~Utawasikia watu wakisema alizaa naye ila hawakufunga ndoa!.


~NDOA nini? Ndoa ni kitendo cha kukutana kimwili km mume na mke. Kwa hiyo kila unaposhiriki tendo la ndoa na mtu yeyote, unakuwa umeoa/umeolewa naye au umefunga ndoa naye!.

~Ndio maana Yesu alipomwambia yule mwanamke Msamalia akamwite mume wake, alipojibu sina mume, Bwana Yesu alimwambia umeolewa na wanaume watano!. #YOHANA 4:18, 

~Ktk macho ya nyama hakuolewa  lakn alikuwa anatembea na waume 5! Mbingu ziliona amefunga ndoa nao.

~Unapofanya mapenzi na watu mbalimbali unafunga nao ndoa, sababu ndoa ni jambo la kiroho ambalo mume na mke hufanyika mwili mmoja Kupitia tendo la ndoa!.
#1WAKORINTHO 6:16
"Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja".

~Harusi ni sherehe ya ndoa na siyo ndoa, ni utaratibu uliwekwa namna ya kuoana, kutokana na kuongezeka maasi ya kuachana, ili kwa macho ya kimwili viwepo vidhibitisho kwamba mlioana, lakini ktk ulimwengu wa roho tendo la ndoa ndilo huthibitisha kwamba mmeoana!.

 ~Rebecca alipokuwa anaolewa na Isaka, Leo ikatolewa Mali kesho akaenda kwa mumewe, hazikuwepo mbwembwe.
#MWANZO 24:58
"Wakamwita Rebeka wakamuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema nitakwenda"
#BARIKIWAKWAKUELEWAMAANAYANDOA
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: