*PHM PUGU- MUSTAFA
MWL BRIGHT NYAHENDE
SOMO: *MWANAMKE ALIYEJITAMBUA NI NGUZO YA MAOMBI KWA KANISA* 
01/10/2019* 

Mwanamke amepewa neema na Mungu ya kuabudu na kuwa karibu na Mungu zaidi kuliko mwanaume katika asili ya binadamu.



Katika maombi kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi(YAHWEH) ,anapendezwa zaidi na unyenyekevu ambao unaweza elezea kama Kufunga,kulia, na kuomboleza.

 *Yoel 2:12* 
"Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;" 

Wanawake wengi wana uwezo wa kulia kwa kunyenyekea mbele za Mungu, wao kimaumbile wana mioyo ya uchungu,tofauti na mwanaume anaweza hata kufiwa na mzazi na hasilie.

 *Kuomboleza* .
Wanawake ni waombolezaji zaidi kuliko mwanaume, mwanamke anaweza pata msiba wa mtoto ikapita miezi hajarejea katika hali yake,Mungu anataka mtu anaeugua moyoni kwa ajili yake, amfate katika siri na kusema nae kwa kuugua moyoni,yaani kushuka na kunyenyekea zaidi.
 *Yoel 2:13* 
"Rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya."

Yaani Mungu anataka moyo ulioraruka ili aweze kughairi mabaya juu yako,moyo uliopondeka wenye kushuka kuhitaji msaada,hii neema anayo mwanamke zaidi kuliko wanaume.

 *ISAYA 22:12* 
"Siku hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, akawaita watu walie na kuomboleza, na kung'oa nywele zao, na kuvaa nguo zakunyenyekea.

Baadhi ya watu wanahisi mambo haya yalikua ya kale tu,lakini hata sasa kuna watumishi wanatenda haya na Mungu anawatumia kwa viwango vya juu.Kwa mtumishi  ni kawaida kuacha kitanda na kulala chini au madhabahuni,au kufunga siku 3 au  7 ,pasipo kula wala kuoga.Kwa Mungu yeye kadri unavyo pata neema ya kuukana mwili ndio unasogelea utukufu wa Mungu.

Unapokua kwenye maombi,kuna wakati unaona mambo aliyotenda Mungu juu yako,au kuna ugumu unakukabili hadi unatamani kulia lakini mwili unakwambia Mkurugenzi husilie hapa kanisani watu wanakuona,ila mwanamke yeye hajali wao hulia na kunyenyekea

 *Kufunga.* 
Wanawake wana uwezo wa kuvumilia njaa na kufunga zaidi kuliko wanaume,katika hali ya kawaida mwanamke anaweza kua na 2000 akatunza na kula na familia jioni,lakini wanaume wengi utamkuta kwenye kahawa,matunda nk.

 *Esta 4:16* 
"Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie." 

Esta anawatuma watu wasile wala kunywa,na wanatenda na kufanikiwa kwa kiwango cha juu zaidi.
Wanawake wengi wanatumiwa na shetani sana,lakini Mungu pia anaowake anao jivunia na wao ni nguzo kwa kuomba/Kanisa

 *Kutoka 15:20* 
"Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza." 
Japo Israel wote walishinda lakini wanawake ndio walio cheza na kusifu.

 *Methali 31:30* 
"Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa." 

Mwanamke aliyejitambua na kusimamia mapenzi ya Mungu huyo hakika utukufu wa Mungu unaonekana juu yake.
Ewe mama au binti uliye kanisani au nyumbani kwako,simama leo katika zamu yako uuone ukuu wa Mungu,Mungu anatamani akufanye kuwa nuru ya familia yako au huduma uliyopo.Dumu Leo katika kuomba ushuhudie wema wa Bwana.

 *@mwl nyahendebright*
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: