*PHM MAJOHE-VIWEGE / DAR ES SALAAM.*
*MWL NYAHENDE BRIGHT*
*SOMO:CORONA NA VITA YA UCHUMI KAMA VITA NYINGINE TUSITUMIE MBINU ZAO*
*


Toka awali niliwahi kusema haitupasi kufata taratibu na njia walizotumia mataifa ya ulaya kupambana na Corona,sisi tuna nafasi ya kuja na mbinu mbadala na kushinda.
Ni hatari sana kufata matakwa yao ili wakusaidie ..maana misaada hiyo ni kama gombo nje ni mitamu lakini kadri unavyo kula inakua michungu na kuumiza..

*Yeremia 17 (SUV)* 
⁵ Bwana asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha Bwana.
⁶ Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.

Ni bahati mbaya sana watu wengi wanafikiri Corona ilitokea kwa bahati mbaya maana inaonekana inaua watu wengi...

Miaka kadhaa iliyopita nikiwa mwanafunzi wa  "Diplomasia ya uchumi katika ngazi ya Post graduate " Niligundua Diplomasia ya uchumi ni kuisaidia nchi kufanikisha mipango yake ya kiuchumi na utawala chini ya mwamvuli wa Diplomasia.

Mataifa mengi yanatumia Diplomasia kama mwamvuli sio njia ya kufikia malengo yao ya kiuchumi.
Wanaweza kutumia njia yoyote lakini ikiwa chini ya mfuniko wa Diplomasia...

Unaona Leo watu wanavyo kufa katika vita duniani vita inaitwa ya wenyewe kwa wenyewe lakini wasuliishi wao ndio wafadhili wa vita izo lengo ni kupata faida ya mafuta,dhahabu,almasi au utawala kupitia nchi hizo wanazofadhili vita uku wakionyesha kusaidia kama Congo,Iraq,Syria..

 *WATU /MATAIFA WATAJIPENDA WENYEWE ZAIDI*
 *2TIMOTHEO 3 (SUV)* 
¹ Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari.
² Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi,
³ wasiowapenda wa kwao, wasiotaka kufanya suluhu, wasingiziaji, wasiojizuia, wakali, wasiopenda mema,

Uku kujipenda Leo unaona mataifa ni kama yanakusaidia lakini kumbe ndio unanyongwa.
Mwaka huu nilipata kusoma ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali katika halmashauri nikaona kuna miradi ya serikali imetoa hadi 15% tu ya bajeti iliyopanga lakini wahisani wametoa 100% ya bajeti yote ya mradi.
Kawaida utaona hawa watu wanatujali kuliko tunavyo jijari lakini ukweli ni kuwa miradi hiyo ya wahisani ,kuanzia vifaa mpaka wataalaam wanatoka kwao hivyo,pesa zile zinarudi kwao kupitia mishahara,na ununuzi wa vifaa ukichanganya na riba ya mikopo hiyo utakuta taifa lilikusaidia ndio lonanufaika hadi wewe ulipe deni umalize unakuta ule msasda ulishafika wakati wa kufanyiwa marekebisho yaani mda wa maangalizi umeisha,unaanza tena kukugharimu..

Viongozi duniani wakati mataifa yaliyoendelea yanapambana kupigania nchi zao kuendelea mbele sisi tunapambana kujipenda na familia zetu ,tunaingia mikataba ya hovyo ata kuleta mauti juu ya watu na watu wachache tu kunufaika.

 *CORONA NI SILAHA KAMA SILAHA NYINGINE.*
Mikakati ya mataifa au watu kutawala dunia yamepita hatua nyingi tu,kuanzia mapinduzi ya viwanda,fedha,vita za dunia hadi Leo..
Kumekua na silaha nyingi za kibaolojia ambazo zimeleta maafa makubwa kwa dunia lengo ni kutawala..
Kwa sasa kumekua na tetesi nyingi kuonyesha silaha nyingi za magonjwa ya kuangamiza ili taifa au taasisi kupata faida..
Ukimwi- ugonjwa huu Leo unaonekana ni hatari lakini unaonekana ulitoka maabara za Marekani kwa lengo la kutawala.

Zika- huu ni ugonjwa uliosumbua sana kama miaka 5 iliyopita kule Brazil lakini ulionekana umetoka maabara ya Microsoft umetengenezwa kama kirusi kwa lengo la kujipatia faida.

Cancer - Leo kumekua na aina nyingi za Cancer lakini nyingi zaidi zinaletwa na aina fulani ya vyakula ambavyo vinaonekana kama suluhisho kumbe ni tatizo kwa baadae...

Corona leo kumekua na tetesi nyingi imeanzia maabara za China,inaonekana kama Marumbano lakini ukweli ipo siku utajulikana..

Mikakati hii inaratibiwa kuzimu na watu wenye akili na ufahamu mkubwa wa kujua nyakati za kiroho na mambo ya kimwili,ndio maana mambo haya ukitafuta ushahidi wa kimwili(Scientific Evidence) utaipata asilimia 100% lakini ukweli ni kua uratibu wake unaratibiwa katika ulimwengu wa roho,ili kukamilisha yaliyotabiliwa kutimia.

 *WATU WA ROHONI UYATAMBUA HAYA* 
 *1WAKORINTHO 2:15* 
“Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.”

Ndio maana nyakati hizi Mungu anainua watu wake anao wapa hekima,akili,utawala na maarifa ya dunia ili kusimama na kuwasidia watu wake kutambua hila za shetani ,maana ni nyakati ambazo shetani anafanya kazi katikati ya wanadamu kwa kutumia maarifa yao.
Ndio maana huwa natamani sana,tukipata watalaam wanao mjua Mungu na kushinda hila za shetani ni rahisi kushinda.

 *HITIMISHO.* 
Mambo haya ni mambo ya kibinadamu kabisa lakini yanaongozwa na ulimwengu wa roho,ikiwa tutashuka na kutamani kusikia sauti ya Mungu pasipo kuongozwa na madaraka,elimu wala ujuzi ,vita hizi za maandalizi ya mfumo mpya wa dunia tutaweza kuzishinda na kupunguza madhara katika watu tunaowaongoza.
Mungu akubariki sana.

 *MATHAYO 18:19* 
“Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.

     *@mwl nyahendebright*
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: