**JE" KUNA WATU WALIOANDIKIWA JEHANAMU MILELE?* YAANI WAMESHAWEKEWA HUKUMU ISIYO FAA KUWAGEUZA?

Kutokana na hoja hapo JUU,


Ni kweli Mara kadhaa,kunawahubiri wanasema, wengine hata uwahubirieje hawata Okoka maana wameandikiwa Hukumu!🤥

Niseme Hoja hii SIO kweli! Ni kutokuwa na Ufahamu wa Kutosha Kuhusu Kristo Yesu na Neema ya Mungu JUU ya Wanadamu  wote!

Kwa hoja zifuatazo,unaweza Ukajifunza,;

1.BWANA YESU KRISTO hakuja KUHUKUMU,Kila MTU ananafasi ya KUMWAMINI na AKAWA na UZIMA wa MILELE.

Ukishajua NIA Ya Kristo Yesu, ndiyo NIA Ya Mungu Mwenyewe!

Yeye hakuja  KUHUKUMU, Bali Kutupa HAKI ,UHURU na UZIMA wa MILELE.

Imeandikwa *" Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu."* Yohana 12:47

Yesu Kristo ni WOKOVU! na MWOKOZI Wetu 

Yeye haleti HUKUMU Bali KUOKOLEWA!

Yeyote atakayemwamini ANAOKOLEWA!

Imeandikwa *"Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye."* Yohana 3:17

Moyo wa BABA Mungu umebeba NIA na MAPENZI tele ya KUWAOKOA wanadamu  sio KUWAHUKUMU au KUWAANGAMIZA!

2.NI MAPENZI YA MUNGU WATU WOTE WAOKOLEWE,WASIFIKIWE NA HUKUMU YA ADHABU.

Yaani Mungu amekusudia watu *"Wote"* ,sasa kusema kuna wameandikiwa, kuhukumiwa  milele, sio sawa!

Nani amewaandikia? Mungu hajipingi mwenyewe!

Na ndio maana MAKAO yanaandaliwa kwaajili ya WATAKATIFU, hakuna mjumbe  wa Mungu anayeandaa JEHANAMU YA MOTO, Kwasababu NIA ya Mungu ni KUOKOLEWA!

Imeandikwa *"ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli."* 1 Timo 2:4

NIA ya MUNGU BABA,Ni watu wote wa OKOLEWE na Kujua yaliyo KWELI!

Kweli ya Kristo Yesu sio kutangaza hukumu JUU ya watu, Bali KUMFUNUA KRISTO YESU ili wamwamini na KUWA NA UZIMA wa MILELE!

Imeandikwa *"Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba."* 2 Petro 3:9

Wow! Mungu hapendi MTU yeyote apotee, Bali aifikilie TOBA!

Hivyo hapa,Nguvu ya Kuwaokoa watu hawa ni INJILI YA KRISTO ITAKAYOWALETA KATIKA TOBA!

Wakitubu,hakuna cha kuwahukumu, wala kuwazuilia Uzima wa MILELE!

Usione ,Yesu amesema atarudi, ukadhani *"Anakawia kana kwamba sio kweli"*   Ukweli ni kwamba *"YESU ANARUDI"*

Isipokuwa Subiria hii,ni Wema  wa Mungu watu wapate KUTUBU,wasipotee Bali WAWE na Uzima wa MILELE!
(Yohana 3:16)

3.BWANA YESU HAKUJA KUANGAMIZA ROHO ZA WATU,BALI KUOKOA!

Unaposema *"Mtu  anahukumiwa MILELE,maana yake Kazi ya Msalaba ni Bure, KWA kuwa Yesu Kristo amemwaga damu yake ya UKOMBOZI na MASAMAHA ya Dhambi! (Waefeso 1:7-8)

Imeandikwa *"Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. "* Luka 9;56

Bwana Yesu hakuja  kuangamiza roho za WATU,kuwaandikia WATU kuzimu,na uharibifu HAPANA!

Amekuja KUOKOA!

Nguvu za Kuokoa zina yeye! 

 _*"Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; 
Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana."*_ Zaburi 68;20

Ndiyo maana tunamhubiri kwa watu wote!

Awe muuwaji,mzinzi,kahaba,mchawi, MUNGU anaNEEMA ya Kumuokoa  MTU huyu!

Imeandikwa *"Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea."* Luka 19:10

Bwana Yesu anatafuta! Kilichopotea ili AOKOE!

Hapotezi MTU! Anatafuta MTU!

Hauhukumu MTU, anaokoa MTU!

Kila anayemwamini hata sasa,anahesabiwa Haki na Urithi wa Uzima wa MILELE!

Sasa, Nani ameandikiwa HUKUMU MILELE? Amefichwa wapi ambako  Bwana Yesu hawezi  kumwona?

Hakuna, NEEMA yake Inatosha KUOKOA! (Tito 2:11)

Jambo kubwa la KUFAHAMU sisi  Wahubiri kazi yetu ni KUIHUBIRI KWELI YA KRISTO YESU,KUMFUNUA BWANA YESU KAMA MWOKOZI WA ULIMWENGU,

Kuhusu KUMUOKOA mtu  ni KAZI YAKE yeye BWANA YESU!

Usitumie VITISHO na KUMHUKUMU mtu, Isivyopasa! Maana sio NIA ya MOYO wa BABA MUNGU!

MUNGU ANATUPENDA MNOO!

Tumemwamini YESU KRISTO Tunao UZIMA wa MILELE!

Hatuna  HUKUMU ya ADHABU tukiwa  KATIKA KRISTO YESU!

Asiyebadilika ni SHETANI, Watu wanabadilika!

Usiendelee KUKAA KATIKA DHAMBI na UOVU, Upokee na Uiamini NEEMA yake,bwana Yesu!

*"Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu."*  Warumi 8:1

🛐utukufu kwa Mungu
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: