JINSI AMBAVYO KIJANA ANAWEZA KUVURUGA WITO ALIYOPEWA NA MUNGU KUPITIA URAFIKI WENYE MAHUSIANO MABAYA
Dodoo zake ni kama hizi:Kwa mujibu wa baraza la kiswahili la taifa(BAKITA)

RAFIKI:Mtu ambaye anaukaribu na ushirikiano wa dhati na mtu mwingine ambaye,huwa siyo ndugu wala mpenzi wake


Kwa hiyo hata maana ya "urafiki" yaweza kutoka hapo kwenye maana ya rafiki;ambayo pamoja na  hii, urafiki ni ukaribu (uhusiano)wa dhati uliyopo kati ya mtu na mtu mwingine

Maana tatu ya neno mahusiano
(1)ni ufanano maalumu uliopo baina ya hali au vitu viwili au Zaidi
(2)ni urafiki wa karibu aghalabu wa kimapenzi baina ya watu wawili wa jinsia tofauti
(3)ni namna watu wawili au Zaidi wanavyounganishwa kwa kuzaliwa au kwa ndoa

Kwa mantiki hiyo kumbe si kila mahusiano yanaweza kupoteza wito wa mtu aliyo nao,isipokuwa Yale yasiyokuwa na tinja iliyodhaniwa

Maana ya WITO
(1)Kauli inayotolewa na chombo mfano taasisi,shirika,serikali au mtu binafsi kuhamasisha watu kuhusu jambo furani
(2)ni agizo rasmi la kutekeleza jambo,mfano kutoka Kwa  mtu au hata kwa Mungu mwenyewe

TWENDE PAMOJA KWENYE WITO WA MUNGU KWA KIJANA

WITO Ki-Biblia

(1)Mungu mwenyewe anawaita watu katika maana ya kuwaamuru au kuwakaribisha(Yer.7:13 Mt.9:13 Isaya 65:12)
(2)Mungu mwenyewe kumuita ai kumuteua mtu na kumuongoza kwa kadrii ya makusudi yake maalumu(Isaya 43:1 ; 46:11 Hosea 11:1 Mdo 16:10 Ebr.11:8)
Kumbuka:Wito wa Mungu siyo tu ni kwenye eneo la Huduma Bali,wito wa Mungu ni Zaidi kuliko kuokoa watu wake tu kutoka adhabu ya dhambi,kwa sababu yeye mwenyewe pia Kuwaita watu ili wafurahie Uhuru( Gal.5:1,13 );Pia Wabadilishwe ili wafanane na Kristo (Rum.8:29-30), tena aliwaita ili waeneze ujumbe wa Kristo (1Pet.2:9)Ili kushiriki ufalme wa Kristo (1Thes.2:12)

NB:Wito pia ni  kile alichokiweka Mungu kwenye moyo wa mtu,ili akifanye akiwa hapa duniani,kwa mfano kwa nabii Yeremia aliweka tabia(roho)ya UNABII (Yeremia 1:1-5)

Kwa hiyo,ikiwa UHUSIANO unaojengwa na watu au marafiki wawili,wakati mmoja  hana nia kama aliyo nao mwezake upo uwezekano aliye na wito wa Mungu ukatoweka  ukadhoofika, kama siyo kufa kabisa.

Jambo hili tunaliona kwenye BIBLIA pale tusomapo katika kitabu cha WAAMUZI sura 16 utaona habari ya SAMSONI ambavyo alivyohusiana na Delila mpaka akafunua siri ya nguvu zake kwa sababu ya tamaa(mimi kusema,tamaa ya PAJA la Delila);

Ndicho nacho chaweza kuwa kilichomufanya apoteze wito wake)anza kusoma Waamuzi sura ya 13,14,15)

Kwa maana hiyo,kwa Kijana Mukristo anapokuwa kwenye mahusiano,kupaswa sana amusikilize Mungu kupitia Neno lake,kuwa anasema nini juu ya UHUSIANO wake na mtu aliye Karibu yake.

Bila nafasi ya Roho mtakatifu kutokukosekana (YOHANA 14:26);yaani kumusikiliza anasema nini? 

Hitimisho: kwa Kijana ni muhimu kutunza AGANO lake na Mungu wake hata kama mbele kuna siketi,sura zilizopakwa uwanja na ndevu zilizochongwa kisasa,suruali nzuri zinazopendeza na kumelameta kama dhahabu,miguu ya biya,makaliyo makubwa,funguo tatu.


Dondoo zingine:

swali:

Ni wakati gani ambao maswala ya mahusiano yaanze?

NB: Hadi kufikia hatua ya mahusiano ambayo yatapelekea ,maana yake kunamuchakato ulianza nao,kwa hiyo hata mtu yeyote akitaka apate rafiki Mwenye baadhi ya tabia anazozitaka mtu ni lazima gharama ya muda itumike

NB: Ishara ya kujua kuwa huyu ni wa kwako:lazima awe anakupushi kwenye wito ulilowekewa na Mungu

NB:Tunza ushuhuda wako,unapokuwa kwenye mahusiano

NB: Elewa si kila mlango,unaweza kuingia,milango mingine ni milango ya watu na mwingine ni WASHETANI

NB: kama unamahusiano mazuri na Mungu,vitu vingine Mungu kuvitoa kama zawadi katika maisha yako

Pia AMANI MOYONI MWAKO:ni ishara (indicator) ya kukupa kujua kwa sehemu kubwa huenda kuwa,uliye naye kwenye mahusiano,ni sehemu katika maisha yako

Swali: Je?ni  vizuri kumwahidi musichana kuwa utamuoa? Au kuahidiana

NB: Elewa mahusiano sahihi pamoja na Mungu,humufikisha mtu kwenye mwisho muzuri,Bali mahusiano mabaya kumpeleka mtu pabaya

         Benjamin Toboka
                0675552440
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: