Swali.

*Kama mbinguni miili yetu hatutoingia nayo, Je wale wanaoenda motoni milele wenywewe wataingia na miili hii ya kibinadam huko jehanam ya moto?
Kama ni ndiyo ,toa sababu?* 

life after death

Mwanadamu aliyekamilika ni muunganiko wa vitu vitatu ambavyo ni; Mwili- asili yake ni udongo unakufa na kupotea.
Nafsi- hii ni utu wa mtu yani hapa ndio kuna utambuzi wa mtu,kama elimu,cheo,ufahamu na vitu vyote visivyo shikika vinavyo weza kumuelezea mtu.
Roho - Hii sio roho ya Mungu kwa maana ya roho mtakatifu hii ni pumzi ya uhai.
Mwanzo 2:7 "Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai." 

Mwili huu ni maalumu kwa ajili ya kuishi duniani tu,mtu alipofanywa kwa mavumbi alikua ni sanamu tu kama roboti.Alipopuliziwa pumzi ya uhai (roho) ndio akawa nafsi.

Unatambua hapo udongo ni wa dunia na nafsi imeungana hapo kilichotoka kwa Mungu ni roho.

Ukitaja Mungu, shetani ,peponi au kuzimu tayari ni vitu vya rohoni ,mwili wa duniani hauwezi kwenda mbinguni au kuzimu ,kule zinaishi roho ambazo Mungu anauwezo wa kuzivisha miili mipya kama atakavyo yeye..

1Korintho 15 :35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?

36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;

37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;
38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.

Unaona Mungu atatoa miili ambayo kwa hiyo ndio itakua ya milele maana baada ya uasi Adam aliwekewa malaika amlinde hasije kula tunda tena akapata mwili wa kuishi milele..
MWANZO 3:22
"Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele;" 

Kwa hiyo miili ya either mbinguni au motoni itakua mipya nayo tutavalishwa pamoja siku ile ya kiyama itakapofika na sio sasa.
Kwa sasa roho zilizo Fanya dhambi ziko kifungoni kuzimu ndio zile Yesu alipokufa alikwenda kuwahubiria na kunyanganya funguo za kuzimu ibilisi.
1Korintho 15:51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,

52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.

Kwa hiyo mwili mpya waliokufa watafufuliwa na kuvalishwa walio hai watabadilishwa ili wa kwenda moto wa milele waende na wakwenda kwa Mungu milele wapokelewe mawinguni.

Pia unaweza kujisomea 1wakorintho 15:yote.

@mwl nyahendebright
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: