MUNGU YUPO UPANDE WAKO KATIKA KILA ENEO LA MAISHA YAKO (MISIMU KATIKA MAISHA) - LIFE SEASONS
Katika maisha kuna misimu au seasons.

Lolote unalolipitia sasaivi lazima ujue ni kwa msimu tu,kama ilivyo misimu ya hali ya hewa vivyo hivyo maisha ya mwanadamu yapo kwenye msimu/misimu.


Hata Yesu alipojaribiwa na shetani baada ya kumshinda,biblia inasema shetani alimuacha Yesu kwa muda tu/he departed from him for a season. 

Kuna msimu ambao biashara zako zinaenda vizuri,kazi nzuri,familia inashamiri,uchumi unakua....uwe na uhakika huo ni msimu wa mafanikio ila utafika muda wakinyume chake,je ukifika muda huo,utakuwa tayari? Are you ready? Mambo tatakapoanza kuyumba,shetan atapoanza kupepeta maisha yako, uchumi ukiyumba,magonjwa yakishamiri kwamo,kiangazi kikizidi kwenye maisha yako...utafanya nini kama hukujua kuwa kila jambo linawakati wake? 

Ayubu alitambua kuwa umefika msimu wa majaribu ndio maana akashinda.

Hakuna awezaye kuishi nje ya kanuni hii,hata Yesu alipita humu.

Nimaombi Yangu uweze kushinda msimu utakapokuja,Muda huu wa amani,muda huu ambapo hnamafanikio,embu mkumbuke Mungu wako,kusanya nguvu kwenye maombi,noa silaha zko kwa mifungo,nunua silaha mpya kwa mikesha, tengeneza misingu imara kwa kusoma na kutafakari neno la Mungu...atakapokuja mjaribu,akakute umejengwa kwenye boma,nyumba yako ni ya chuma na msingi wako upo juu ya mwamba yaani Yesu kristo .


Maana, tazama, nimekufanya leo kuwa mji wenye boma, na nguzo ya chuma, na kuta za shaba, juu ya nchi yote; juu ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wa nchi hii. Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.
YER. 1:18‭-‬19 

By maestrorabbon 
Tzworships.blogspot.com
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

1 comments: