Follow Us

TRENDING NOW

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa pekee ,ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.


 Karibu kutazama video ya fundisho kuhusu somo la Nguvu ya Mwanamke kutoka kwa Dr. Myles Munroe

Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa pekee ,ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.

 Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili vilevile.

Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule*
"Wanafunzi wakakubali halafu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.

Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia
Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu, akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake halafu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo nyumbani.
Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi yao


Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu usiowapenda moyoni
kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya, kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo wako unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.?
Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika, na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokoko moyoni mwako. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na visivyo na chuki ndani yake
Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe maana ni moja ya virutubisho vya moyo wako,Samehe kwa kila anayekukosea na kukukwaza



Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa pekee ,ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
The man of God, Man of People, Askari wa Mungu  na Mtu wa muhimu nabii/mwalimu Tb joshua umeenda,Pumzika kwa amani.


Bwana ametoa Bwana ametwaa. Tunajua upo mbinguni sasahivi.

LET LOVE LEAD
#EMMANUEL 

#tbjoshua #Emmanuel
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa pekee ,ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
πŸ’₯BIBLE STUDYπŸ’₯
Program: Christian theology & systemic theology.
(Kijana Mkristo-KM)

Sehemu 4
--------

Bwana Yesu asifiwe sana. Leo. Leo tunaendelea tena kama ilivyoada kwenye kipindi cha theolojia, na Leo tunaangalia juu ya


Majadiliano haya ndio chimbuko la mambo mengi ya muhimu unayoyajua leo juu ya Mungu na maandiko kwa ujumla. Tuanze pamoja na tumalize pamoja.


1. THE EXTENT OF NEW TESTAMENT CANON (MFUMO WA KUTENGENZA AGANO JIPYA)

πŸ‘‰πŸΌNaomba tuwe makini na hizi terms au misamiati ya kingereza nitakayoitumia kwenye kipindi hiki. Hii yote ni kuhakikisha sipotezi maana halisi ya maneno kwa kutumia lugha ya kiswahili.

🌀️Kama tulivyoona mwanzoni, ya kwamba Theolojia ya kikristo asili na chimbuko lake ni kwenye maandiko (scripture).

🌀️Kipindi kile cha patristic period au kipindi cha mafather au waanzilishi na waasisi wa hii theolojia, tuliweza kushuhudia maamuzi mengi wakiyafanya, moja ya uamuzi waliofikia kipindi kile ni huu hapa..


Au kuweka sawa na kuuunganisha maandiko ya agano jipya. Neno "canon" linahitaji ufafanuzi.

Neno hili limetokana na neno la kigiriki "kanon" likimaanisha kuongoza au a fixed reference point (sehemu pa kuanzia). Sasa maana ya CANON OF SCRIPTURE ni maandiko yenye mamlaka na yaliyowekwa pamoja na kupitishwa na Fathers ili yatumike kwenye kanisa la kikristo. Kwahiyo haya maandiko yote tunayoyatumia sasa hivi yamewekwa kwenye kitu kinachoitwa CANON.

MFANO: Injiri ya mtakatifu Luka ni "canical:" yaani imeptishwa itumike kwenye kanisa ila ijiri ya Thomas ni extracanonical (haikupitishwa). Naamini umeanza kuelewa namaanisha nini.

🌀️Kwahiyo,wakongwe hawa walikaa chini na tujadili maandiko yote ya agano la kale na jipya. Na yale waliyoyapitisha ndio walioyaweka kwenye canon of scripture.

Mpaka kufikia muda wa Father Irenaeus,ilipitishwa na kukubaliwa kuwa zipo INJIRI NNE TU (MATHAYO,LUKA,MARKO NA YOHANA).

Mwishoni mwa karne ya 2 mjadala mwingine ukakaliwa na kupitisha kuwa kitabu cha MATENDO YA MITUME na Barua za mtume paulo zina uvuvio wa Mungu (inspired scripture), kwa hiyo nazo zikaingia kwenye canonical of scripture.

🌀️Kufikia C.150 na C215) clement wa alexandria na wenzake walipitisha INJILI NNE,MATENDO,BARUA 14 ZA PAULO MTUME NA UFUNUO WA MITUME.

🌀️mwaka 367, Athanasius akatangaza na kuzungusha barua yake ya 39 ambayo ilijumuisha vitabu 27 vya agano jipya kama tunavyovijua leo.

🌀️Debate nyingi zikaendelea baada ya hitimisho hilo zilihusu idadi ya vitabu vinavyotakiwa kuwepo. Kwa mfano kanisa la mashariki walikuwa wanasitasita kuweka kitabu cha waebrania kwenye canon wakisema kuwa hakikuwa na uhakika kama kimeandikwa na Paulo mtume.pia na vitabu kama 2petro, 2 na 3 Yohana na yuda,mara kwa mara vilikuwa vinatolewa kwenye list ya vitabu vya agano jipya.

🌀️Baada ya hapo sasa likaja swala la mpangilio wa hayo maandiko. Makubaliano yamwanzoni yakafikiwa kuwa INJILI ZA YESU zikae mwanzoni kabisa mwa vitabu vya agano vikifuatiwa na MATENDO. Lakini kanisa la mashariki wao wakataka kuziweka barua 7 za roma (Yakobo, petro 1&2 , Waraka wa 3 wa Yohana na Yuda) kabla ya barua 14 za paulo (waebrania ilikubaliwa kama barua ya Paulo) lakini kanisa la magharibi wao wakaziweka barua za pualo 14 mara tu baada ya kitabu cha matendo baada ya hapo ndipo zikaa barua za roma au catholic letters. Kitabu cha ufunuo kilikuwa cha mwisho kwa pande zote 2.

🌀️mjadala huu wa mpandilo ulifungwa na wote wakaamua kufuata utaratibu wa kanisa la magharibi na wakakubaliana kuwa mada hii isiibuke tena.

🌀️Kipindi kijacho tutatazamia kitu kinachoitwa ECUMENICAL CREEDS (IMANIZA MAKANISA)

Zipp tatu tu
1. Apostles creess.
2. Nicene creed
3. Athanasian creed.

Stay tuned.

Cc; kijana mkristo.
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa pekee ,ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
πŸ’₯BIBLE STUDYπŸ’₯
Program: Christian theology & systemic theology.

(Kijana Mkristo-KM)

Sehemu ya 2.
-----------------------------------

Asili ya kanisa (ukristo).
---------------###---------------

Ukristo Asili yake hasa inaanzia "palestina" au palestine. Katika hii palestina kuna sehemu inaitwa JUDEA na ukifika hapa JUDEA kuna mji mkubwa uliochangamka unaitwa Yerusalemu. Hapo Yerusalemu sasa,ambayo ipo ndani ya palestina,ndipo ukristo ulipoanzia mnano karne ya 1 au First century (1 AD).

Fathers of The church

Sasa hapa palestina ndipo penye shida. Naamini wewe msomaji kuna maswali umeanza kujiuliza, inawezekanaje ikawa ni Yerusalemu halafu tena ndani ya palestina? Mimi nilidhani ni israeli?... Ni baadhi ya maswali unayojiuliza natambua. Sasa ukweli upo hapa chini.

πŸ•Έ️ Waandishi (scholars) wanaamini ya kwamba jina la palestina limetokana na neno "Philistia" neno ambalo linamaanisha "wafilisti". Kutokana na ushahidi wa biblia, wafilisti wanaonekana kukaa eneo hili la Philistia mnano karne ya 12 BC au kabla ya . Mengi tutajifunza zaidi kuhusu uhusiano wa Palestinina.

πŸ•Έ️Sasa kama tulivyoona ya kwamba ukristo umeanzia yerusalemu ndani ya palestina, ila kimsingi kabisa ukristo chimbuko lake ni dini ya JUDAISM huko judea.

Judaism ni nini?
------###------

Ukristo halisi chimbuko lake ni Kwenye dini hii ya Judaism ambayo yenyewe ilianzia pale kwenye hekalu la pili la Suleiman. Yani katikati ya ujenzi wa hekalu la pili na  kuanguka wa hekalu hilo,hapo ndipo judaism ilipoanzia BCE 515.

Dini hizi mbili zilitengana na kuwa tofauti ndani ya karne ya 1 kwa sababu zifuatazo.

πŸ‘‰πŸΌukristo huu tunaujua leo imani yake ipo kwenye AGANO JIPYA ambalo mwanzilishi wake ni YESU KRISTO. Hivo ukristo huu unaitwa ORTHODOXY yaani kutoka ndani ya agano jipya. 

πŸ•Έ️Hii judaism yenyewe ni kinyume cha ORTHODOX. Yenye imejikita Kwenye orthopaxy yaani tabia njema. Asili yake hasa ni kwenye AGANO LA MUSA AU ZILE AMRI 10 au unaweza kuita MOSAIC COVENANT. Wao wanaamini sana kwenye TORAH na TALMUD (Tutayazungumzia baadae).

πŸ•Έ️wakristo tunaamini kwenye wokovu binafsi kutoka kwenye dhambi kupitia kumpokea Yesu kristo kama Bwana na mwokozi wako. 

Judaism au dini ya wayahudi wao wanaamini kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu kupotia rituals(ibada za kitamaduni nk).

πŸ•Έ️Wakristo sisi tunaamini kwenye utatu mtakatifu. Yani Mungu mmoja kwenye nafai tatu (baba mwana ma Roho mtakatif). Pia tunaamini alama vile YOHANA 1 inavyosema kuwa Mungu aliuvaa mwili akawa kama sisi kupitia Yesu. Na ndio maana Yesu anaitwa Yesu kristo. Yesu ikiwa ni sehemu yake ya ubinadamu na kristo ni sehemu yake ya uungu (tutazungumza kwa undani).

πŸ•Έ️Hawa wayahudi wao hawaamini juu ya concepts zote izi. Wao wanaamini kuwa Mungu ni mmoja na hamna utatu pia hawaamini kuwa kuna siku Mungu aliuvaa mwili akawa mwanadamu.

Mambo haya ndio yanayotifautisha kati ya JUDAISM (UYAHUDI) NA UKRISTO (CHRISTIANITY)



THE PATRISTIC PERIOD
(FATHERS OF THE CHURCH)
--------###--------

Patristic period au kipindi cha waanzilishi wa kanisa (ukristo), ni kipindi cha muhimu sana kwenye historia na uendelevu wa dini hii ya kikristo. 

πŸ•Έ️Ma fathers hawa ndio wenye mchango mkubwa sana sana kwenye kujenga msingi imara wa kanisa ambalo tunaliona leo hii. Kila mkondo wa kikristo ikiwemo Lutheran,Eastern orthodox,anglican na hata Romam catholic, wanatambua kuwa Kipindi hiki  cha patristic ndicho kipindi pekee ambacho kimelitambulisha kanisa na ndio nguzi ya maandiko ya kikristo yote (Christian doctrines).

πŸ•Έ️Makanisa haya yote yanaendelea kukua kwenye misingi ambayo tayari umewekwa na nawa waandishi wa kwanza au waandisho wa kale.

πŸ•Έ️Utangulizi
-------###------

Neno patristic limetokana na neno la kilatin PATER LIKIMAANISHA "FATHER ". Jina hili la patristic bado lina debate nyingi sana na hii imepeleka literature au waalimu wengine wa theolojia na baadhi ya vitabu kutumia majina mengine kutambulisha kipindi hiki cha waandishi hawa wa kale wanaojulikana kama Fathers of the church.

1.kipindi hiki cha Fathers kilianza mwishoni kabisa mwa "New testament writtings" - mwisho wa uandisho wa maandiko ya agano la kale mnano karne ya 100 mpaka mwanzo mwa uanzishwaji wa baraza la CHALCEDON (Tutalizungumzia mbeleni).

2. Patrology:- hili ni somo ndani ya theology ambalo linahusika na kipindi hiki cha mafathers hawa tu. Unaweza ukajua umuhimu wao sasa kwenye dini ya kikristo. Patrology ni somo la ma Fathers kama vile Theology ilivyo somo la Mungu.

AGENDA KUBWA ZA KIPINDI HIKI.
-------###--------

πŸ•Έ️Kazi kubwa ya Fathers au waandishi hawa wenye heshima kubwa kwenye dini hii ya kikristo ilikuwa ni kutengeneza na kuweka mambo sawa. Mambo haya ni mambo ambayo yalikuwa yanaleta mkanganyo mkubwa baina ya watu kwenye ukristo.

πŸ•Έ️Mfano wa jambo ambalo wakongwe hawa ilibidi waliweke sawa ni uhusiano kati ya UKRISTO NA UYAHUDI (JUDAISM).

Kwa hiyo kwenye karne ya kwanza hawa mafathers walikuwa na kazi yeah kusolve mambo kama haya. Pia kuna mambo mengine ya msingi ambayo paulo ameyaongelea kwenye barua zake, mambo ni

1. Je, mkristo ambaye sio myahudi (gentile) ni lazima kufanyiwa tohara?

2.je, wakristo ni lazima wafuate sheria za chakula za kiyahudi?

3. Ipi ni nja sahihi ya kutafsiri agano la kale?

πŸ•Έ️Mambo haya yote na mengine mengi yenye ukakasi na ugumu ndio ililiwa kazo ya hawa mafathers au waandishi wa hizi doctrine kuyatatua.

Hapa ndipo panapoanza uzuri wa theolojia. Tutakapoanza kumchambua Father mmoja mmoja na kujua mchango wake kwenye ukristo ndipo utajua kwa nn tunasoma theolojia.

πŸ•Έ️Pia hawa mafathers ndio baadae wakaleta ile idea ya APOLOGETIC.  APOLOGETICS hawa ni watu ambao kazi yao ni kuitetea imani na dini ya kikristo kutokana na wale wote wanaoipiga vita.

πŸ•Έ️Kimsingi kipindi hiki kizima cha karne ya kwanza kanisa lilikuwa kwenye presha kubwa sana dhidi ya nchi (Roman empire), kwahiyo agenda nyingi za kipindi hiki zilikuwa ni za survival (jinsi ya kufanya kanisa liendele kuwepo) na hapa ndipo hawa apologetics walikuwa na kazi ya ziada.

πŸ•Έ️Hali iliendelea kuwa mbaya kwa kanisa mpaka ilipofika miaka ya (306-37) ambapo CONSTANTINE alikuwa rasmi Kiongozi wa Empire ya Roma. Constantine alifanikiwa kuipatanisha Roman empira na kanisa hivyo kwenye hii karne ya 4 ukristo ukawa dini kamili. 

πŸ•Έ️Rasmi mwaka 321, cinstantine akatoa tamko kuwa siku ya JUMAPILI iwe public holiday. Huu ndio mfululizo wa uanzishwaji wa dini hii.

πŸ•Έ️KIPINDI kijacho tutaenda kusoma wazee watuatao (church Fathers) na utaona jinsi gani wamepigana kuhakikisha wanajenga misingi imara ya dini ya kikristo.

1. Justin matryr (C.100-165)
2.Iraneus of Lyon (c. 130-200)
3. Origen(c 185-254)
4. Cyprian of carhage (alikufa 258).

πŸ•Έ️Pia tutaangalia kitu cha msingi sana kinaitwa
THE CAPPADOCIAN FATHERS hapa tutajifunza zaidi juu ya utatu mtakatifu.

Mungu akubariki sana wewe mfuatiliaji.

By
Maestro (rabbon)

YouTube: kijana mkristo
Instagram: kijana_mkristo
Web : Tzworships.blogspot.com
(0685225275,0623725275)
Yohana 3:16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanawe wa pekee ,ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.
πŸ’₯BIBLE STUDYπŸ’₯
Program: Christian theology & systemic theology.
(Kijana Mkristo-KM)

Sehemu 3
--------

Bwana Yesu asifiwe sana.
Kama tulivyosema kuwa leo tutaendelea na kuangalia wanatheolojia wachache wa muhimu na mchango wao kwenye msingo wa kanisa.

1. JUSTIN MARTYR (c.100- c. 165)

Huyu Justin yamkini ndiye apologist mkubwa zaidi kuwahi kutokea. Kama unakumbuka nilikwambia kwamba,hawa apologists ni watu ambao walikuwa na kazi ya kutetea wokovu kipindi hicho cha nyuma ulipokuwa unapigwa vita na wapagani. Kwhiyo katika watu ambao waliotetea vizuri imani, basi justin ni mmoja wao.

Huyu alikuwa kipindi cha karne ya 2. Alizaliwa palestina lakin maisha yake kwa kiasi kikubwa aliisha Roma ambapo alipata umaarufu kama Mwalimu wa kikristo.

Katika kitabu chake cha kwanza kinachiitwa "First apology" justin aliongea jambo la ajabu na la kustaajabisha sana. Nanukuu

"UKWELI WA UKRISTO, UPO KWENYE VYANZO VIKUBWA VYA KIPAGANI" yaaniiii

"Traces of Christian truth were to be found in Great pagan sources "

Inashangaza e??

Pia akaja kuandika andiko au doctrine inayoitwa SEED BEARING WORD ambapo humo alisema kwamba

MUNGU ALIANDAA NJIA YA KUJIFUNUA KWA MARA YA MWISHO KUPITIA YESU

Utaelewa zaidi mbeleni.


2. IRENAEUS OF LYONS (c.130-c.200)

Huyu alizaliwa SMYRAN (uturuki) lakini naye akakulia mjini Roma. Akaja kuwa askofu ndani ya Roma mwaka 178 na kufariki miaka miwili baadae aliwa askofu.

πŸ•·️Irenaeus anakumchango mkubwa sana na anakumbukwa mno hasa kwenye utetezi wake wa CHRISTIAN ORTHODOXY dhidi ya GNOSTICIM (waabudu miungu)

Najua unakumbuka niliwahi kukuelezea juu ya Orthodoxy kuwa ni imani ya kikristo inayoamini Mungu mmoja,utatu mtakatifu,Yesu Kristo kufa na kufufuka kwake.

3. TERTULLIAN (C.160-225).

Huyu alikuwa mpagani kutoka afrika kaskazini ambaye aliamua kuja kuwa mkristo akiwa na miaka 30. Wengi wanasema huyu ndiye Baba wa Theolojia ya kilatin au Latin theology.

πŸ•·️Alitetea sana sana Muunganiko wa agano la kale na agano jipya. Kulikuwa na kundi la watu wanaitwa MARCION ambao wao wanasema kuwa agano la kale na agano jipya ni miungu miwili tofauti. Hii ni dhana ambayo imani yake inatutoa Kwenye imani ya kristo.

πŸ•·️Tertullian ndiye aliyekuwa kwenye midahalo na hawa watu na kuwafundisha kuwa Mungu wa agani jipya ndiye Mungu wa agano la kale. Kwa kufanya hivyo, huyu ndiye alikiwa mtu wa kwanza kuweka Msingi wa maandiko ya utatu mtakatifu(doctrine of The trinity).

Tutakuja kuona yote haya.

4. ATHANASIUS (C.293-C. 373).

Athanasius akiwa na miaka 20 tu aliandika treaties juu ya INCARNATION OF THE WORD au NENO KUFANYWA MWILI.

πŸ•·️Hizi treaties ambazo alikuwa anaandika juu ya swala hili zilianza kujenga imani kwa watu ya kwamba Mungu alichukua umbo la mwanadamu kupitia mwanadamu Yesu kristo. Maandiko ya Athanasius yalikwa na mchango mkubwa sana kwenye maandiko ya bwana Arius ambaye nayeye alikuwa anatetea hoja hii ya Mungu kuwa mwanadamu. Huyu arius alisema kwambaaa, kama Yesu hakuwa Mungu kamili au Full God, basi majanga yafuatayo yangetokea

a) Ingekuwa Ngumu kwa Mungu kumuokoa mwanadamu kwa sababu haiwezekani kiumbe kuokoa kiumbe kingine.

b) Kama Yesu hakuwa Mungu,basi wakristo wote wanakufuru kwa sababu Tangu enzi zake za kwenye biblia, Yesu amekuwa akiabudiwa na kupelekewa maombi. Hoja hi ilikuwa ngumu sana kwa wapinzani kuijibu.

5. THE CAPPADOCIAN FATHERS.

Kuna hawa sasa wanaoitwa Cappadocians. Jina hili linatumika sana kwenye theolojia likuhusisha wanatheolojia wakubwa watatu (ndugu wawili wa kiume na rafiki yao) ndani ya kanisa la kigiriki mjini Cappadocia.

Wanatheolojia hawa watatu ni.
- BASIL THE GREAT (Huyu alikuwa askofu wa Kaisaria na kaka mkubwa wa Gregory wa nyssa)

- Gregory of nyssa (huyu alikuwa askofu wa Nyssa)
- Gregory wa Nazianzus ambaye alikuwa askofu wa Sasima na baadae Constantinople.

Waandishi hawa wote watatu wana umuhimu wao wa kipekee sana japokuwa kwa umoja wao waliweza kuweka

MSINGI WA MAANDIKO YA UTATU MTAKATIFU (DOCTRINE OF THE TRINITY)

πŸ•·️Huwezi kuzungumzia maandiko ya Roho mtakatifu na utatu mtakatifu bila kujifunza habari za Hawa watu watatu.

Tuangalie kiundani.
-----------------###---------------------

Kuna mtu wa muhimu sana apa nataka tumalize nae kwa leo. Mtu huyu anaitwa

AUGUSTINE OF HIPPO
------------------####--------------------

Alizaliwa mwaka 353 na alifariki mwaka 430. Wengi wanaamini kuwa huyu ndiye mtu mwenye mchango mkubwa sana kwenye kanisa la kikristo kutokana na historia yake ndefu.

πŸ•·️Augustine alivutiwa na mahubiri ya kristo baada ya kuhubiriwa na askofu ambrose akiwa mjini milani. Augustine baada ya hapo akarudi kaskazin mwa afrika ndani ya mji wa hippo (algeria kwa sasa) ambapo alikuwa askofu huko. Katika miaka yake 35 ya mwisho,Augustine alishuhudia changamoto nyingi sana ambazo zilikuja kuwa na umuhimu kwenye kulijenga kanisa la kikristo na mchango wa Augustine kwenye kuweka sawa changamoto hizi ulikuwa wa muhimu sana sana.

πŸ•·️Sasa, mchango mkubwa wa Augustine ulikuwa kwenye kukuza Theology kutoka kuwa kama chombo cha ubishani na kuwa KAMA SOMO LA DARASANI (ACADEMIC DISCIPLINE).

KATIKA KUSOMA KWENTU THEOLOJIA, TUTAMSOMA SANA AUGUSTINE ILI TUJUE MAWAZO YAKE YALIKUWA VIPI.

πŸ•·️Kwahiyo, Katika kipindi chote icho, Augustine aliweza kutengeneza mifumo mizuri hasa kwenye maeneo haya matatu.

- Doctrine of church and sacrament (maandiko ya kanisa na ubatizo)
- Doctrine of Grace (maandiko ya neema)
- Doctrine of trinity( maandiko ya utatu).

πŸ•·️Lakini cha kushangaza na cha ajabu, Augustine hakuwahi kuzungumzia swala la CHRISTOLOGY ama maandiko ya kristo.

Christology ni somo maalumu linalohusu Utu wa Yesu (Doctrine of Person of Christ).
-----------------####---------------'---

πŸ•·️Leo nimejarbu kukuletea kwa ufupi juu ya maisha ya watu wa muhimu sana kwenye THEOLOGY. Natumaini unaelewa maana ya neno THEOLOGY sasa.

Kipindi kijacho tutaona juu ya

🌀️KEY THEOLOGIAN DEBATES.

Cc: KIJANA MKRISTO