๐Ÿ’ฅBIBLE STUDY๐Ÿ’ฅ
Program: Christian theology & systemic theology.
(Kijana Mkristo-KM)

Sehemu 3
--------

Bwana Yesu asifiwe sana.
Kama tulivyosema kuwa leo tutaendelea na kuangalia wanatheolojia wachache wa muhimu na mchango wao kwenye msingo wa kanisa.

1. JUSTIN MARTYR (c.100- c. 165)

Huyu Justin yamkini ndiye apologist mkubwa zaidi kuwahi kutokea. Kama unakumbuka nilikwambia kwamba,hawa apologists ni watu ambao walikuwa na kazi ya kutetea wokovu kipindi hicho cha nyuma ulipokuwa unapigwa vita na wapagani. Kwhiyo katika watu ambao waliotetea vizuri imani, basi justin ni mmoja wao.

Huyu alikuwa kipindi cha karne ya 2. Alizaliwa palestina lakin maisha yake kwa kiasi kikubwa aliisha Roma ambapo alipata umaarufu kama Mwalimu wa kikristo.

Katika kitabu chake cha kwanza kinachiitwa "First apology" justin aliongea jambo la ajabu na la kustaajabisha sana. Nanukuu

"UKWELI WA UKRISTO, UPO KWENYE VYANZO VIKUBWA VYA KIPAGANI" yaaniiii

"Traces of Christian truth were to be found in Great pagan sources "

Inashangaza e??

Pia akaja kuandika andiko au doctrine inayoitwa SEED BEARING WORD ambapo humo alisema kwamba

MUNGU ALIANDAA NJIA YA KUJIFUNUA KWA MARA YA MWISHO KUPITIA YESU

Utaelewa zaidi mbeleni.


2. IRENAEUS OF LYONS (c.130-c.200)

Huyu alizaliwa SMYRAN (uturuki) lakini naye akakulia mjini Roma. Akaja kuwa askofu ndani ya Roma mwaka 178 na kufariki miaka miwili baadae aliwa askofu.

๐Ÿ•ท️Irenaeus anakumchango mkubwa sana na anakumbukwa mno hasa kwenye utetezi wake wa CHRISTIAN ORTHODOXY dhidi ya GNOSTICIM (waabudu miungu)

Najua unakumbuka niliwahi kukuelezea juu ya Orthodoxy kuwa ni imani ya kikristo inayoamini Mungu mmoja,utatu mtakatifu,Yesu Kristo kufa na kufufuka kwake.

3. TERTULLIAN (C.160-225).

Huyu alikuwa mpagani kutoka afrika kaskazini ambaye aliamua kuja kuwa mkristo akiwa na miaka 30. Wengi wanasema huyu ndiye Baba wa Theolojia ya kilatin au Latin theology.

๐Ÿ•ท️Alitetea sana sana Muunganiko wa agano la kale na agano jipya. Kulikuwa na kundi la watu wanaitwa MARCION ambao wao wanasema kuwa agano la kale na agano jipya ni miungu miwili tofauti. Hii ni dhana ambayo imani yake inatutoa Kwenye imani ya kristo.

๐Ÿ•ท️Tertullian ndiye aliyekuwa kwenye midahalo na hawa watu na kuwafundisha kuwa Mungu wa agani jipya ndiye Mungu wa agano la kale. Kwa kufanya hivyo, huyu ndiye alikiwa mtu wa kwanza kuweka Msingi wa maandiko ya utatu mtakatifu(doctrine of The trinity).

Tutakuja kuona yote haya.

4. ATHANASIUS (C.293-C. 373).

Athanasius akiwa na miaka 20 tu aliandika treaties juu ya INCARNATION OF THE WORD au NENO KUFANYWA MWILI.

๐Ÿ•ท️Hizi treaties ambazo alikuwa anaandika juu ya swala hili zilianza kujenga imani kwa watu ya kwamba Mungu alichukua umbo la mwanadamu kupitia mwanadamu Yesu kristo. Maandiko ya Athanasius yalikwa na mchango mkubwa sana kwenye maandiko ya bwana Arius ambaye nayeye alikuwa anatetea hoja hii ya Mungu kuwa mwanadamu. Huyu arius alisema kwambaaa, kama Yesu hakuwa Mungu kamili au Full God, basi majanga yafuatayo yangetokea

a) Ingekuwa Ngumu kwa Mungu kumuokoa mwanadamu kwa sababu haiwezekani kiumbe kuokoa kiumbe kingine.

b) Kama Yesu hakuwa Mungu,basi wakristo wote wanakufuru kwa sababu Tangu enzi zake za kwenye biblia, Yesu amekuwa akiabudiwa na kupelekewa maombi. Hoja hi ilikuwa ngumu sana kwa wapinzani kuijibu.

5. THE CAPPADOCIAN FATHERS.

Kuna hawa sasa wanaoitwa Cappadocians. Jina hili linatumika sana kwenye theolojia likuhusisha wanatheolojia wakubwa watatu (ndugu wawili wa kiume na rafiki yao) ndani ya kanisa la kigiriki mjini Cappadocia.

Wanatheolojia hawa watatu ni.
- BASIL THE GREAT (Huyu alikuwa askofu wa Kaisaria na kaka mkubwa wa Gregory wa nyssa)

- Gregory of nyssa (huyu alikuwa askofu wa Nyssa)
- Gregory wa Nazianzus ambaye alikuwa askofu wa Sasima na baadae Constantinople.

Waandishi hawa wote watatu wana umuhimu wao wa kipekee sana japokuwa kwa umoja wao waliweza kuweka

MSINGI WA MAANDIKO YA UTATU MTAKATIFU (DOCTRINE OF THE TRINITY)

๐Ÿ•ท️Huwezi kuzungumzia maandiko ya Roho mtakatifu na utatu mtakatifu bila kujifunza habari za Hawa watu watatu.

Tuangalie kiundani.
-----------------###---------------------

Kuna mtu wa muhimu sana apa nataka tumalize nae kwa leo. Mtu huyu anaitwa

AUGUSTINE OF HIPPO
------------------####--------------------

Alizaliwa mwaka 353 na alifariki mwaka 430. Wengi wanaamini kuwa huyu ndiye mtu mwenye mchango mkubwa sana kwenye kanisa la kikristo kutokana na historia yake ndefu.

๐Ÿ•ท️Augustine alivutiwa na mahubiri ya kristo baada ya kuhubiriwa na askofu ambrose akiwa mjini milani. Augustine baada ya hapo akarudi kaskazin mwa afrika ndani ya mji wa hippo (algeria kwa sasa) ambapo alikuwa askofu huko. Katika miaka yake 35 ya mwisho,Augustine alishuhudia changamoto nyingi sana ambazo zilikuja kuwa na umuhimu kwenye kulijenga kanisa la kikristo na mchango wa Augustine kwenye kuweka sawa changamoto hizi ulikuwa wa muhimu sana sana.

๐Ÿ•ท️Sasa, mchango mkubwa wa Augustine ulikuwa kwenye kukuza Theology kutoka kuwa kama chombo cha ubishani na kuwa KAMA SOMO LA DARASANI (ACADEMIC DISCIPLINE).

KATIKA KUSOMA KWENTU THEOLOJIA, TUTAMSOMA SANA AUGUSTINE ILI TUJUE MAWAZO YAKE YALIKUWA VIPI.

๐Ÿ•ท️Kwahiyo, Katika kipindi chote icho, Augustine aliweza kutengeneza mifumo mizuri hasa kwenye maeneo haya matatu.

- Doctrine of church and sacrament (maandiko ya kanisa na ubatizo)
- Doctrine of Grace (maandiko ya neema)
- Doctrine of trinity( maandiko ya utatu).

๐Ÿ•ท️Lakini cha kushangaza na cha ajabu, Augustine hakuwahi kuzungumzia swala la CHRISTOLOGY ama maandiko ya kristo.

Christology ni somo maalumu linalohusu Utu wa Yesu (Doctrine of Person of Christ).
-----------------####---------------'---

๐Ÿ•ท️Leo nimejarbu kukuletea kwa ufupi juu ya maisha ya watu wa muhimu sana kwenye THEOLOGY. Natumaini unaelewa maana ya neno THEOLOGY sasa.

Kipindi kijacho tutaona juu ya

๐ŸŒค️KEY THEOLOGIAN DEBATES.

Cc: KIJANA MKRISTO
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: