SOMO: UFAHAMU UFALME WA MUNGU (MAOMBI NA KUFUNGA) - PART 2

Bwana Yesu asifiwe. 
Tulianza hili somo ili tuweze kuelewa nini maana ya maombi. Lakini kabla ya kufika uko,ilibidi kwanza tujifunze juu ya ufalme. Tukaona kuwa Mungu hawezi fanya lolote duniani bila mwanadamu,Mungu anakuhitaji wewe ili atimize malengo yake hapa duniani. 


Natambua kuwa ni jambo gumu sana kulielewa,ila namuomba Mungu kwa ajili yako ili twende sawa 

Leo tutaendelea kidogo kujifunza juu ya hili na kujua sababu inayofanya Mungu asiweze kufanya jambo lolote duniani bila mwanadamu,na baada ya kujua na kuifahamu hii siri,utaanza kuiona biblia kwa namna nyingine sasa,na ukiisoma utaelewa na maombi yako yatabadilika pia.

Mungu amempa mwanadamu pekee uhalali wa kisheria wa kuitawala dunia,na si kiumbe kingine  (God only give legal authority on earth to human) hapa kidogo imeeleweka. Haki zote za msingi za dunia hii,Mungu alimkabidhi mwanadamu.

Swali linakuja sasa,mwanadamu ni nani??? Nitakachokufundisha leo,utakuwa ni ugunduzi mpya ambao hujawahi ujua labda kwenye maisha yako yote.

Wewe una roho?
Wewe hauna Roho,wewe ni Roho. Mtu hana roho wala hamiliko roho,ila mtu ni roho.  Wewe ni Roho ila unaishi kwenye mwili wa mavumbi (mfu). Mungu aliutengeneza mwili wako kwa mavumbi ya ardhi,kwa hiyo mwili waku asilimia 100 ni mfu (dead body). Na ndio maana hata ukifa,mwili wako tunaurudisha kwenye uchafu,kwenye ardhi.

Kama ni mweupe,mweusi au rangi yeyote bado mwili wako ni uchafu,kwahiyo usijipime utu wako kwa rangi ya ngozi yako.

Ngoja nikueleweshe kidogo. HUMUS ni neno la kiingereza lenye maana ya uchafu (udongo) na MAN inamaanisha ROHO. Neno MAN kibrania linaitwa ISH ikimaanisha Roho. Kwahiyi wewe unaitwa MAN kwa kiingereza ikimaanisha ROHO , Na mwili wako unaitwa HUMUS ikimaanisha uchafu ama udongo na ndio maana kiingereza mwanadamu anaitwa HUMUSMAN ambapo kutokana na urefu wa hili neno,sikuizi tunafupisha na kuita HUMAN. Kwahiyo mwanadamu maana yake ni Roho ndani ya mwili wa udongo ama uchafu ama dead body,mwili uliokufa.
Yote haya ni muhimu sana ili uweze kuelewa maana ya maombi.

Baada ya hapa,baada ya uumbaji wa mwanadamu,Mungu akamwambia mwanadamu AKATAWALE DUNIA (HAVE DOMINIONS ON EARTH).

Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na KUITIISHA; MKATAWALE samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
MWA. 1:27‭-‬28 

Mamlaka haya ya kutawala Mungu akimpa mwanadamu,yaani Mwanadamu ambaye ni Roho ndani ya mwili uliokufa ndiye aliyepewa haya mamlaka na si vinginevyo.

Kwahiyo, kiumbe pekee kilichopewa haki ya msingi na kisheria ya kutawala na kumiliki dunia na Mungu mwenyewe ni mwanadamu na si kiumbe kingine..A HUMAN IS SPIRIT IN A DEAD BODY

Neno La Mungu ni sheria na neno la Mungu halibadiliki. MUNGU AMEJIFUNGA KWENYE NENO LAKE...

SUBSCRIBE: YOUTUBE
Tutataendelea .........

By Maestrorabbon 
Tzworships.blogspot.com
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: