Bwana Yesu asifiwe. Namshukuru Mungu kwa ajili ya kila mmoja aliye humu, kwa vile Mungu  alivyoweza kuwatunza na kuwatetea mkiwa ndani ya Yesu.


 Tunaenda kujifunza somo maalumu sana siku ya leo
 Ninaomba masikio yako na moyo wako. Nimaombi yangu leo Mungu ayafungue masikio ya kila mmoja wenu mahali hapa ,ili tupate kusikia na kuelewa nini Roho wa Mungu anasema. siku ya leo
 Nitazungumza kwa ufupi sana leo juu ya maombi,lakini naamini vitu nitakavyonena leo,vitabadilisha maisha yako yote kwanzia siku ya leo...👏🏻

 MAOMBI
 Maombi ni shughuli pekee ambayo haijawahi kueleweka hapa duniani. Maombi ni shughuli nzito sana sana na wachache sana wamepewa neema ya kuilewa hii dhana ya maombi
 Sio kwako tu. Hata kwa watumishi wengi sana,Neno maombi lilishawahi kuwapa shida sana uko nyuma mpaka kuja kuelewa nini maana ya maombi
 Ili kuelewa maombi, ni lazima kwanza ujue nini maana ya UFALME(KINGDOM) Ninaposema ufalme,namaanisha Ufalme wa Mungu.... GODs KINGDOM

 Kitu cha ajabu ni kwamba,watu wengi wanaoomba,hawajui jinsi ya kuomba
 Halafu sasa,maombi ndio kitu chenye umuhimu zaidi kwenye ufalme wa Mungu
 Sasa kuna msemo alishawahi kuusema JOHN WESLEY KUHUSU MAOMBI
 Alisema na nanukuu
 WITHOUT GOD, MAN CANNOT AND WITHOUT MAN GOD WILL NOT
 Yaani mwanadamu hawezi kufanya lolote bila Mungu hapa duniani,na Mungu hawezi kufanya lolote duniani bila mwanadamu.

 Ni kitu kinachanganya sana sana..lakini namuomba Mungu uweze kuelewa sana hili
 Mungu hawezi kufanya lolote hapa duniani bila mwanadamu wewee na pia Mwanadamu hawezi lolote bila Mungu

 Lolote linalotokea duniani lazima ujue kuwa wewe ni chanzo
 Chochote kile,kiwe kizuri kiwe kibaya lazima ujue kuwa wewe ni chanzo
 Sasa labda nikupe definition ya maombi kidogo.

MAOMBI NI LESENI YA DUNIANI INAYOKUPA RUHUSA YA KUFANYA LOLOTE MBINGUNI
 Prayer is the earthly license for heavenly interference
 Maombi sio option kwa muamini,maombi ni lazima kabisaa
 Maombi sio shughuli ya kidini,ni shughuli ya kisheria... prayer is a legal activity
 Lakini huwezi kuyaelewa haya kama huelewi habari  ya ufalme
 Na hii ndiyo nguvu ambayo amepewa mwanadamu

 Napenda kuiita power of human
 Mwanadamu ndiye kiumbe chenye nguvu zaidi hapa duniani na ni Mungu alifanya iwe ivo
 Kwanini imekuwa hivi? Cha kwanza ambacho unatakiwa kuelewa ni kuwa Mungu amempa utawala wa kisheria mwanadamu hapa duniani
 God only gave legal authority on earth to man..only man
 Swali la msingi linalokuja hapa ni hili..

Mwanadamu ni nani?????
 Naomba tuishie hapa leo,kesho muda kama huu tutaendelea tena

Mungu awabariki
 Amen
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: