakristo wengine pamoja na medica books au vitabu
vya uganga.
Baada ya
miaka mingi kupita baada ya kuandikwa kitabu hiki,kilifika katika maktaba ya PRAGUE ambao ndiyo mji
mkuu wa CZECH,ambapo
baada ya vita iliyoitwa “thirty years’ war”,maktaba hiyo iliharibiwa vibaya na
vitabu vingi kupotea,pia na codex gigas nayo ilipata madhara lakini ilisalimika
haikuweza kuungua baada ya mtu mmoja asiyejulikana kuibeba na kuitupia
dirishani nje ya maktaba ambapo ilianguka juu ya mtu ambaye alikuwa amesimama
chini ya maktaba hiyo na kumdhuru vibaya
kwa sababu ya uzito wake. Baada ya hapo biblia hii kubwa ilichukuliwa mpaka
maktaba kuu ya mji wa Sweden huko Stockholm ambapo sio kila mtu anaruhusiwa
kuiona.
Codex Gigas
kimefanyiwa binding kwa mbao,pia karatasi zake au velum ambapo maandishi
yameandikwa zimetokana na ngozi za punda wapatao 160 ambacho kina jumla ya page
320.Kwa sasa kitabu hiki kina page 310,mpaka sasa kuna maswali mengi juu ya
karatasi 10 zilizopungua,huku ikiwa haijulikani ni nani au kwanini karatasi
hizi hazipo huku wengine wakisema labda ziliungua siku ile ya moto maktaba
nk.Maandishi ya kitabu hiki yameandikwa kwa mwandiko wa aina moja yakiwa na
rangi za kijana,buluu,nyekundu na dhahabu.Kitu kingine kinastaajabisha juu ya
kitabu hiki ni picha mbili,moja ya mbingu na nyingine ya dunia wakati wa
uumbaji.
HISTORIA
YAKE (FROM LEGENDS)
Kutokana na
kumbukumbu,codex gigas iliandikwa na HERMAN THE RECLUSE mjini CZECH ambaye alikuwa ni MONK.Monk huyu inasemekana alikuwa
amevunja(amefanya kosa) baadhi ya sharia zao za kimonk,hivyo alihukumiwa kifo
kibaya cha adhabu kali kinachoitwa “walled up alive” yaani unajengewa kijumba
chako kidogo sana ambacho hakina upenyo ,kisha unaingia kwa kusimama mpaka
utakapokata roho.
kuepuka adhabu hiyo,monk huyu aliamua kutoa ahadi
kwa wakubwa zake na miungu yao kua atatengeneza kitabu kimoja kikubwa kwa usiku
mmoja ambacho kitakuwa na hekima yote ya dunia hii na kuwatukuza mamonks wote
milele na Ili milele.
Alipoanza
kufanya hiyo kazi,katikati ya usiku alianza kuona kuwa hawezi kuandika kitabu hicho
akamaliza kwa usiku mmoja peke yake hivyo alihitaji msaada. Alifanya maombi maalumu sio kwa Mungu bali
kwa Lucifer ama shetani ili amsaidie hiyo kazi.Legends zinasema Lucifer
alikubali kumaliza hiyo kazi huku akitaka roho ya Herman kama shukrani kwake.Hivi
ndivyo kitabu kilivyoandikwa na kuna sababu za msingi nyingi ambazo
zinathibitisha kitabu hiki hakikuandikwa na mwandamu moja wapo hii hapa.
1. Kwa mahesabu ya wanasayansi wanasema
kama kitabu hiki kingeandikwa na mwanadamu basi kingechukua Zaidi ya miaka 30
kukiandaa kutoka na umakini ambacho kinacho hiki kitabu,ikiwemo marembo mengi
tena yasiyopishana hata kidogo.
Mengine tutayaangalia kwenye toleo
jingine
Unaweza kutoa maoni yako chini,Ahsante.
Nice story,yaaani imenifurahisha sana.
ReplyDeleteAsante sana
ReplyDelete👏🏽
ReplyDeleteTupate kil
ReplyDeleteIchoandikwa ndani