Kuna wakati mtu anagundua kwamba nguvu za rohoni zimepungua sana. Hawezi kuomba tena, hawezi kusoma neno tena, hawezi kufunga tena. Kwamba amedumaa hakui tena bali anashuka kila siku.

Zipo sababu nyingi zinazoweza kusababisha jambo hili. Biblia imetuambia sababu kuu ni dhambi.

Kuna tabia ambazo unaweza kuwa unazifanya na hujui madhara yake na zikawa zinakunyonya nguvu taratibu bila wewe kujua. Dawa yake ni toba ya kweli. Kwa maana Mungu wetu ni mwema sana na yu tayari kusamehe (Zaburi 86:5).
.
.
MFANO: {WAAMUZI 16}
Samsoni ametajwa katika Waebrania 11:32 kama mfano mzuri kwetu. Kuna muda ambao kwa sababu ya dhambi ya Samsoni macho yake yaliondolewa na nywele zake pia na akapoteza nguvu zake. Alijaribu kuvunja vifungo kama alivyokuwa akifanya zamani lakini hakuwa na nguvu hiyo tena.
.
"Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha."
Waamuzi 16:20

Maadui zake wakamkamata. Hapa tunajifunza kwamba maadui zako hawakuwezi mpaka watakapofanikiwa kuharibu nguvu zako. Kwa hiyo ni jambo la msingi sana kujifunza jinsi ya kutunza nguvu za Mungu katika maisha yako.

Katika mapito hayo ya Samsoni alimgeukia Bwana na kuomba.

Akasema
.
"Samsoni akamwita Bwana, akasema, EE BWANA MUNGU, UNIKUMBUKE, NAKUOMBA, UKANITIE NGUVU, NAKUOMBA, MARA HII TU, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili."
Waamuzi 16:28

Mungu akasikia maombi ya Samsoni akamrejeshea nguvu maradufu.
.
"Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake."
Waamuzi 16:30


Kupitia mfano huu neno la Mungu linatifundisha namna ya kuomba pale tutakapo pungukiwa nguvu. Nikuomba kama Samsoni.

MAOMBI:
.
"EE BWANA MUNGU, UNIKUMBUKE, NAKUOMBA, UKANITIE NGUVU, NAKUOMBA, MARA HII TU. Katika jina la Yesu Kristo. Amina." Utaomba toba ya kweli alafu utaomba hayo maombi.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: