Miaka iliyopita kidogo niliwahi kusoma kitabu cha mwandishi aliyejaribu kuelezea kijiografia kwa kutumia vielelezo vya biblia na uhalisia wa kimazingira kuonyesha Tanzania yamkini ndipo hasa Edeni ilipokua.


Lakini Leo ninaangazia neema ya Mungu iliyo juu ya nchi hii,ambayo Mungu akuwahi kuwaacha watu wake waangamie hata siku moja katika hasira yake.Kama ilivyokua Edeni ambapo Mungu aliwapenda wanadamu wala hakutaka uovu uonekane kwao na wala hakuruhusu majanga kuwaangamiza.

Hasira ya Mungu juu ya wanadamu ilidhihirishwa na mauti kubwa iliyowapata watu ambayo Mungu aliruhusu iwapate watu kwa Tauni,Vita au kuruhusu nzige ili kupata njaa ilietayo maangamizi.

*Zaburi 106:29*
“Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia.”
Biblia inaonyesha tauni ambayo ndio leo tunaita magonjwa ya milipuko yasiyo na tabia ili ni matokeo ya dhambi.

Hiyo ilikua adhabu ya kwanza lakini pia nzige uletwa na hasira ya Mungu.

*Amos 7*
¹ Haya ndiyo aliyonionyesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme.
² Ikawa, nzige walipokwisha kula majani ya nchi, ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, samehe, nakusihi; Yakobo atasimamaje? Kwa maana ni mdogo.

Majanga makubwa kama matetemeko,magonjwa yasiyo na tiba, nzige ilionekana ni pigo toka kwa Mungu.
Japo hapo tunapishana na wataalamu wa Leo wao watakwambia ni " *natural population control"*
Wakiwa na maana popote palipo na watu wengi dunia inatabia ya kuruhusu majanga ili kupunguza wingi wa watu waendane na eneo walilopo.

Katika somo nita onyesha ambavyo majanga haya ya milipuko yalikuwepo na yalisababishwa hasa na nini..

*@mwl Nyahendebright*
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: