Tunajua Mungu ndiye muanzilishi wa Ndoa.Yeye ndiye aliyemuumba mwanadamu wa kwanza na kumewka katika eden. Baada ya muda akona sio vema huyu mtu awe peke yake, akamtafutia mke na sio wake. MWANZI 1:26.
Wake wengi ni kitu ambacho kimezoeleka snaa afrika na katika jamii nyingi za waislamu.

Swali ni je,Mungu mpango wake kwa ndoa ni upi?

Tunajua Mungu ndiye muanzilishi wa Ndoa.Yeye ndiye aliyemuumba mwanadamu wa kwanza na kumewka katika eden. Baada ya muda akona sio vema huyu mtu awe peke yake, akamtafutia mke na sio wake.
MWANZI 1:26.

Kama Mungu angetaka Adamu awe na wake wengi basi angewaumba wanawake wengi kwa sbabu anao huo uwezo,ila aliona kuwa mwanamke mmoja anamtosha adam.

Kuna mifano mingi ya ndoa za wake weng kwenye biblia na muanzilishi ni Lamech (mwanzo 4:19).

Mwingine ni Abrahamu,Esau pia.pia usisahau kuwa ,hata mwanadamu mwenye hekima kuliko wote,suleiman, nae alikuwa na wake wengi mno mno,wake 700 na michepuko 300.

Wote waliokuwa na wake zaidi ya mmoja kwenye biblia walipata madhara,ukianzia na suleimani.

Sasa tuangalie baadhi ya sheria za Mungu juu ya ndoa.
Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja. Nao walikuwa uchi wote wawili, Adamu na mkewe, wala hawakuona haya.
MWA. 2:23‭-‬25 

Utaona kuwa Mungu alisema Mwanaume ataenda pamoja na mkewe,sio wake bali mke..pia mwandishi anasema hawo wawili,watakuwa mwili mmoja..ni wawili tu..na hii ndiyo ndoa ya Mungu.

Paulo mtume anafananisha ndoa ya mke na mume kama kristo na kanisa

Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
EFE. 5:23 ,Efeso 1:22-23


Paulo anamfananisha mke kama mwili,huwezi kuwa na mwili zaid ya mmoja.kama Yesu alivyo na kanisa moja,hivyo hivyo mume awe na mke mmoja.

Naomba nifupishe hii kitu kwa mumalizia na andiko hili.

Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha;
1 TIM. 3:2 

Mke mmoja tu.

Sasa swali,je mwenye wake zaid ya mmoja,afanyaje ili aokoke

Kwanza kabisa.

Lazima mtu huyu amkubali Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake na atambue kuwa yeye ni mwenye dhambi na imempasa kutubu. (Marko 16:16,matendo 2:28,warumi 10;10)

Akitubu,lazima aachane na wake wake wote,isipokuwa yule wa kwanza,huyo ndiye Mungu Mungu anatambua kama mtu uliyefanya naye agano.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: