๐Ÿ’ฅBIBLE STUDY๐Ÿ’ฅ
Program: Christian theology & systemic theology.

(Kijana Mkristo-KM)

Sehemu ya 2.
-----------------------------------

Asili ya kanisa (ukristo).
---------------###---------------

Ukristo Asili yake hasa inaanzia "palestina" au palestine. Katika hii palestina kuna sehemu inaitwa JUDEA na ukifika hapa JUDEA kuna mji mkubwa uliochangamka unaitwa Yerusalemu. Hapo Yerusalemu sasa,ambayo ipo ndani ya palestina,ndipo ukristo ulipoanzia mnano karne ya 1 au First century (1 AD).

Fathers of The church

Sasa hapa palestina ndipo penye shida. Naamini wewe msomaji kuna maswali umeanza kujiuliza, inawezekanaje ikawa ni Yerusalemu halafu tena ndani ya palestina? Mimi nilidhani ni israeli?... Ni baadhi ya maswali unayojiuliza natambua. Sasa ukweli upo hapa chini.

๐Ÿ•ธ️ Waandishi (scholars) wanaamini ya kwamba jina la palestina limetokana na neno "Philistia" neno ambalo linamaanisha "wafilisti". Kutokana na ushahidi wa biblia, wafilisti wanaonekana kukaa eneo hili la Philistia mnano karne ya 12 BC au kabla ya . Mengi tutajifunza zaidi kuhusu uhusiano wa Palestinina.

๐Ÿ•ธ️Sasa kama tulivyoona ya kwamba ukristo umeanzia yerusalemu ndani ya palestina, ila kimsingi kabisa ukristo chimbuko lake ni dini ya JUDAISM huko judea.

Judaism ni nini?
------###------

Ukristo halisi chimbuko lake ni Kwenye dini hii ya Judaism ambayo yenyewe ilianzia pale kwenye hekalu la pili la Suleiman. Yani katikati ya ujenzi wa hekalu la pili na  kuanguka wa hekalu hilo,hapo ndipo judaism ilipoanzia BCE 515.

Dini hizi mbili zilitengana na kuwa tofauti ndani ya karne ya 1 kwa sababu zifuatazo.

๐Ÿ‘‰๐Ÿผukristo huu tunaujua leo imani yake ipo kwenye AGANO JIPYA ambalo mwanzilishi wake ni YESU KRISTO. Hivo ukristo huu unaitwa ORTHODOXY yaani kutoka ndani ya agano jipya. 

๐Ÿ•ธ️Hii judaism yenyewe ni kinyume cha ORTHODOX. Yenye imejikita Kwenye orthopaxy yaani tabia njema. Asili yake hasa ni kwenye AGANO LA MUSA AU ZILE AMRI 10 au unaweza kuita MOSAIC COVENANT. Wao wanaamini sana kwenye TORAH na TALMUD (Tutayazungumzia baadae).

๐Ÿ•ธ️wakristo tunaamini kwenye wokovu binafsi kutoka kwenye dhambi kupitia kumpokea Yesu kristo kama Bwana na mwokozi wako. 

Judaism au dini ya wayahudi wao wanaamini kwenye mawasiliano ya moja kwa moja na Mungu kupotia rituals(ibada za kitamaduni nk).

๐Ÿ•ธ️Wakristo sisi tunaamini kwenye utatu mtakatifu. Yani Mungu mmoja kwenye nafai tatu (baba mwana ma Roho mtakatif). Pia tunaamini alama vile YOHANA 1 inavyosema kuwa Mungu aliuvaa mwili akawa kama sisi kupitia Yesu. Na ndio maana Yesu anaitwa Yesu kristo. Yesu ikiwa ni sehemu yake ya ubinadamu na kristo ni sehemu yake ya uungu (tutazungumza kwa undani).

๐Ÿ•ธ️Hawa wayahudi wao hawaamini juu ya concepts zote izi. Wao wanaamini kuwa Mungu ni mmoja na hamna utatu pia hawaamini kuwa kuna siku Mungu aliuvaa mwili akawa mwanadamu.

Mambo haya ndio yanayotifautisha kati ya JUDAISM (UYAHUDI) NA UKRISTO (CHRISTIANITY)



THE PATRISTIC PERIOD
(FATHERS OF THE CHURCH)
--------###--------

Patristic period au kipindi cha waanzilishi wa kanisa (ukristo), ni kipindi cha muhimu sana kwenye historia na uendelevu wa dini hii ya kikristo. 

๐Ÿ•ธ️Ma fathers hawa ndio wenye mchango mkubwa sana sana kwenye kujenga msingi imara wa kanisa ambalo tunaliona leo hii. Kila mkondo wa kikristo ikiwemo Lutheran,Eastern orthodox,anglican na hata Romam catholic, wanatambua kuwa Kipindi hiki  cha patristic ndicho kipindi pekee ambacho kimelitambulisha kanisa na ndio nguzi ya maandiko ya kikristo yote (Christian doctrines).

๐Ÿ•ธ️Makanisa haya yote yanaendelea kukua kwenye misingi ambayo tayari umewekwa na nawa waandishi wa kwanza au waandisho wa kale.

๐Ÿ•ธ️Utangulizi
-------###------

Neno patristic limetokana na neno la kilatin PATER LIKIMAANISHA "FATHER ". Jina hili la patristic bado lina debate nyingi sana na hii imepeleka literature au waalimu wengine wa theolojia na baadhi ya vitabu kutumia majina mengine kutambulisha kipindi hiki cha waandishi hawa wa kale wanaojulikana kama Fathers of the church.

1.kipindi hiki cha Fathers kilianza mwishoni kabisa mwa "New testament writtings" - mwisho wa uandisho wa maandiko ya agano la kale mnano karne ya 100 mpaka mwanzo mwa uanzishwaji wa baraza la CHALCEDON (Tutalizungumzia mbeleni).

2. Patrology:- hili ni somo ndani ya theology ambalo linahusika na kipindi hiki cha mafathers hawa tu. Unaweza ukajua umuhimu wao sasa kwenye dini ya kikristo. Patrology ni somo la ma Fathers kama vile Theology ilivyo somo la Mungu.

AGENDA KUBWA ZA KIPINDI HIKI.
-------###--------

๐Ÿ•ธ️Kazi kubwa ya Fathers au waandishi hawa wenye heshima kubwa kwenye dini hii ya kikristo ilikuwa ni kutengeneza na kuweka mambo sawa. Mambo haya ni mambo ambayo yalikuwa yanaleta mkanganyo mkubwa baina ya watu kwenye ukristo.

๐Ÿ•ธ️Mfano wa jambo ambalo wakongwe hawa ilibidi waliweke sawa ni uhusiano kati ya UKRISTO NA UYAHUDI (JUDAISM).

Kwa hiyo kwenye karne ya kwanza hawa mafathers walikuwa na kazi yeah kusolve mambo kama haya. Pia kuna mambo mengine ya msingi ambayo paulo ameyaongelea kwenye barua zake, mambo ni

1. Je, mkristo ambaye sio myahudi (gentile) ni lazima kufanyiwa tohara?

2.je, wakristo ni lazima wafuate sheria za chakula za kiyahudi?

3. Ipi ni nja sahihi ya kutafsiri agano la kale?

๐Ÿ•ธ️Mambo haya yote na mengine mengi yenye ukakasi na ugumu ndio ililiwa kazo ya hawa mafathers au waandishi wa hizi doctrine kuyatatua.

Hapa ndipo panapoanza uzuri wa theolojia. Tutakapoanza kumchambua Father mmoja mmoja na kujua mchango wake kwenye ukristo ndipo utajua kwa nn tunasoma theolojia.

๐Ÿ•ธ️Pia hawa mafathers ndio baadae wakaleta ile idea ya APOLOGETIC.  APOLOGETICS hawa ni watu ambao kazi yao ni kuitetea imani na dini ya kikristo kutokana na wale wote wanaoipiga vita.

๐Ÿ•ธ️Kimsingi kipindi hiki kizima cha karne ya kwanza kanisa lilikuwa kwenye presha kubwa sana dhidi ya nchi (Roman empire), kwahiyo agenda nyingi za kipindi hiki zilikuwa ni za survival (jinsi ya kufanya kanisa liendele kuwepo) na hapa ndipo hawa apologetics walikuwa na kazi ya ziada.

๐Ÿ•ธ️Hali iliendelea kuwa mbaya kwa kanisa mpaka ilipofika miaka ya (306-37) ambapo CONSTANTINE alikuwa rasmi Kiongozi wa Empire ya Roma. Constantine alifanikiwa kuipatanisha Roman empira na kanisa hivyo kwenye hii karne ya 4 ukristo ukawa dini kamili. 

๐Ÿ•ธ️Rasmi mwaka 321, cinstantine akatoa tamko kuwa siku ya JUMAPILI iwe public holiday. Huu ndio mfululizo wa uanzishwaji wa dini hii.

๐Ÿ•ธ️KIPINDI kijacho tutaenda kusoma wazee watuatao (church Fathers) na utaona jinsi gani wamepigana kuhakikisha wanajenga misingi imara ya dini ya kikristo.

1. Justin matryr (C.100-165)
2.Iraneus of Lyon (c. 130-200)
3. Origen(c 185-254)
4. Cyprian of carhage (alikufa 258).

๐Ÿ•ธ️Pia tutaangalia kitu cha msingi sana kinaitwa
THE CAPPADOCIAN FATHERS hapa tutajifunza zaidi juu ya utatu mtakatifu.

Mungu akubariki sana wewe mfuatiliaji.

By
Maestro (rabbon)

YouTube: kijana mkristo
Instagram: kijana_mkristo
Web : Tzworships.blogspot.com
(0685225275,0623725275)
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: