Bwana Yesu asifiwe. Leo tena katika kuichambua biblia,tunaendelea kusoma na kujifunza kutoka katika kitabu cha MWANZO na leo tutajikita kwa ufupi kwenye  MWANZO 1:3-25


Katika mistari hii nitajaribu kukuonyesha mambo yamsingi kabisa ambayo ni nguzo kwenye maisha yetu.

Leo ngoja tuanze kuangalia kipengele hiki kimoja cha muhimu ambacho tulikiacha kama kipolo kipindi kilichopita...

Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
MWA. 1:2 

And the earth was without form(ukiwa), and void(utupu); and darkness(giza) was upon the face of the deep. And the Spirit of God moved upon the face of the waters.
Genesis 1:2 

Mstari wa muhimu sana huu kwenye historia ya mwanadamu na dunia kiujumla. Fuatana nami tunavyoenda kuchambua mstari huu.

Hapu juu nimeweka maandiko kwa kiingereza na kiswahili. Huu ni mwanzo kabisa wa kila kitu,ni mwanzo wa mbingu na nchi. Ni mistari ambayo inaonyesha dunia ilivyoumbwa na kila kitu kilivyokuwa kabla leo. 

Mungu ni alpha na omega...yaani alikuwako hata kabla ya haya hayajakuwapo,wewe na mimi na babu zetu hatupo ila Mungu alikuwepo.... 

Sasa haya maandiko  mafupi yanatuonyesha kitu cha msingi,kuwa Baada ya Mungu kuumba kila kitu,dunia inaonekana ikiwa na giza na muundo tofauti.

Twende taratibu hapa.
Mwanzo 1:1  
Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.

Yani hapa alikiwa kashamaliza kuumba kila kitu. 
Hii ni description fupi tu ila inamaanisha Mungu aliumba vyote vinavyoonekana ndani na nje ya dunia tayari....

Hii nchi aliyoiumba ndiyo ilikuwa ukiwa na utupu🤩

Swali..je Mungu aliumba dunia ambayo inaukiwa(kiingereza imeandika WITHOUT FORM) yaani ikimaanisha kuwa mwanzoni ilikiwa ipo vizuri ila sasahivi imevurugika au imeharibika. Sijui tunaenda pamoja?

Mungu ni omniscient yaani anajua kila kitu,ni Mungu mwenye hekima na maarifa yote. Kwa mantiki hii hawezi kuumba kitu ambacho kipo formless,hakina shepu yaani kimevurugika...lazima kuna jambo lilitokea hapa ambalo lilifanya dunia iwe  WITHOUT FORM. 

Pia tunaona dunia ilikuwa ukiwa (without form) na giza. Nini maana ya giza basi? Giza ni ishara ya uharibifu au kutokuwepo kwa hekima ya Mungu

Tusome kidogo hapa chini ili tuone maana halisi ya giza.

Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
YN. 1:4‭-‬5 

Swali na hili giza pia lilitoka wapi? Giza ni ishara ya uharibifu..embu ngoja tujarib kujib haya maswali

Wataalami wa theolojia na scholars wanasema kuwa uharibifu huu wa dunia pamoja na hili giza vinasadikika kuhusiana sana na hukumu au vita ya kale iliyopiganwa mbinguni kati ya shetani na majeshi ya Mungu.

Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
UFU. 12:7‭-‬9 

Yohana anaeleza wazi kabisa ni wapi shetani alitupwa...ukumbuke hii vita imepiganwa katikati kabla ya mwanadamu hajaumbwa.

Mstari wa chini pia unzidi kuweka wazi hili
Na joka yule alipoona ya kuwa ametupwa katika nchi, alimwudhi mwanamke yule aliyemzaa mtoto mwanamume.
UFU. 12:13 

Kabla ya kufika kwenye hitimisho tutazame jambo jingine pia

(EZEKIEL 28:12-15,ISAYA 14:9-15)

Kwenye mistari hii utaona  jinsi Mungu anavyomuelezea shetani,lakini ukisoma kwa makini mwishoni mwa mistari hii utaona Mungu anasema "LAKINI NILIKUTUPA MPAKA NCHI AU DUNIANI"

Kwahiyo ni dhahiri shetani alitupwa mpaka duniani na wanatheolojia wanahusisha hii vita na uharibifu wa dunia unaoonekana kwenye mwanzo 1:2.

Kwahiyo kwenye mstari wa 3,Mungu anaposema iwe NURU, inaamana alikuwa anaendelea na kazi ya kuirekebisha dunia...

HIVI NDIVYO THEOLOGY NA SCHOLARS WA BIBLIA WANAVYOELEZEA HILI SWALA.. wewe unaelezeaje???

Mungu akasema "iwe nuru ,ikawa Nuru"

Kitu cha kwanza Mungu kukiumba baada ya ulimwengu ni Nuru. Baada tu ya kumaliza kazi ya uumbaji wa mbingu na nchi,Mungu akaumba nuru. Vyote vilivyofanywa baada ya hapa vilifanywa ndani ya Nuru hii. Nuru hii ilikuwa haitegemei jua wala mwezi,nuru hii ilikuwa haitegemei kitu chochote,bali Yesu kristo mwenyewe ambaye ndiye mjenzi na muumbaji mkuu ndiye aliyekuwa Nuru ya ulimwengu.

Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.
YN. 1:5 

Ile nuru ambayo ni Yesu ndiyo iliyoondoa giza. Hii inamaana gani?

1. Jua lilikuja kuumbwa baadae sana,lakini bado Nuru ilikuwepo na usiku na mchana ulikiwepo..iliwezekanaje hii? Jua sio chanzo cha Nuru,jua ni chanzo cha mwanga tu. Jua ni kanuni ya kimwili ya kutupa mwanga,ila nuru halisi ipo ambayo haitegemei kanuni za kimwili,haitegemei mwangaza wa jua.

Hii ndiyo maana ya ulimwengu wa roho na wa mwili.. ulimwengu wa roho ni ulimwengu dhahiri ila hauonekani kwa macho ya nyama. Chochote unachoona kinatendeka au kinatokea duniani ujue chanzo chake ni rohoni... Tunasema mvua hainyeshi bila misitu,ila baada ya miaka mitatu na nusu Eliya alileta mvua huku misitu wala unyevu kwenye anga haupo... misitu ni kanuni ya kimwili tu,ila kwenye ulimwengu wa roho mvua haitegemei misitu. Vile vile Nuru hii inayozungumziwa hapa haitegemei jua wala mwezi,ila jua ni kanuni ya kimwili tu ya kuleta mwangaza. Nuru halisi ni Yesu.

2. Kabla ya kufanya lolote Mungu anakaribisha kwanza nuru (Uwepo wa Yesu). Hivyo hivyo na sisi,kwenye haya maisha kabla ya kufanya lolote lazima tuikaribishe kwanza nuru kwa sababu hii nuru ambayo ndiyo Yesu kristo ndiyo inayoondoa giza kwenye maisha yetu..Ukiikaribisha hii Nuru,ndipo ufanye mambo mengine...YESU NDIYE NURU YA ULIMWENGU,NDIYE NYOTA YA ASUBUHI,NDIYE MWANA WA ASUBUHI NA NDIYE MWANGAZA WA ULIMWENGU

Natamani kuendelea zaidi lakini naomba niishie hapa,nitaendelea tena siku ijayo.

Mungu awabariki sana

By
Maestrorabbon
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: