Historia zote za watu wakubwa na mashughuli katika Biblia hazijaanza wakiwa mashughuli. Utamkuta Daudi machungani, Yusufu utumwani, Daniel utumwani, na hata mitume 12 wa Yesu walitikea katika hali za chini kama Petro na wana wa Zebedayo walikuwa wavuvi, Mathayo mtoza ushuru, n.k.
Kuna watu wanaibukia tu kutamani kuwa wachngaji, wahubiri wakubwa, lakini wanasahau kanuni ya kuinuliwa ni kuwa chini kwanza. Kila aliyeanzia juu kama ameitwa na Mungu ni lazima ashushwe chini ili aanze moja na Mungu!
Usijivunie speed uliyonayo sasa ya kujenga Nyumba ya ghorofa tisini kama haujajenga msingi wenye uwezo wa kuhimili ghorofa hizo. Gharama ya Nyumba nzuri inapatikana wakati wa kutengeneza msingi imara wa Nyumba yako.
Huduma yako, biashara yako, kazi yako, masomo yako, umevijenga kwenye msingi ulio Imara kiasi gani? Msingi wa kustahimili nyumba ya vyumba vitatu hauwezi kufanana na msingi wa ghorofa nne.
Yale magumu unayoyapitia na na changamoto za hapa na pale havijaja kwako kwasababu umelaaniwa ama Mungu hakujui. Ni ili kukukujengea msingi ulio Imara kwenye hicho ukifanyacho. 1 Petro 1:7 ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Imani ya mtu juu ya nguvu za Mungu hapa inatajwa kuwa ni ya thamani sana. Kwasababu kila kitu tunakipata kwa Imani. Unataka kuwa Mchungaji mwema amini katika yeye alitekuita, unataka kuwa mhubiri mkubwa ama mfanyabiashara mashughuli, amini Mungu katika lile uliloitiwa. Lakini, hakikisha hiyo Imani yako unakubali ipimwe. Kwasababu ina thamani kuliko dhahabu. Imani ndiyo itakayokupa chochote na nafasi yoyote unayoitaka. Sasa usikimbilie lile jina ama yale mafanikio. Imarisha Imani yako katika Kristo kwa kukubali mitihani toka kwake, na hilo Jina litakufuata.
LTzworships.blogspot.com
Post A Comment:
0 comments: