Ukiwa kama mtumishi wa Mungu,majaribu ni lazima yakupate,kiuharisia jaribu ni changamoto ambazo lazima ukutane nazo katika safari yako ya imani,hazikimbiliki kabisa. Yesu alijaribiwa pia alipokuwa duniani ili kutuonyesha yatuoasayo kuyafanya kipindi tupitapo kwenye majaribu.
Kuna kitu kingine ambacho wengi tunakichanganya wengi tunaamini jaribu ni lazima mtu upate shida fulani,ama magonjwa,kuyumba kiuchumi nk,hii dhana haipo sahihi sana,kuna aina ingine ya majaribu ambayo haihusiani na mambo hayo kabisa.
Basi tuanze kuangalia mambo ya msingi,naamini baada ya kipindi hiki,maswali mengii kuhusu majaribu tutakuwa tumeyajibu. Amen
AINA ZA MAJARIBU
Kuna aina kuu mbili za majaribu ambayo tunayapitia katika maisha ya wokovu.
1. KUJARIBIWA KWA KUFANYA MAOVU
Tutachukua muda mwingi kuzungumzia aina hii ya kujaribiwa.Hivyo vipengele vitakavyofuata (maana ya jaribu,vyanzo vya majaribu,aina mbali mbali za kujaribiwa kwa maovu,jinsi ya kushinda majaribu) vyote vitakuwa vinazungumzia aina hii ya majaribu NB; KUARIBIWA KWA MAOVU HAKUTOKANI NA MUNGU.
YAKOBO 1:13 - Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.Kujaribiwa kwa maovu ni tendo la kumvuta na kumdanganya mtu ili ikiwezekana mtu huyo atende dhambi (YAKOBO 1:14-15). Kujaribiwa sio dhambi,ila kuingia kwenye namna hii ya majaribu na kuvutika mpaka kufanya uovu ndio dhambi.
Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.EBR. 4:15
Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.1 THE. 3:5
Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo.2 KOR. 11:3
Wakatokea Mafarisayo, wakaanza kuhojiana naye; wakitafuta kwake ishara itokayo mbinguni; wakimjaribu.MK. 8:11
Post A Comment:
0 comments: