WAZEE ISHIRINI NA WANNE
Ufunuo 4:4 inatuambia ya kwamba kuna wazee 24, ambao wamevikwa mavazi meupe na kuvikwa taji ya dhahabu katika vichwa vyao, wameketi katika viti 24 vinavyozunguka Kiti cha Enzi cha Mungu.
Tumejifunza ya kwamba Wazee ishirini na wanne wanasujudu kwa kuinama mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu, kutoka katika Ufunuo 5:14 na 19:4. Wazee 24 pia wanasimamia maombi ya Watakatifu (Ufunuo 5:8) kuna wazee sita ambao wanawajibika katika kila sehemu ya robo moja ya eneo lote lenye robo nne za eneo (6x4=24)
Kazi ya Mduara wa Ndani na wa Nje:
Wazee 24 wanaozunguka Kiti cha Enzi cha Mungu, wanafanya Baraza (Council). Baada ya Masihi kutiwa mafuta kuliko wenzake wote na kukubalika kuwa mganda uliotikiswa na kukubalika kuwa sadaka iliyo bora zaidi, muundo wa Baraza la Kiti cha Enzi cha Mungu unakuwa kama ifuatavyo hapa chini;
(1) Mungu ameketi katikati ya mambo yote
(1) Masihi ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu
(4) Viumbe wanne wenye uhai
(24) Wazee 24.
Jumla ya idadi yote hapa ni 30, ambayo ni idadi inayofanya Baraza la ndani la Mungu aliye Juu sana Aliyetukuka. Baraza la nje linajumlisha wazee wengine 40 wanaofanya idadi ya wajumbe wote wa baraza kuwa 70. Kundi la nje lenye wazee wanne kila moja kutoka katika kundi la wale Wazee 40 wa Baraza la Nje, wanasaidiana na wale viumbe wenye uhai na kundi la Baranza la ndani la wazee 24 likiwa limegawanyika katika kundi la wazee sita sita, wanasaidia katika utawala wa sheria za Mungu. Robo kila kundi likiwa na mamlaka katika robo ya eneo lao.
Kuna kumbukumbu nyingi katika idadi ya namba hii ya 70 katika Maandiko. Kihistoria inaonyesha ya kwamba Musa aliwatia mafuta wazee 70 (Hes. 11:24-26). Hata katika Baraza la makuhani (Sanhadrin), ambalo ndilo lilikuwa Baraza kuu la Utawala wa Wana wa Israel lilikuwa na jumla ya idadi ya Wazee 70 wa Baraza lote. ( tazama pia Kut. 24:1,9; na Lk. 10:1,17).
Huu ndiyo ulikuwa asili ya Muundo wa Utawala wa Baraza la Mungu tangu awali, kutoka katika Maandiko tunaona jinsi Mungu anavyopanua Baraza lake, na tutazungumzia jambo hili kwa undani zaidi baadaye. Mungu atawaweka pia viumbe wapya kushika mamlaka ya tangu awali yaliyoachwa wazi kwa sababu ya maasi ya Jeshi la Mbinguni.

Post A Comment:
0 comments: