CODEX GIGAS au kwa kiswahili (kitabu kikubwa),ndio kitabu kikubwa Zaidi kuwahi kuandikwa duniani tangu medieval periods ( karne za kumi kumi).The codex Gigas kina ukubwa wa (urefu sm 92,upana sm 22) na uzito wa kilogramu 75.

THE DEVIL’S BIBLE
(CODEX GIGAS)

CODEX GIGAS au kwa kiswahili (kitabu kikubwa),ndio kitabu kikubwa Zaidi kuwahi kuandikwa duniani tangu medieval periods ( karne za kumi kumi).The codex Gigas kina ukubwa wa (urefu sm 92,upana sm 22) na uzito wa kilogramu 75.Kitabu hichi pia kinaitwa “Devil’s bible” au biblia ya shetani kutokana na historia yake ,Pia katikati mwa kitabu hiki cha maajabu kuna picha kubwa ya malaika wa zamani aliyetupwa yaani ibilisi na shetani ambayo inaongeza utata juu ya kitabu hichi kikongwe.
Kitabu hiki kiliundwa mwaka (karne ya 13) mwanzoni huko monastery of podlacize ndani ya mji ambao kwa sasa unaitwa CZECH REPUBLIC.

Ndani ya kitabu hichi kuna biblia ya kiitaliano (latino) inayoitwa VULGATE BIBLE ikiwa ndiyo biblia ya kwanza kwa lugha ya kiitaliano mwishoni mwa karne ya 4 ambayo baadae ndiyo ilikuwa kuwa biblia halisi ya kikatoliki.Vitabu vingine mashuhuri vilivyomo katika codex gigas ni pamoja na baadhi ya maandishi ya agano jipya na agano la kale la biblia ya wakristo wengine pamoja na medica books au vitabu vya uganga.
Baada ya miaka mingi kupita baada ya kuandikwa kitabu hiki,kilifika katika maktaba ya PRAGUE ambao ndiyo mji mkuu wa CZECH,ambapo baada ya vita iliyoitwa “thirty years’ war”,maktaba hiyo iliharibiwa vibaya na vitabu vingi kupotea,pia na codex gigas nayo ilipata madhara lakini ilisalimika haikuweza kuungua baada ya mtu mmoja asiyejulikana kuibeba na kuitupia dirishani nje ya maktaba ambapo ilianguka juu ya mtu ambaye alikuwa amesimama chini ya  maktaba hiyo na kumdhuru vibaya kwa sababu ya uzito wake. Baada ya hapo biblia hii kubwa ilichukuliwa mpaka maktaba kuu ya mji wa Sweden huko Stockholm ambapo sio kila mtu anaruhusiwa kuiona.

Codex Gigas kimefanyiwa binding kwa mbao,pia karatasi zake au velum ambapo maandishi yameandikwa zimetokana na ngozi za punda wapatao 160 ambacho kina jumla ya page 320.Kwa sasa kitabu hiki kina page 310,mpaka sasa kuna maswali mengi juu ya karatasi 10 zilizopungua,huku ikiwa haijulikani ni nani au kwanini karatasi hizi hazipo huku wengine wakisema labda ziliungua siku ile ya moto maktaba nk.Maandishi ya kitabu hiki yameandikwa kwa mwandiko wa aina moja yakiwa na rangi za kijana,buluu,nyekundu na dhahabu.Kitu kingine kinastaajabisha juu ya kitabu hiki ni picha mbili,moja ya mbingu na nyingine ya dunia wakati wa uumbaji.
HISTORIA YAKE (FROM LEGENDS)
Kutokana na kumbukumbu,codex gigas iliandikwa na HERMAN THE RECLUSE mjini CZECH ambaye alikuwa ni MONK.Monk huyu inasemekana alikuwa amevunja(amefanya kosa) baadhi ya sharia zao za kimonk,hivyo alihukumiwa kifo kibaya cha adhabu kali kinachoitwa “walled up alive” yaani unajengewa kijumba chako kidogo sana ambacho hakina upenyo ,kisha unaingia kwa kusimama mpaka utakapokata roho.
kuepuka adhabu hiyo,monk huyu aliamua kutoa ahadi kwa wakubwa zake na miungu yao kua atatengeneza kitabu kimoja kikubwa kwa usiku mmoja ambacho kitakuwa na hekima yote ya dunia hii na kuwatukuza mamonks wote milele na Ili milele.

Alipoanza kufanya hiyo kazi,katikati ya usiku alianza kuona kuwa hawezi kuandika kitabu hicho akamaliza kwa usiku mmoja peke yake hivyo alihitaji msaada.  Alifanya maombi maalumu sio kwa Mungu bali kwa Lucifer ama shetani ili amsaidie hiyo kazi.Legends zinasema Lucifer alikubali kumaliza hiyo kazi huku akitaka roho ya Herman kama shukrani kwake.Hivi ndivyo kitabu kilivyoandikwa na kuna sababu za msingi nyingi ambazo zinathibitisha kitabu hiki hakikuandikwa na mwandamu moja wapo hii hapa.
1.      Kwa mahesabu ya wanasayansi wanasema kama kitabu hiki kingeandikwa na mwanadamu basi kingechukua Zaidi ya miaka 30 kukiandaa kutoka na umakini ambacho kinacho hiki kitabu,ikiwemo marembo mengi tena yasiyopishana hata kidogo.

Mengine tutayaangalia kwenye toleo jingine

Unaweza kutoa maoni yako chini,Ahsante.

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

4 comments: