MTI WA UZIMA NA MTI WA UJUZI WA MEMA NA MABAYA.(THE TREE OF LIFE AND TREE OF GOOD AND EVIL)
Bwana Yesu asifiwe Brethren.
Kuna kitu nataka sio tujifunze,ila ni kama tukijadiri kwa pamoja kuhusu Miti hii miwili ambayo Bwana Mungu aliweka katika bustani ya Eden kabla ya kumuumba mwanadamu,ama adamu.Nitafurahi kama baada ya kusoma maongezi haya,utachukua muda wako kukomenti chochote kuhusiana mada hii.


Kuna maswali mengi sana na mijadala mingi inazukaga juu ya ukweli wa mada hii.mfano wa maswali ni kama yafuatayo.
1. Kwanini Mungu aliamua kuifanya miti miwili bustanini?
2.Je,alishindwa kuweka mti mmoja tu,mti wa uzima?
3.hii miti miwili ni miti kweli au ni lugha ya picha?
4.Maana nyingine ya miti hii miwili,

Na maswali mengine mengi sana...ila nitayajibu yote kwa pamoja kama ifuatavyo

Mungu alimuumba mwanadamu siku ya 6 baada ya kuumba kila kitu.Mungu aliumba mbingu,nchi,wanyama na miti yote kabla ya kukuumba wewe.Baada ya Mungu kumuumba mwanadamu,hapo hapo akampa masharti ya jinsi ya kuishi katika nchi aliyomuandalia yaani Eden.tusome chinii
...
BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza. BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
MWA. 2:15‭-‬17

Unaweza ukaona jinsi Mungu alivyotoa maagizo ya moja kwa moja kwa adamu juu ya utaratibu wa kuishi mahali pale.

Utata ndipo unapoanzia hapa,hi miti ilikuwa ni nini?

Twende taratibu kidogo.
Muda huu Mungu anamuumba mwanadamu,au muda huu ambao Mungu alikuwa anaumba vitu vyote, shetani au Lucifer alikuwa tayari ameshaasi na ameshatupwa kutoka mbinguni,yaani alitupwa mpaka nchi. Ukumbuke kuwa ,moja ya kosa zito lililomfukuzisha kazi shetani mbinguni ni kiburi na wivu. Aliwashawishi na baadhi ya malaika ambao sasahivi tunawaita mapepo kuwa upande wake wa kuasi,hivyo walitupwa pamoja kutoka mbinguni.

Kwahiyo muda ule Mungu anamuumba adamu,alijua kabisa kuwa hatakuwa peke yake,tayari yupo Bwana mdogo mmoja mjanja mjanja katangulia uku.

Mungu ni pendo,na upendo haufosiwi,ili Mungu adhihirishe upendo wake,lazima atoe uhuru kwa watu...hata joshua aliwaambia wana wa israel kuwa wachague ni nani watakae mtumikia,aliwapa machaguzi na ndivyo Mungu alivyo.

Kama angetaka mwanadamu amfuate yeye tu,asingeshindwa,ila huenda tungemfuata kwa hofu na sio upendo kitu ambacho kingemtoa Mungu kwenye asili yake ya upendo.

Mungu akaumba miti miwili.Hapa alikuwa ameweka falme mbili,yaani ufalme wa kuzimu/shetani na ufalme wa mbinguni na kumwachia mwanadamu achague aende wapi,lakini pia alimwambia kuwa asichague ufalme wa giza kwa sababu atakapouchagua tu,atakufa...inashangaza sana
..
Kumbe ile miti miwili,zilikuwq falme mbili,ila ilikuwa ni miti kama miti. Mungu alikuwa anataka apime utii wa mwanadamu hapa. Lakini mwanadamu akachagua ufalme wa giza na hapa ndipo shetani alipopata nguvu kwenye maisha yetu.

Mungu aliendelea na aina hii ya uumbaji mpaka alipokuja kumleta Yesu. Ila ngoja nikujuze kitu cha ajabu ambacho labda hukuwahi kukijua au hukuwahi kusikia kabla.

Mara tu ya mwanadamu kula lile tunda,na kuasi kwa Mungu. Yesu/Mungu pale pale akatafuta plan B ya kumkomboa mwanadamu. Kitendo cha adamu kula lile tunda,ilikuwa ni mfano wa kufanya agano na kuzimu au ufalme wa giza. Sasa agani linakuwa na vitu vitatu vikubwa. Cha kwanza ni ahadi au benefits/promises of covenant,cha pili ni principles au kanuni za agano na cha tatu ni signs au seal of the covenant. Adamu alipokula lile tunda,alikuwa ameshajifunga kwenye vitu viwili vya mwanzo kikabakia kimoja tu, (sign/seal of the covenant) ambao ulikuwa ni mti wa uzima.kama adamu angekula na tunda ka mti wa uzima,basi tungeishi kwenye maisha ya dhambi milele,kwa sababu angekuwa amejifungia mwenyewe kwenye agano la kuzimu milele.Mungu kwa kutambua hilo,pale pale baada ya adamu kula lile tunda,akawatuma Makerubi wenye panga zikatazo kuwili waulinde mti wa uzima ili adamu asije akaula. Ashukuriwe Mungu kwa kuulinda wokovu wetu kwa njia ya hawa makerubi.

BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; kwa hiyo BWANA Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
MWA. 3:22‭-‬24 


Wokovu ni neema kubwa sana. Kama adamu angekula lile tunda,basi tungeishia kwenye dhambi maisha yote.

Kwa hiyo ile miti miwili ni falme mbili m,ufalme wa giza na ufalme wa Nuru. Ufalme wa giza umetamba sana juu ya mwanadamu mpaka alipokuja Yesu. Adamu akamzaa kaini na abeli. Abeli alisimama badala ya ufalme wa nuru,kaini ufalme wa giza,lakini giza lilishinda Nuru. Yesu Yesu pekee ndiye aliyelishinda giza.Yesu anasema katika kitabu cha Yohana. 

YUAJA MKUU WA ULIMWENGU,LAKINI HANA KITU KWANGU.

Hauwezi kumshinda shetani kama hauna Yesu.Yesu peke ndiye aliyemshinda Shetani.

Kama unashida,kimbilia kwa Yesu,unaumwa ni Yesu pekee mwenye majibu kwako.shetani hawezi kufitinika mwenyewe,pepo hawezi kumtoa pepo mwenzake.Unapoenda kwa waganga,unakuwa unatoa pepo kwa mapepo kitu ambacho hakipo na hakiwezekani,ni kujiongezea shida zaidi. Mkimbilie Yesu,yeye anasema ndiye njia,kweli na UZIMA. yeye ndiye UFUFUO NA UZIMA. uzima wa Roho na mwili upo kwake ba sio kwingine.

Amen.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

1 comments:

  1. Mimi nikisoma vizuri naona kama Mungu aliumba miti ya aina tatu
    1. Kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa
    2. Mti wa uzima
    3.mti wa ujuzi wa mema na mabaya

    Lakini pia tunda gani hilo walikula mara wakawa uchi?,,, na je watoto wawili aliowazaa hawa walitoka wapi, kama aliwazaa na adamu kwann kaini anawakilisha ufalme wa giza

    ReplyDelete