Kwa mfano jiulize... mwanaume asipooa anakuwa amefeli maisha?au anakuwa anashida? Kama hajafeli maisha je huyo mwanamke ataolewa na nani kama mwanaume haoi? Sasa kwanini useme mwanamke kafeli maisha🌚🌚



Ok biblical references.
👉paulo mtume hakuoa (kila mtu atahukumiwa sawa na injiri ya paulo)

Inamaana maandiko ya paulo kwenye agano jipya ni yamuhimu sana....

Huyu paulo hakuoa na wala hakuwa na mwanamke wa aina yeyote.

Ushauri wake ni huu hapa.

Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo(wasioe na wasiolewe). Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa. Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo. Ndivyo ninavyoagiza katika makanisa yote.
1 KOR. 7:8‭-‬9‭, ‬17

Je,kuoa au kuolewa ni lazima?? Je,uliumbwa ili uje kuolewa au kuoa?? Kama uliumbea kwa ajiri ya ndoa,kwanini Paulo anashauri usiingie kwenye ndoa??????

Jibu ni hapana... Kwenye katiba yetu (bible)
Kusudi la kuubwa lipo wazi kabisa.

MWANZO 1:26
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
MWA. 1:26

KUMILIKI NA KUTAWALA DUNIA NDIO KUSUDI LA KUUMBWA WEWE...

Just imagine...why Mungu akuumbe ili uwe na ndoa? Yeye anafaidika nini???😂

Hope umenielewa point yangu kidogo.

Tuendelee...

Ndoa Sio primary purpose ya mwanadamu.
Mungu alituumba kwa ajiri yake mwenyewe (ibada).
Tumeumbwa kwa ajiri ya kufanya ibada na si vinginevyo... Mambo mengine yote ambayo tunayapata DUNIANI ni ili yaturahisishie kifanya ibada.

Moyo wenye amani na moyo uliotilia ndio moyo wenye uwezo wa kufanya ibada.

Kwa hiyo..Mungu alimuumbia mazingira mazuri mwanadamu,ikiwemo NDOA,ili aweze kumuabudu Mungu.

So why God created us?
Ni maelezo marefu sana yapo hapa...but nitakupa kwa ufupi ...

Kusudi la Mungu Mungu kumuumba mwanadamu linasababishwa na Ugomvi uliotokea kati yake na shetani....shetani ndiye aliyekuwa mbeba upako na utukufu wa Mungu...baada ya kutenda dhambi,Mungu ikabidi atafute mbadala wa shetani....

In the recreated earth, God’s purpose is to have man on earth reflecting His image and having dominion over the earth under His sovereignty.

This is the reason kwanini Yesu alikuja. Alikuja ili kutafuta watu ambao wataziba pengo la shetani,watu ambao watamwabudu Mungu kiukweli....hii ndio primary purpose.

Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.
YN. 4:23

So..Ili Mungu apate waabuduo halisi thats why alitumia siku 6 kuandaa mazingira ya mwandamu,ili akikaa asiwe na tabu awaze kumuabudu Mungu tu..

Kwahiyo ukimuabudu Mungu,hayo mengine kama Mungu anataka uwe nayo utayapata ,ila kama hayapo kwenye hatima yako hutapata..


Ndoa,utajiri,mafanikio,afya njema...vyote hivi ni kwa ajiri ya utukufu wa Mungu...

In case of ndoa ni maamuzi. Soma mwanzo mpaka ufunuo ,hamna sehemu panaposema unatakiwa uoe au uolewe...ila biblia mwanzo mpaka mwisho inasisitiza TUWE WATAKATIFU

Mungu haitaj ndoa yako,he needs u to serve him


KWANINI MUNGU ALITUUMBA NA KWANINI ALIUMBA NDOA NA VITU VINGINE?

Ni kwa ajiri ya fellowship na yeye.

Kwa maana macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake.
2 NYA. 16:9

Thats why God created you.

Mwanadamu anatamaa kwa sababu ya mwili wake. So,kama hutaki kutenda dhambi ingia kwenye ndoa...kama unajiamini basi kaa kama ulivyo..yote yapo mikononi mwako
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: