SEHEMU YA 1
1 samwel 15:22(b)
"Angalia utii ni bora kuliko dhabihu."
wafilipi 2:3,8
2."msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake."
8."Tena alipo onekana ana umbo Kama Mwanadamu alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti ya msalaba".
Mathayo 24:13"lakini kuvumilia hata mwisho, ndiye atakaye Okoka "
Utangulizi:
Katika Hatua za muendelezo wa ukuaji au uhimarishwaji viwango mbalimbali vya maisha ya kiroho na kimwili, utimilifu wake umefichwa kwenye mambo matatu ambayo ni
UNYENYEKEVU.
UTII.
USTAHIMILIVU.
Utii- ni hali kukubali kutekeleza jambo au agizo fulani unalotakiwa kufanya haijalishi litaleta matokeo hasi au chanya.
Katika maisha ya ukuaji uhimarishwaji wa fikra zetu utii ni nyenzo muhimu sana, ambayo mtu akiishi itamsaidia kuimarika fikra na nafasi yake aliyonayo mbele za Mungu.
1samweli 15 :22(b) tunaona umuhimu wa utii , inadhihirisha kuwa ndani ya utii kuna kitu cha thamani ,utii ubeba na kuficha mafanikio yako ya sasa na baadae kwasababu ndani utasaidiwa kupambanua mambo au vitu kulingana na mahali unako elekea. Ndani ya utii kuna kutukuzwa /kuinuliwa na Mungu kwenye maeneo yote aliyo ketishwa mtu.
Tulio wengi tunashindwa kuwa watii, na hapo ndipo tunapoteza nafasi zetu katika ulimwengu wa Roho na ulimwengu wa mwili pia. Fahamu Mungu anahitaji mtu Mwenye roho ya utii ,kwasababu katika kuyatimiza mapenzi ya Mungu kunahitajika utii ndani ya muhusika. wafilipi 2:8 Roho Mtakatifu anakukumbusha kwamba Utii wa Yesu Kristo umetuletea wokovu kwa njia ya msalaba, sijui wewe utii ulio nao umeleta matokeo gani mbele za Mungu kwa kuzingatia nafasi uliyo nayo.
unyenyekevu -hali ya kujishusha pasipo kuangalia haki, hadhi, au kiwango ulicho nacho kwenye eneo ulipo. Unyenyekevu huambatana na utayari wa kujifunza mambo mbalimbali, ukiwa mnyenyekevu mbele za Mungu kuna vitu vina achiliwa ndani yako kwa lengo la kukuzidisha katika viwango vya kufikiri na kuimarisha misingi yako na Mungu.
wafilipi2:3
Tunaona mtuma Paulo anasema nasi kuwa aliye na unyenyekevu hawez kujihesabia haki au kuona yeye bora kuliko mwingine.
Sikia hakikisha una uiishi unyenyekevu katika maisha yako yote, Fanya unyenyekevu kuwa chakula chako cha kila siku, itakusaidia kufika mahali fulani.
Ustahimilivu - ni hali ya kuvumilia mambo au jambo kwa kipindi fulani kwa kuzingatia matokeo tarajiwa. Mtu Mwenye ustahimilivu anauwezo wa kutekeleza malengo au kusudi la Mungu lililo ndani yake kwa kiwango cha juu. Mathayo 24:13.
Inasikitisha Sana majira tuliyo nayo watu Wengi ndani ya mioyo yao wamepungukiwa na mambo haya matatu.
Tafuta uso wa Bwana mwambie akuumbie roho ya utii, unyenyekevu na Ustahimilivu maana ndani yake kuna matokeo ya Ukomavu wa kifikra.
Mambo haya matatu ni afya mifupani kwa yeyote anayetambua na kuelewa wapi anako elekea au anapo taka kufika na Bwana,ingawa hugeuka kuwa ugonjwa kwa mtu yeyote ambaye hajui /hatambui wapi anako elekea.
Mungu akubariki Sana kwa utayari wa kujifunza.
Post A Comment:
0 comments: