Katika sehemu iliyopita  tuliona jinsi ambavyo Mungu alimpa utawala wa kisheria mwanadamu wa kutawala na kumiliki dunia kwa sababu  mwanadamu anaitwa HUMUSMAN/Human yaani roho ndani ya
mwili wa mavumbi.


Pia tukaona kwa ufupi ya kwamba huu utawala wa kisheria ambao Mungu alimpa mwanadamu yeye  mwenyewe Mungu hakujihusisha na utawala huo.Kwa nn?? Ntajibu leo hilo swali

Katika kipindi kilichopita tulijifunza kanuni kuu 2 za maombi. leo tutajifunza nyingine 3.

3. Roho pekee iliyopo ndani ya mwili  wa mavumbi (HUMUSMAN) ndiyo yenye  mamlaka  ya kisheria ya kutawala(Legal on earth).

4. Roho  yoyote ambayo haina mwili (A spirit without a dead body is illegal on earth, thats includes God  himself), hii kanuni inamtoa Mungu  mwenyewe kwenye uhalali wa kisheria wa kutawala/authority ya Dunia. Mwanzo 1:26-30.
(Ninaposema utawala/mamlaka simaanishi nguvu,utawala/mamlaka na nguvu ni vitu viwili tofauti,unaweza ukawa na nguvu lakini usiwe na mamlaka..authority and power..Mungu ni mwenye nguvu,lakini aliamua kujivua mamlaka).

Najua ni somo gumu sana au kanuni ngumu sana kuelewa.  Kufanya hivi haimaanishi Mungu hana nguvu, Bali Mungu hawezi kuvunja neno lake mwenyewe kwa hiyo  aliposema WAKATAWALE alimaanisha Roho yenye mwili na Mungu hana mwili. 

5. Hakuna jambo lolote la kiroho linaloweza kufanyika Duniani bila ushirikiano wa mwanadamu. Lolote linalotokea duniani  liwe zuri au baya uwe na uhakika mwanadamu unahusika kwa sababu wewe  ndo mwenye legal rights/haki ya kisheria.

Hapa tunapata swali 1 la msingi ambalo labda hukuwahi  kujiuliza.

Swali: kwanini Mungu hakumzuia Eva pale bustani ya eden wakati anataka kula kile tunda? Mungu alikuwa haoni au haelewi kitakachotokea? Unataka kuniambia Mungu ambaye anajua kila kitu,aliyeumba Mbingu na nchi, omnipotent, omnipotent, omniscient God hakuweza kumzuia eva asile lile tunda ili kuzuia anguko la mwanadamu? 

Naamini saizi utakuwa umepata jibu.

MUNGU HAKUWA NA MWILI (DEAD BODY) na ndio maana hakuweza kuingilia maswala ya mwanadamu. Mungu angeingilia pale,basi angekuwa ameenda kinyume na neno lake,na tusingemwamini tena.

Embu kwa sasa tumzungumzie shetani kidogo ili tupate kuelewa zaidi. 

Shetani anamuendea Eva pale bustani akitaka kufanya nae bishara. Lakini huku akijua kuwa yeye ni roho na sasa tunafahamu kuwa Roho kama roho haina uhalali wa umiliki au kufanya lolote duniani kama haipo ndani ya mwili wa mavumbi (dead body).

Kwa kutambua hilo shetani akamuingia nyoka (serpent). Nyoka ama serpent asilimia 100 ni mavumbi ya nchi,kwa kufanya hivyo shetani akawa amepata muda kidogo wa kufanya biashara duniani na Eva. 

Kumbe hata shetani alihitaji mwili wa mavumbi ili awe na uhalali wa kisheria hapa duniani (legal authority).

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa anguko la mwanadamu pale edeni.

Lakini bado kuna maswali mengi utakuwa unajiuliza kuwa Mungu alikuwa wapi? Kweli Mungu muweza wa yote alishindwa kufanya jambo kuzuia anguko hili??

Mambo haya yote yaliyotokea pale eden hayamaainishi Mungu hana nguvu au mamlaka ya kuamua jambo. Mungu ni muweza ya yote, hashindwi jambo lolote, akiamua hufanya na analotaka hutimia. Ila hapa. Je, kwanini Mungu hakuingilia hapa na kuzuia anguko.?

Naomba nikufundishe kitu leo.. KIMYA CHA MUNGU KINA MAJIBU MENGI. Unapoona Mungu kama hajibu au kama kanyamaza ujue kuna jambo analipika na bado mda mchache litapakuliwa.

Mungu alikaa kimya kwenye hili kwa sababu kuu mbili.
1. Mungu hakuwa na mwili,hakuwa na uhalali wa kisheria wa kuingilia mambo ya mwanadamu, na kama angeingilia hili jambo basi angekuwa amevunja neno lake mwenyewe na sisi tusingeweza kumwamini,lakini ashukuliwe Mungu kwa sababu ni mtunza maagano (Daniel 9:14).

Kwa lugha nyingine unaweza kusema kuwa anguko la mwanadamu ni kwasababu ya uaminifu wake kwenye neno lake.

2. Mungu tayari alikuwa anajua kitakachotokea pale eden baada ya kumuumba mwanadamu,hivyo akaanda kabisa na plan ya wovoku kwa huyo mwanadamu 

"Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. "

BWANA Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
MWA. 3:8‭, ‬14‭-‬15

Hapa ndipo plan ya wokovu ilipoanzia.

Shetani alifanya vyote ila alisahau kuwa Mungu kweli hawezi kuingilia yale maamuzi ya mwanadamu,ila still Mungu anauwezo wa kuongea akiwa duniani...

MUNGU AKAMGEUKIA NYOKA NA KUMWAMBIA, NA SIO EVA.....AKAMLAANI NYOKA KWA SABABU ALIRUHUSU MWILI WAKE UTUMIKE NA SHETANI,Au aliimpa uhalali wa kisheria shetani kuleta uharibifu duniani.

Baada ya hapo ndipo wokovu ukaingia duniani.

MUNGU AKAMWAMBIA SHETANI KUWA, MWANAMKE HUYU HUYU ULIEMTUMIA KULETA ANGUKO,KULETA DHAMBI,KUINGIZA MABAYA..NA MIMI NITAMTUMIA MWANAMKE HUYU HUYU KULETA WOKOVO....KWA KUTUMIA MWANAMKE HUYU,NITAPATA MWILI,NITAKUJA DUNIANI NA NITAKUWA NA UHALALI WA KISHERIA WAKUFANYA JAMBO LOLOTE DUNIANI NA NITAKUPONDA KICHWA SHETANI.....HALELUYAAAA👏🏻

Hii ndiyo inaitwa INCARNATION OF JESUS CHRIST.

Wakati ujao nitakueleza kwa undani sana juu ya INCARNATION ama kuja kwa roho ya Yesu duniani na tukimaliza hapo utakuwa umeelewa sasa kwanini tunaomba.



Itaendeleaaaa.......

By maestrorabbon 
Tzworships.blogspot.com 
Youtube : OUR CHANNEL
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: