Bwana Yesu asifiwe sana sana. Leo tunaendelea tena na mada hii ya uumbaji hasa kutoka kwenye kitabu cha MWANZO katika kuichambua biblia.

Leo tutaangazia jambo la msingi sana kwenye maisha ya mwanadamu. Hili si lingine bali ni Asili ya mwanadamu na chimbuko lake.


Hivyo mistari yetu ya kusimamia leo itakuwa hii hapa
 (MWANZO 1:26-27)

Nanukuu
"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
MWA. 1:26‭-‬27 "

Mambo mazito sana yamezungumzwa hapa. Ngoja tuanze kuangazia moja badala ya lingine.

1.Mwanadamu aliumbwa,hakutokea tu. Yesu anathibitisha hili kwenye MARKO 10:6.
- Kuna mambo mengi sana sasa hivi ulimwenguni yanajaribu kukenguesha uumbaji wa Mungu. Kumekuwa na wachunguzi wengi wa mambo pamoja na wanasayansi mbali mbali hasa ma atheist (wapagani) ambao wanaamini kuwa mwanadamu aliibuka tu yaani alitokea tu na hakuumbwa. Biblia ni neno la Mungu na limethibitishwa mara 7 na kupimwa kwa moto kuwa linafaa kwa matumizi yetu,na neno hili ambalo linatoka kwa Mungu na ni Mungu mwenyewe leo linatupa historia nyingine kabisa kuwa mwanadamu aliumbwa tofauti na wanasayansi na wapagani wanavyodai. (Ipo siku nitakuja kuelezea kwa undani juu ya swala hili zito).

2.Jambo la pili na lamuhimu sana ni hili.
MWANADAMU AMEUMBWA KWA MFANANO SAWA NA MUNGU ,aneumbwa kwa sura na mfano wa Mungu mwenyewe. 

Mungu ni Roho na mtu ni Roho. Usichanganye hapa.

Mungu alianza kumuumba MTU na sio MWANADAMU.
yule mtu aliyemuumba ndiye biblia inaemsema kuwa anafana na Mungu na yupo kama Mungu (kiroho). Ila baadae Mungu akamfanyie yule mtu nyumba ya nje inayoitwa mwili,yule mtu akaanza kuitwa mwanadamu.

Kwa hiyo mwanadamu ni Muunganiko wa vitu vitatu.
MWILI,NAFSI NA ROHO. Kati ya hivi vitatu,iyo roho ndiyo inayofanana na Mungu wetu.

Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
1 THE. 5:23 

Andiko hili linathibitisha utatu wa mwanadamu.

a) Roho ni sehemu ya mwanadamu yenye kujua na yenye ufahamu juu ya Mungu. The part of man that KNOWS. 1 kolosai 2:11

b) NAFSI ni sehemu ya mwanadamu yenye ufahamu na akili. Hisia zote ,akili,maamuzi hayakai rohoni bali kwenye nafsi. Kuna muda biblia inachanganya kati ya nafsi na moyo.

C)MWILI ndiyo sehemu pekee iliyotofauti na roho na nafsi. Mwili ndio unaokufa. Nafsi na Roho hazifi.

Katika somo UTAMBUE UFALME WA MUNGU nimeongelea sana juu ya mwili na thamani ya mwili wako.

Huu ndio muunganiko wa mwanadamu.

Pia ni lazima ujue kuwa,mwanadamu pekee ndiye aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mimea na wanyama hawakuumbwa kwa mfano wa Mungu. Ukisoma sehemu ya pili ya somo hili utaona jinsi mimea ilivyotokea.. "MUNGU akasema nchi itoe mimea kwa aina yake" lakini ilipokuja kwenye swala la kukuumba wewe,Mungu alijifananisha na wewe..

Kwahiyo usije ukajidharau hata kidogo wala usimuache mtu audharau uwanadamu wako,wewe ni final master piece of God. Katika vitu alivyoviumba Mungu ,basi wewe umevizidi vyote.

👉🏽pia kuna aina mbili za uumbaji zinazoonekana kwenye kitabu cha mwanzo (tutazungumzia mbeleni)

Ila kwenye mstari wa 27..Mungu anasema alimuumba mwanamke na mwanaume, hao wote aliwaumba.

Mwanaume ni Adamu,je mwanamke ni nani???

Bila shaka utasema EVA na kweli ni EVA. ila kuna nadharia nyingi hapa ambazo mimi naona sio za kimungu kabisa kuhusu swala hili.

Yote haya na mengine tutayaangalia kwenye sehemu ya nne.
Mungu akubariki sana snaa

Tzworships.blogspot.com 
By Maestrorabbon
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: