Na Pastor Myamba

 2 Wafalme 19:19 Basi sasa, Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA Mungu, wewe peke yako.

 Haya yalikuwa ni maombi ya Hezekia dhidi ya mfalme wa Ashuru aliyetuma ujumbe wa kumtukana Mungu wa Israel, na BWANA akajibu maombi Hezekia. Sikia hili neno juu yako mchana wa Leo Yamkini wapo waliomtukana MUNGU wetu kwasababu ya unayoyapitia, hata kwa kuuliza tu kuwa yupo wapi Mungu wake anaemwamini mpaka apitie yote hayo anayopitia.

 BWANA anaenda kujitukuza kupitia shida unayoipitia, chukua neno hili la kinabii mchana huu wa leo, BWANA anaenda kutia maji mahali pakavu ndani yako ili wale waliokuwa wanajiuliza kimya kimya kuwa yuko wapi MUNGU wako wapate kujua kuwa yupo MUNGU anaejibu kwa MOTO. Neno hili linaenda kutimia ndani yako leo, nasema linaenda kutimia, kuna hali ya hewa inaenda kubadilika ndani ya maisha yako na utamshangilia BWANA kwa namna ya ajabu, utarukaruka na kucheza kama ndama wa mazizini.

 Aliyetayari kupokea neno la unabii huu na aseme Ameen!!

 ——-——————————
 Pastor Myamba
+255 713 842 123
+255 744 982 517
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: