Swali:
Nitajuaje huu ndio wakati sahihi wa kuoa au kuolewa?


Kwanza lazima tufahamu swala la kuoa na kuolewa ni jambo ambalo limetunzwa na Mungu kwenye nyakati/muda

Sasa utajuaje kuwa ni nyakati zako?
Fahamu kuwa Muda hua unaongea ndani ya nafsi ya mtu hasa pale ambapo anatambua lugha anayo tumia kuwasiliana na nafsi yake.
Mfano :
-Mtazamo wa kifikra.
-mawazo.
-mwenendo.

1.unapo ona kwamba umeingia kwenye Hatua ya kufikiri kwa level ya Mume(sio mwanaume) na kufikiri kwa level ya mke(sio mwanamke).
2.mawazo ya kufanya mambo kwa level ya familia ingawa Ukweli Upo single nacho ni kiashiria cha muda wa kufanya Maamuzi ya kuoa au kuolewa.
3.mwenendo-pale unapo amua kubadilika na kuuishi mwenendo ambao unaleta afya kwa familia yako. Mf :unaiishi tabia ya baba bora au mama bora ingawa bado hiyo nayo nimoja ya alama ya kuzingatia ili ufanye maamuzi.

Barikiwa.
Wako katika Bwana.
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: