Askofu mkuu wa kanisa la Full gospel bible fellowship Askofu zacharia kakobe,hivi karibuni alikubwa na kizaa zaa baada ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kudai kuwa askofu kakobe halipi kodi hivyo kuanza uchunguzi juu yake.

Leo tarehe 20-Feb uchunguzi umekamilika na mambo haya matano yamegundulika kwenye uchunguzi huo

MAMBO MATANO

1.Imesema Askofu huyo hana akaunti wala fedha katika taasisi ya fedha hapa nchini. Aidha uchunguzi ulibaini kuwa Askofu Kakobe ni mmoja wa wasimamizi wakuu wa akaunti za kanisa zilizopo katika benki ya NBC zenye jumla ya kiasi cha Sh8.2bilioni, kiasi hiki cha fedha kimetokana na sadaka, zaka na changizo ambazo zinatolewa na waumini wa kanisa tajwa hapo juu, hivyo kwa mujibu wa sheria hakitozwi kodi.

2 Kanisa lilikwepa kulipa kodi kiasi cha Sh20.8milioni.

3.Kampuni inayomilikiwa na watoto wa Askofu Kakobe ilikwepa kulipa kodi ya Sh37.2 ambazo zimelipwa baada ya uchunguzi. Kwa ujumla kiasi kilicholipwa kutokana na uchunguzi ni Sh58.1milioni.

4.Kanisa linatunza kiasi kikubwa cha fedha kwenda ndoo na ‘majaba’ kinyume na taratibu za utunzaji fedha.

5.Kanisa halitengenezi hesabu za mapato na matumizi ya fedha kitu ambacho ni kinyume na katiba ya kanisa na sheria ya usimamizi wa fedha ambayo imepelekea matumizi mabaya ya fedha za waumini kama vile safari za nje ya nchi ambazo zimedhaminiwa na kanisa lakini wanaosafiri ni Askofu na familia yake.

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: