EZEKIEL 47:1-5.

Utangulizi :- 
 kama ilivyo katika maisha yetu  kuna  hatua tunapita  kufikia hatua nyingine.  Ndivyo ilivyo katika  huitaji wa kumtafuta Mungu na nguvu zake  kunavyo temegea juhudi binafsi katika maisha yetu ili kufikia  kiwango ambacho unakihitaji. 

Ukisoma  Ezekiel 47:3-5  
Tunaona Mungu anabainisha  hatua mbali mbali ambazo   alimpitisha   Ezekiel  kama ifuatavyo :-

🍇nguvu  zinazo ishia  mpaka  viweko vya miguu. Ezekiel 47 :3,

🍇nguvu zinazo ishia mpaka magotini. Ezekiel 47 :4(a)

🍇nguvu zinazo ishia mpaka viuno .
Ezekiel 47 :4(b)

🍇nguvu zisizo weza kuvukika. Ezekiel 47 :5

Hapa 👆🏻tunaona Mungu  akitumia mfano wa  maji  kupitia kipimo cha  uzi,   
   
Swali  : kiwango kipindi cha nguvu za Mungu zinaweza kunishindia vita dhidi ya adui Zangu?  

 Hapa  lazima ufahamu  kila  vita  Ina kiwango chake  cha  nguvu ya kupambana kinacho takiwa uende nacho mbele ya adui zako ili  kupata ushindi  . 

Mfano : adui  anakuja mbele zako  akiwa na  nguvu  zilizo pita  viweko vya  miguu ,  hapo inamana lazima  wewe  umkabili kwa nguvu Zaid ya  yeye  ili  upate  ushindi.  

Kumbuka  goriati alienda mbele ya  daudi na  nguvu zake  kwa kiwango alicho ona kinaweza kumshindia,  ila DAUDI  alimkabili  kwa kiwango cha  nguvu zisizo weza kuvukika  na ndio Maana  alishinda.  

 Sasa  kwanini  wengi  tunashindwa  kumshinda adui? 

Ni kwasasabu  tunaenda kukabiliana na adui  tukiwa na  nguvu ndogo  unakuwa chini ya kiwango, sasa  usitegemee uwe na nguvu zinazo ishia mpaka viweko vya miguu  upate ushindi dhidi ya adui zako  walio kuja na  nguvu zinazo ishia mpaka  magotini  nk.  

 NINI  KIFANYIKE  
🍇fahamu Mungu  hajibu na nguvu za Mbinguni  moja kwa moja,  Isipokuwa  anatumia kiwango cha nguvu zilizo ndani yako  kwanza  baada ya  kutumika, ndipo  anazirejesha  ndani yako. 

🍇 jifunze kutathimini  kiwango cha nguvu za Mungu   zinazo ishi ndani yako. 

🍇 vaa utayari binafs kwaajili ya kutafuta uso wa Mungu kwa bidii. 

🍇usiogope gharama ya kuwa na nguvu za Mungu. Kwa sababu kila kiwango kina changamoto zake. 

🍇 fahamu kila kiwango cha nguvu za Mungu unacho kihitaji kinapelekea  uingie kwenye  msimu  mwingine  wa maisha ya kiroho na kimwili. 

NOTE : Usiridhike na  nguvu ulizo nazo  tamani  kupanda nguvu hata nguvu.  
Zaburi 84:7(a). 

UBARIKIWE 
wako katika Bwana 
TULINAGWE MWABUKUSI
TANGA 
14/5/2020
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: