Hii ni sehemu ya 5 na ya mwisho ya somo letu la ufalme wa Mungu, na sehemu hii ya 5 itazungumzia INCARNATION OF JESUS (Yesu kufanyika mwili).

Kabla ya kuendelea huko ningependa nikukumbushe nyuma kidogo.

1. Mungu ni Roho
2. Mtu ni roho
3. Mwanadamu ni roho na mwili+nafsi

Hapo mwanzo Mungu alipoziumba mbingu na nchi pamoja ndipo aliposema NA TUMFANYE MTU (ROHO) KWA MFANO WETU ILI AKATAWALE(HAVE DOMINIONS OVER THE EARTH).

Aliposema hivyo alikuwa anampa mtu utawala wakisheria (legal authority) wa kumiliki na kutawala dunia...

Mungu mwenyewe akajitoa kwenye huo utawala (PALE ALIPOSEMA TUMFANYE MTU AKATAWALE, YEYE ALIJITOA KWENYE HUO UMILIKI)

Kwahiyo,kiumbe chenye mwili ndicho kilikuwa na uhalali wa kutawala na kufanya lolote duniani
ROHO YEYOTE HAINA UHALALI WA KUWEPO HAPA DUNIANI, WALA HAINA UWEZO WA KUFANYA JAMBO LOLOTE BILA KUTUMIA MWILI.

Tukaona jinsi ambavyo adamu alianguka pale eden ,shetani alivyomdanganya na kwanini Mungu hakuweza kumzuia shetani kwenye hilo.

Sasa,Kwanini MUNGU aliamua kuwa mwanadamu?

Kuna sababu kuu mbili za kwanini Mungu aliamua kuwa mwanadamu.

1. Mungu asingeweza kujihusisha na maswala ya wanadamu kwa sababu yeye sio mwanadamu (hana mwili).

2. Sababu ya msingi kabisa ni hii hapa. MUNGU NI MUNGU WA HAKI (JUST GOD).

Tuangalie baadhi ya maandiko
(Kumbukumbu 1:17, zaburi 9:16) utaona kwa jinsi gani Mungu ni Mungu wa haki. He is a just God.

Ok ipo hivi,Mungu sio mtakatifu,ila utakatifu ndio uungo wenyewe. Yani Mungu hana utakatifu,bali yeye ndio huo utakatifu. Kama ilivyo kuwa ,Mungu hana upendo ila yeye ndiye pendo . Kwa sababu hii Mungu hawezi kudanganya..he is holly.

Kwa sababu yeye ndio utakatifu,yeye ni Mungu wa haki,basi kila anachokisema lazima ahakikishe kinatimia. Neno lolote linalotoka kwa Mungu ni sheria,na kwa sababu ni sheria basi lazima litakuwa na hukumu...twende taratibu hapa...hii ndiyo concept ya muhimu itakayokufanya uelewe nini maana ya REINCARNATION OF JESUS...Yesu kufanyika mwili.

Sasa MUNGU anaanza kazi.
..anamuumba mtu na kumuweka bustani ya edeni
...anambariki yule mtu
...anampa kazi za kufanya atakapokuwa pale bustaninii
...kisha Mungu akaanza kusema/kuweka sheria (shida ikaanza).

Mungu akamwambia mwanadamu atii amri zake,ale kila kitu ila asiguse mti fulani,kwa sababu akigusa tu ATAKUFA. Mungu akajifunga kwenye maneno yake.

Mungu akajiahidi mwenyewe kuwa atamuua mwanadamu kama hatatii amri zake. Kumbe Mungu ndiye aliyetengeneza kifo na sio shetani.

"Kifo kilikuwepo ila kilikuwa hakina nguvu. Na Mungu alipoumba kila kitu ,kama unakumbuka alisema kila kitu ni Safi (kikiwemo kifo)."

Kwa hiyo Mungu akajiahidi mwenyewe kumuua mwanadamu. Mwanadamu alipovunja amri ya Mungu, Mungu hakuwa na namna ila kuhakikisha kile alichokisema kinatimia,na hapa ndipo kifo kikapata upenyo,kifo kikaingi rasmi kazini. (Ili Mungu aendelee kuwa mtakatifu,ilikuwa lazima atimize hili).

Utakachopanda lazima uvune, huu ndio utaratibu wa Mungu. Ukipanda ubaya,utavuna ubaya...isipokuwa kama Mungu ataamua avune huo ubaya kwa ajiri yako.

Vile vile,Haukuwa mpango wa Mungu mwanadamu afe. Kwa upendo wa ajabu wa Mungu alibidi aweke mpango rasmi wakujiua yeye mwenyewe badala ya mwanadamu. (Yote hii ni ili lile neno alilosema litimie). Na hapa ndipo penye maana halisi ya krismas.

"BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
MWA. 3:14‭-‬15 "

Maandiko haya ndiyo yalikuwa chanzo cha agano jipya.

Twende taratibu.
Mungu alijua kabisa ya kwamba katika project yake ya mwanadamu, shetani atakuja ili aiharibu...Kwanini Mungu alijua na bado aliruhusu yatokee? Linaweza likawa ndio swali unalojiuliza sana muda huu...

Mungu ni omnipotent, omniscient , omnipresent...yani Mungu ni mwenye nguvu,anajua kila kitu na yupo kila mahari..hii inamaanisha alijua yatakayotokea.

Kwa kufahamu hilo,MUNGU alifanya njia ya kutoke mapema mno hata kabla ya mwanadamu hajafanya dhambi na shetani hayupo.


...(NITAWEKA UADUI KATI YAKO NA MWANAMKE).

Mungu alimaanisha nini alimpomwambia maneno haya shetani???

Mwanamke anapokuwa mjamzito,damu yake haigusani na damu ya mtoto aliyetumboni....mtoto anakuwa na damu ya baba asilimia 100. Huu ndio uadui ambao Mungu alikiwa anauzungumzia.

Maana yake.
MUNGU ANAMWAMBIA SHETANI,
Mwanamke huyu huyu uliyemtumia, na mimi nitamtumia Mwanamke huyu huyu,nitakuja duniani kupitia huyu mwanamke,nitakuwa na uhalali wa kuwa duniani kwa sababu nitakuwa mwanadamu (emannuel),nitakupiga kisheria,nitakushinda kisheria,nitakupokonya hiyo mamlaka uliyoiba leo kisheria,nitawarudishia hii mamlaka wanadamu kisheria.

HIVI NDIVO MUNGU ALIKUWA ANAMAANISHA.

Mshukuru Mungu kwa wokovu ambao amekupa,ulimgharimu Mungu gharama kubwa sana sana sana.

Hii ndiyo sababu Yesu ilibidi aje duniani kupitia mwanamke,sababu ya Yesu kuvaa mwili.

Yesu amezaliwa na bikira mariamu,lakini damu ya Yesu ni ya Mungu mwenyewe....haihusiani na mbegu ya mwanadamu....

Naomba tuishie hapa kwa leo...katika siku nyingine tutamalizia hii summary ya mwisho

Mungu awabariki sana

(Masomo haya pia yanapatikana YouTube,Bonyeza hapo then subscribe

https://m.youtube.com/channel/UCvUbITHU6Nt6YSyrZHp01xA

Tzworships.blogspot.com
Maestrorabbon
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: