Wenye Uhai Wanne Tulipokutana.

Leo jioni nilikuwa na hii tafakari na nikaona nishare na wewe ili tujifunze pamoja:


Mungu anapokuinua kwa kiwango cha juu kimamlaka siku zote kumbuka kuwainua watu wako ambao unawafahamu na mnasimamia kitu kinachofanana,la sivyo utapotea.

Baada ya Daniel kuinuliwa na mfalme Nebuchadnezzar mkakati wake wa kwanza aliufanya ni kuhakikisha kuwa anawaombea nafasi watu ambao ametoka nao mbali,wenye uwezo mkubwa katika majukumu anayowapa na wenye misimamo inayofanana na ya kwake.(Daniel 2:49). Kwa sababu ya heshima aliyokuwa nayo Daniel katika ufalme,ombi lake lilikubaliwa.

Utagundua kuwa watu hawa aliotamani aendelee kukaa nao pamoja hata mara baada ya kupanda juu ni wale ambao huko nyuma wakiwa watu wa kawaida walikuwa marafiki na walikuwa wanafanya mambo kwa pamoja ikiwemo kusaidiana wakati wa shida kimwili na kiroho pia(Daniel 2:17)

Ingawa Mungu alimtumia Daniel kupata majibu na kupata kibali mbele ya mfalme,ila alijua ili aendelee kufanikiwa zaidi ilimbidi asiwaache wale wenzake watatu.

Mungu atusaidie tusiwasahau wale tulioanza nao kimkakati.Ni hatari kuwa juu ukiwa peke yako.

See You At The Top

@joelnanauka_
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: