SOMO: TEKNIKSI AU MBINU ZA MSINGI AMBAZO ZITAFANYA UMILIKI NA UJUBIWE MAOMBI YAKO SAWA SAWA NA HAJA YA MOYO WAKO. (FAIDA NA HASARA ZA NADHIRI)

Bwana Yesu asifiwe,nina wasalimu.
Tayari tumeshaangalia vitu vitatu vya msingi ambavyo ni
1.Maombi
2. Kufunga
3. Zaka

Leo tunaenda kuangalia kitu kingine cha 4 cha msingi kabisa na kitakuwa  kitu cha mwisho katika mfululizo huu wa haya masomo.

4. NADHIRI
Nini maana ya Nadhiri?
Kabla ya kujibu hili swali,ningependa nikukumbushe kuwa,nadhiri ni mbinu ya nne ya kufanya ili Mungu aweze kushughulika na haja za moyo wako.

Inawezekana umeomba sana bila majibu,umefunga sana na bado mambo magumu..sasa ni wakati wa kujaribu kumtolea Mungu nadhiri na uone kama hatajibu haja ya moyo wako.

NADHIRI: Nadhiri ni kinyume cha Agano. Nadhiri ni kiapo (Vow) ambacho anaapa mwanadamu na Mungu wake.

Ngoja niweke sawa hapa.
Nimesema nadhiri ni kinyume cha agano. Agano ni makubaliano kati ya Mungu na watu wake. Na mara zote Mungu ndiye anayekuwa mwanzilishi wa agano kati yake na wanadamu. Na hili agano halivunjiki.,kuvunjika kwa agano maana yake Mungu amekufa au hayupo..kitu ambacho hakiwezekani. MUNGU WETU NI MTUNZA MAAGANO.

Nadhiri ni tofauti kidogo tu na agano. Nadhiri inaanzishwa na mwanadamu na sio Mungu kama ilivyo kwa agano. Agano analianzisha Mungu ila nadhiri (kiapo) anaanzisha mwanadamu ila kina kuwa kinamuhusu Mungu...

Kwamba Baba kama utanifanyia hivi basi na mimi ntakufanyia hivi.
Unaweka ahadi mbele za Mungu ya kwamba kama atakupa kazi,basi utamjengea kanisa,kama atakupa mtoto basi utamtoa kwa Bwana,kama atakufaulisha mitihani,basi utatoa kitu fulani kwa Bwana..nk

Unaapa na kula kiapo na Mungu wako..hiyo ndiyo nadhiri....ukifanya hivyo Mungu anakuja chap chap kutimiza haja ya moyo wako...

NADHIRI haijawahi kushindwa hata siku moja.

"Mtu atakapomwekea BWANA nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake."
HES. 30:2

Unapomwekea Bwana nadhiri,unakuwa umeifunga nafsi yako kwa Bwana,hilo ulilolitaja halitatanguka mpaka litimie. Usiweke nadhiri kwa haraka haraka kama huwezi kuitimiza,fikiri sana na mara nne nne kabla ya kuweka nadhiri na Mungu wako kwa sababu utakachosema hakitatanguka...Mungu atafanya upande wake halafu atakuwa anakusubiri wewe ufanye upande wako..na hapo ndipo penye tatizo wapendwa. Mungu anapokuwa anakusubiria wewe,ndipo penye tatizo hapo...tuendelee kidogo.

Kwahiyo kwa nadhiri unakuwa umefunga Mungu ashughulikie swala lako na umejifunga wewe mwenyewe kutimiza nadhiri yako.

MADHARA YA NADHIRI
....
MATENDO SURA YA 5 panaweka wazi juu ya madhara ya nadhiri.
Anania na safira
(Mkewe) waliweka nadhiri kwa Bwana juu ya kiwanja chao,kuwa wakikiuza kiwanja chao,ile fedha watatoa kwa Bwana....Mungu akafanikisha hilo,wakauza kiwanja chao. Mungu akawa anasubiri nao watimize nadhiri zao,Anania na mkewe wakashindwa kutoa kwa Bwana kama walivyo ahidi,mwisho wa siku kifo kikawafikia wote wawili..

Vivyo hivyo,usiwe mwepesi kuweka nadhiri kwa Bwana kama huwezi au hujiamini kwa sababu hii nadhiri unayoitoa itaenda kuwa tanzi maishani mwako siku zote...na sio kushindwa tu kutoa,hata kupitiliza muda wa kutoa Mungu hataka....

Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako.
AYU. 22:27

Ukimwomba Mungu kwa nadhiri anakusikia na anajibu maombi yako na pia anakusubiri na wewe utimize sehemu yako.

HANA mama yake samweli,ilibidi aweke nadhiri kwa Mungu ili Mungu akutane na haya zake. Alimwomba Mungu kuwa kama atakutana na haja zake,basi huyo mwanae atamuweka nyumban mwa Bwana milele...huu ni mfano mzuri kabisa wa nadhiri. UNAOMBA NA WEWE UNATOA na Mungu hajawah hata siku moja kutokujibu maombi ya nadhiri.

Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.
1 SAM. 1:11
(Mwanzo 28:20-22, NAHUMU 1:15)

Mistari yote hii inazungumzia kuhusu kutimiza nadhiri zako.

TATIZO

Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.   Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?
MHU. 5:4‭, ‬6

Usije ukasema uliweka nadhiri kwa bahati mbaya, Mungu atatumia iyo bahati mbaya yako kuiharibu kazi ya mikono yako...

NADHIRI INA FAIDA SANA

Tembelea
Tzworships.blogspot.com

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: