Katika kifungu hiki tutaangalia namna ya Yesu alivyokuwa akijaribiwa jinsi alivyokuwa anakabiliana na hayo majaribu na pia tutajifunza jinsi ya kukabiliana na hayo majaribu.
Maandiko yanasema YESU NDIYE NJIA YA KWELI NA UZIMA – Yohana 14:6
Maana yake kama unataka kuishi maisha ya utakatifu
na siku moja tuje kumuona Mungu,basi lazima tuishi sawa sawa na mafunzo ya Yesu
ambaye ndiye njia ya kwenda kwa Mungu baba.
Mathayo 4:1-3
YESU ANAJARIBIWA
“Ndipo
Yesu akaongozwa na roho kuingia nyikani ili kujaribiwana Ibilisi. 2 Alipokuwa
amefunga siku 40,mchana na usiku, akaona njaa. 3 Pia,
Mjaribuakaja na kumwambia: “Ikiwa wewe ni mwana wa Mungu, yaambie mawe haya
yawe mikate”
Hapa unaweza
kudhani kuwa labda shetani alikuja akawa anaongea nayesu uso kwa uso,labda
akiwa na mapembe na uso mbaya kama wengine tunavyodhani shetani alivyo,HASHAA!!
Biblia haituambii popote pale kama shetani anamapembe au kama shetani anamwili
wa kibinadamu,ila biblia inasema kuwa shetani ni Roho na alikuwa malaika mkuu
mbinguni. EZEKIEL 28 na
ISAYA 14:12
Kwa hiyo ujio wa
shetani kule jangwani alikuja kiroho zaidi na sio tunavyofikiria.alikuja katika
roho,kama ufunuo kwa yesu au mawazo,na yesu akatambua kuwa huyu ni adui kutoka
na maneno yake.
Kabla ya kuendelea
tuangalie vitu vya msingi vilivyojitokeza hapa
- Katika maandiko hapo juu,unaweza ona njia ambayo shetani anaitumia kumjaribu au kumlaghai yesu kuwa ni ile ile ambayo aliitumia katika bustani ya EDEN kumdanganya EVA(haijabadilika). –MWANZO 3:1-3Hapa pia anamjaribu yesu kwa kumuuliza “je,wewe ni mwana wa Mungu”?kwani shetani hakujua kama Yesu ni mwana wa Mungu?JIBU SAHIHI HAPA NI KUWA SHETANI ALIJUA YESU NI NANI,ILA ALITAKA KUPANDA HOFU(DOUBTS) KWA YESU ILI AACHE KUMUANGALIA MUNGU NA AANZE KUSIKILIZA SAUTI ZA SHETANI.
- Shetani hutumia udhaifu wetu kama fimbo ya kutupigia kila siku,katika Mathayo 4:2 yesu anasikia njaa baada ya kufunga kwa siku 40,Punde si punde shetani anakuja kumjaribu yesu kwa MIKATE (chakula).
- Pia tunajifunza kuwa katika mifungo huwa tunaingia rohoni,na ukiwa rohoni lazima ukutane na roho tofauti tofauti (za aina tatu).-ROHO WA MUNGU-ROHO WA SHETANI-ROHO YA MWANADAMU.Hapa yesu alikutana na roho wa shetani lakini alimtambua kwa sababu yeye alikuwa na roho wa Mungu (ROHO MTAKATIFU) .Baada ya Yesu kujaribiwa na shetani mara tatu MATHAYO 4:4 Yesu alijibu hivi.“IMEANDIKWA” Sio imeandikwa tu,ila imeandikwa wapi (BIBLIA).Kukabiliana na hili yesu alijua kabisa njia pekee ya kumshinda shetani ni kwa kutumia maandiko au NENO LA MUNGU.Neno la kwanza kutoka kwa yesu baada ya kila jaribu ilikuwa ni IMEANDIKWA,Hakuanza kuongea na shetani kwa maneno mengine kama ( unamaanisha nini,wewe ni nani,kwani vipi nk) yeye alijua kabisa kuwa anahitaji neon la Mungu kama lilivyo.Baada ya kusema imeandikwa ,ndipo akafuata kutaja maandiko kama yalivyoandikwa kwenye BIBLIA (neon la mungu) “IMEANDIKWA MTU HATAISHI KWA MKATE,BALI KWA KILA NENO LITOKALO KWA MUNGU”Hivi ndivyo ambavyo yesu alimshinda shetani na ndivyo ambavyo kila aami niye anapaswa kufanya ili kumshinda shetani.Yesu alifanya hivyo kwa majaribu yake yote.JE, UNADHANI SHETANI ANGEONDOKA BILA YESU KUTUMIA NENO/MAANDIKO?YAKOBO 4:3 – “ Mpingeni shetani naye atawalimbia ” –Tunampinga shetani kwa neon tu,na neon la Mungu.Baada ya shetani kumjaribu EVA wote tunajua yaliyofuata.JE TUNAFANYAJE KWENYE MAJARIBU?“Fanya kabisa yote unayoweza ili ujitoe kwa Mungu ukiwa mtu aliyekubaliwa, mfanyakazi asiye na lolote la kuonea aibu, ukilitumia sawasawa neno la kweli” 2 TIMOTHEO 2:15
Amen.
ReplyDeleteBarikiwa sana mtumishi wa mungu