Bwana Yesu apewe sifa!!!!.......
kwanza kabisa kabla ya kujua kusudi la kubatizwa tupitie maneno haya;

*Warumi  6:4 Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima*

Ubatizo maana yake kuuzika utu wa kale yaani utu wa Adamu na kuwa kiumbe kipya yaani kuvaa mwili wa Kristo
*(maana nyingine ni kuzaliwa mara ya pili)*

✨ *lengo kuu la kubatizwa:*
dhima kuu ya kubatizwa ni kuwa na dhamiri safi mbele za MUNGU.
1 Petro 3:21.
 Unapo amini kuwa Yesu Kristo ni Bwana na mwokozi unasamehewa dhambi, lakin tendo la kubatizwa ni kuuzika ule mwili ambao ulikuwa kwenye vifungo vya dhambi na kufufuka pamoja na mwili mpya wa Kristo. Ndio maana unatakiwa upate ubatizo wa maji mengi na uzamishwe ndani ya maji ili kukamilisha yote hapo unakuwa umeokoka.
Marko 16:16
Wakolosai 2:12

*kwanini tunatakiwa tubatizwe*
_jibu:_
Tunatakiwa kubatizwa ili kupata ondoleo la dhambi
Marko 1:4
 Ni tendo la kuonyesha kuamini uweza wa Mungu alipo mfufua Kristo kutoka katika wafu
Wakolosai 2:12
kuwa na ushirika ndani ya watakatifu
Waefeso 4:5

*Yesu alibatizwa kwa ubatizo wa maji mengi mto Yordani kwa sababu alikuwa ameuvaa mwili wa Adamu nasi tuenende kwa kuzifuata nyayo zake*

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: