Bwana Yesu asifiwe,leo tunaanza uchambuzi wa kitabu cha MWANZO na hasa mstari wa kwanza na wa pili.

👉🏽Mwanzo 1:1-2

"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
MWA. 1:1‭-‬2 "

Haya ndiyo maandiko ya msingi ya siku ya leo. Lakini kabla ya kuanza kuchimba kiundani,kwanza tuanze kuangalia mwangaza wa kihistoria.

KITABU CHA MWANZO (GENESIS).

Kama neno lilivyo MWANZO, na huu ndio mwanzo wa historia ya mwanadamu na dunia kwa ujumla.

GENESIS au MWANZO ndio mwanzo wa mambo yote ikiwemo
..muda,maisha,dhambi na ukombozi au redemption..

Pia kwenye kitabu cha mwanzo tunaweza kuona muumganiko wa matukio makubwa manne kwenye historia ya mwanadamu ambayo ni
1. Uumbaji
2.Anguko la mwanadamu
3. Gharika
4. Kutawanyika kwa mataifa.

Haya ndiyo matukio makubwa manne ambayo tunayadiscus kwa undani kabisa.

Pia ni mwanzo wa historia ya wazalendo wa Mungu wanne,watu ambao mpaka Mungu akaamua kujiita kwa majina yao nao ni IBRAHIMU, ISAKA,YAKOBO NA YUSUF.

Kitabu hiki cha mwanzo kimeandikwa na nabii MUSSA na ndio msingi hasa wa vitabu vyote vya biblia...Agano la kale limegawanyika kwenye mafungo matatu

1. Foundational books
Hivi ni vitabu vya msingi ambavyo lazima uvijue kabla ya kusoma biblia. Ili uweze kuifahamu biblia vizuri,lazima kwanza ujue hivi vitabu..kwa lugha ya kitheolojia vinaitwa PENTATEUCH.

Vitabu hivi vipo vitano.

MWANZO
KUTOKA
,WALAWI,
HESABU NA KUMBUKUMBU.

Hivi ndivyo vitabu vya msingi ama foundational books.

Vitabu hivi vinatoa maelekezo ya namna ya kuishi na utaratibu wa kuishi. Kwahiyo vimewekwa maalumu kwa ajir ya kutoa malekezo juu ya watu wamungu walivyopaswa kuishi. Baada ya kumbukumbu la torati,utaanza kuona namna ya historia ilivyokuwa inaendelea na utaona ni namna gani vitabu hivi vya msingi vilikuwa vinatumika.

kwahiyo kitabu cha mwanzo ni kitabu cha msingi sana ,na ndio nguzo ya vitabu vyote kwenye bibilia,katika kitabu cha mwanzo  kinatuonyesha mwanzo kabisa utabili wakuja kwa. messia(3:15), kupitiaukoo wa seti(4;25), mtoto wa shem(9:27), ukoo wa abraham (12:3), isaka(21;12), na yakobo (25:23),na kutoka kwenye ukoo wa yuda(49:10)

kitabu cha mwanzo ndicho kitabu ambacho kinachukua mda mwingi  kuliko vitabu vyote 

kitabu hichi kinaanza kwa neno 'HAPO  MWANZO' na kinaishia  na neno 'MAKABURI YA MISRI' hii inamanisha mwanadamu aliyeumbwa ili asife ,atakufa kwa sababu ya dhambi.

kwamaana hiyo msomaji wa kitabu hiki anakuwa na shauku  yakutaka kujua safari hii ya ukombozi inaishia wapi.

MWANZO 1:1
Hapa tunaanza kuona jinsi Mungu alivyoumba vitu kutoka kwenye utupu. Kwenye maandiko haya tutagundua kuwa dunia imeumbwa na ina umri wa miaka elfu kadhaa na sio milioni kadhaa kama wanavyosema wanasayansi.

TUINGIE NDANI SASA

Mwanzo 1:1
"Hapo mwanzo" hili ndilo neno la kwanza kabisa kwenye biblia, kwa kiingereza linaitwa IN THE BEGINNING yaani mwanzo wa kila kitu kilicho hai na kisicho hai.

Mstari huu unaonyesha ukuu wa Mungu,kuwa japokuwa mwanzo kabisa kulikiwa hamna kitu,lakini yeye alikuwepo kabla ya huo mwanzo. Kwahiyo unaposema hapo mwanzo uwe na unajua kuwa ndio mwanzo wa kila kitu kasoro Mungu. Mungu ndiye huo mwanzo kwa hiyo hawezi kuzuiwa na muda... Mungu ndiye mwanzo na mwisho nikimaanisha mwanzo na mwisho vinaishi ndani yake. 
(ZABURI 90:2 - KABLA HAIJAZALIWA MILIMA,WALA HUJAIUMBA DUNIA , NA TANGU MILELE HATA KILELE WEWE ULIKUWEPO)

"MUNGU ALIUMBA(CREATED"

Sentensi inayofuata ndiyo hiyo,inaonyesha Mungu anaanza uumbaji.

Neno Mungu linalotumika kwenye hii sentensi ni neno ELOHIM. neno ELOHIM  ni neno la kiebrani ambalo lipo kwenye uwingi likimaanisha Mwenye mamlaka na mwenye Nguvu sanaa. Pia kwa sababu neno hili lipo kwenye wingi linatupa mwangu kuwa hii kazi ya uumbajo haikufanywa na  mmoja bali na  wengi na hapa ni mwanzo kabisa ya ule tunaoita utatu wa Mungu (God's trinity) yaani Mungu baba m,mwana na Mungu Roho mtakatifu. 


Kwa hiyo nafsi zote hizi tatu zilihusika kwenye uumbaji wa mbingu na dunia na kila kitu.

"MUNGU ALIZIUMBA"
Tuangalie upande mwingine wa neno ALIZIUMBA. Neno hili limetokana na neno kwa kingereza linamaanisha CREATED. Neno created ni tofauti na neno made. Kucreate/kuumba maana yake kutoka kwenye sifuriii. Mungu aliumba kila kitu kutoka kwenye hakuna. Anapoumba dunia hakuwa na lori la mchanga wala hakuwa na mbao wala simenti,alitumia neno tu. Kwahiyo ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kuumba na sio mwanadamu. Mwanadamu hawezi kuumba ila anatengeneza. Kila kitu anachofanya mwanadamu sasa hivi kinatokana na kazi ya Mungu aliyoifanya tangu mwanzo,kwahiyo mwanadamu anatengemeza bali Mungu ndiye muumbaji.

"Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono;
MDO 17:24 "

Mwanadamu anauwezo wa kutibu ila sio kuponya,mwenye uwezo wa kuponya ni Mungu tu na ndiye mwenye nguvu za kuhuisha kwa sababu yeye ndiye muumbaji wa mwanzo,alivyoumba hakuhitaji kitu chochote cha kumsaidia ila neno lake tu (Yesu kristo).

Pia kwenye andiko hili la MWANZO 1:1 utagundua kuwa hii ilikuwa ilikuwa ndiyo mara ya kwanza Mungu anaumba orijino dunia,dunia kwa mara ya kwanza,...ila mstari wa 2 kuna jambo tutaliona ambalo tutalizungumzia kwa undani sana kwa sababu limebeba maana kubwa sana.

"Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya
 Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
MWA. 1:2 "

Kuna mambo manne hapa ya kuangalia
1.ukiwa
2.utupu
3.giza
4. Roho wa Bwana.

Ijumaa tutazungumzia hapa kwa undani zaidi.

Mungu awabariki sana

By Maestrorabbon 
Tzworships.blogspot.com
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: