Bwana Yesu asifiwe sana. Leo tunaendelea kidogo na somo letu la ufalme wa mbinguni na namna ya kuomba. 


Kama tunaenda sambamba basi naamini utakuwa unakumbuka ni wapo tuliishia. Ninamuomba Mungu akupe masikio ya kusikia,na Roho mtakatifu ayathibitishe haya mafundisho kwenye moyo wako Amen.

...Mungu alitoa utawala wa kisheria wa kumiliki dunia kwa kiumbe chenye mwili wa udongo,Kiumbe chenye mwili ndicho kiumbe halali duniani. Kwa  lugha nyingine tungeweza kusema hivi..UTAWALA WA KISHERIA WA KUTAWALA NA KUMILIKI DUNIA, ILIPEWA ROHO AMBAYO IPO NDANI YA MWILI WA UDONGO AU DEAD BODY(MWILI MFU)...Mwanadamu.

Najua ni mafunisho magumu ila tutaelewana. 

Hapa ndipo penye siri kubwa sasa ,tusikilizane ..
KIUMBE CHOCHOTE AMBACHO HAKINA MWILI HAKINA HAKI YA KISHERIA YA KUWEPO DUNIANI(ILLEGAL ON EARTH)...any being without a body,is illegal in earth.

Kama huelewi hii kanuni, inawezekana ndiomaana biblia huielewi muda mwingine,Kama huelewi hii kanuni basi itakuwa ngumu sana kuelewa juu ya kuzaliwa kwa Yesu (Incarnation of jesus).

Incarnation maana yake ni Roho ndani ya mwili (tutaangalia baadae).

Kwahiyo,Roho yeyote ambayo haina mwili haina haki ya kisheria kuwepo duniani(illegal on earth).

Sasa utakuwa unajua kwanini mapepo,mizimu nk hawahitajiki duniani au hawana haki ya kisheria ya kuwepo hapa. Any spirit without a dead body is illegal on earth.

Kwahiyo, kitu ambacho cha muhimu sana kwako hapa duniani au silaha ya muhimu sana Mungu aliyokupa hapa dunian sio roho yako bali ni mwili wako.(the most powerful weapon you posses is not your spirit, is your body).
Na hii ndiomaana hata wewe ukipoteza mwili wako,unakuwa illegal unapoteza haki ya kuwepo hapa na inabidi uondoke duniani,tunaita kifo...Naomba ukumbuke kuwa Roho haifi,hivyo wewe haufi ni mwili unaokufa.

Kwahiyo silaha ya muhimu uliyonayo hapa duniani ni mwili wako,kwasababu mwili unakupa hali ya kisheria ya kuwepo duniani na kutawala na kumiliki kila kitu.

Na hii ndiomaana hata mapepo yanajaribu kuingia kwenye mwili wako. Yanatafuta uhalali wa kisheria wakuwepo duniani ili waweze kufanya mambo yao. Roho yoyote isiyokuwa na mwili,haiwezi kufanya lolote duniani,ili mapepo waweze kuleta uharibifu,wanahitaji mwili. Kwa sababu wewe unamwili basi una mamlaka ya kisheria ya kuwasambalatisha na kuwafukuza mapepo (Luka 10:19).

*Pointi ya msingi*
Mungu aliamua kujinyima haki ya kisheria ya kumiliki na kutawala dunia .

Najua kabisa,katika jambo gumu nililoliongea basi ni hili hapa,na inawezekana ukapata ugumu wa kuamini hiki kitu,lakini Mungu mwenyewe ndiye alieamua iwe ivyo. 
Kwanini? MUNGU HANA MWILI

Ngoja nikueleweshe taratibu uelewe....
....MUNGU AKASEMA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU NA KWA SURA YETU,AKATAWALE.... soma kwa makini hapo...MTU AKATAWALE DUNIA,Mungu hakusema TUKATAWALE ila WAKATAWALE yeye akajitoa hapo. Kwa kiingereza imeandikwa hivi..LET THEM HAVE DOMINIONS sio LET US HAVE DOMINIONS. 

Mungu hakosei na wala hasemi kitu kwa bahati mbaya au kwa kubahatisha. Kwa kusema vile Mungu alikuwa anaweka sheria duniani kuwa Mtu mwenye mwili ndiye mwenye mamlaka ya kutawala dunia (Roho ndani ya mwili wa mavumbi).

Mungu hakuwa na mwili,alikuwa mwili wewe... baada ya hapo akatengeneza sheria (LET THE) au (WAKATAWALE),wakina nani? ROHO ndani ya mwili yaani mwanadamu au HUMUSMAN kama unakumbuka vizuri.

Mungu anapoongea kila neno huwa sheria,na MUNGU hawezi kuvunja sheria zake mwenyewe,kama angevunja hii sheria basi tusingemwani tena na angeacha kuitwa Mungu.

Kwahiyo Mungu anamuhitaji mwanadamu,ili aweze kuingilia maswala ya duniani hii yote ni kwasababu hawezu kuvunja sheria zake mwenyewe.hakuna jambo linaweza kutokea duniani bila ushirikiano wa mwanadamu. Huu ndio ukuu ambao mwanadamu unao.

Mungu mwenyewe hawezi kuingilia jambo lolote duniani bila ruhusa na leseni yako ya ushirikiano. Najia ni kitu kigumu sana kuamini,lakini kama huamini hii, labda ndiomaana maombi yako hayajibiwi,umekuwa ukiomba sana lakin bado mgonjwa,bado huna hela,bado maisha magumu nk....HII NI KWASABABU UNAMSUBIRIA MUNGU AFANYE KITU

Naomba tuishie hapa kwa leo,ila nakupa hizi kanuni saba za maombi uzishike.

1. Utawala wa haki wa kisheria wa dunia alipewa mtu mwenye mwili.

2. Mungu hajuhusisha Kwenye utawala wa dunia(hii sio kwa sababu Mungu hana nguvu, hana uwezo...hapana,ila ni kwa sababu  Mungu hawezi kupinga maneno yake)
..
...
....

Katika kipindi kijacho nitakupa kanuni zingine 4

1. Pia nitakwambia kwanini Mungu alifanya hivi.
2. utajua kwanini Mungu hakuweza kuzuia anguko la mwanadamu eden
3. Na kwanini Yesu alikuja duniani.

Ubarikiwe sana wewe ambaye tunaenda sawa.
Kama ulipitwa na masomo mengine mawili,basi tembelea website hapo chini,utayapata

Itaendelea.........

SUBSCRIBE : OUR YOUTUBE CHANNEL

Tzworships.blogspot.com 
Ahsante
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: