PHM PUGU-MUSTAFA
Mwl BRIGHT NYAHENDE
SOMO: IJUE BIBLIA NA TAFSIRI SAHIHI YA NENO 1.

Watu wengi wanafikiri Biblia kama neno la Mungu ni kitabu tu kilishushwa na kuelezea mambo ya Mungu na wanadamu,hasa kulingana na mapokeo na mafundisho wanayopewa.


Lakini ukweli ni kuwa Biblia ni kitabu kinacho elezea maisha halisi ya watu na Mungu jinsi walivyo husiana,hivyo lazima ujue huwezi kuelezea Biblia kwa usahihi pasipo kuangalia mfumo,historia na tamaduni halisi za walengwa.

Kutoka 1:1
"Basi majina ya wana wa Israeli walioingia Misri ni haya; kila mtu pamoja na jamaa zake walikuja pamoja na Yakobo." 

Kama kulikua na ukoo wa Yakobo na makazi na kumbukumbu basi ni maisha halisi ya watu.

Hivyo lazima ujue  kabla ya kutumia andiko aliandikiwa nani? Lengo lilikua nini na unawezaje kulitumia kwa wakati huu na likabeba maana ile ile iliyokusudiwa au unayokusaudia wewe kuwakilisha.

Lakini pia kuna watu wanamtazamo kuwa Biblia waliandikiwa watu hasa wasio mjua Mungu wa kweli,kwa agano la kale kwa sehemu sawa, lakini agano jipya kuanzia Warumi hadi ufunuo waliandikiwa wakristo walio mjua Mungu kabisa,either waliasi au waliendelea na utakatifu.

1Wakorintho 5:1
"Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye."

Unaona andiko kama hilo waliandikiwa wakristo kabisa wa Korintho,ni mji ulio na kumbukumbu na historia kamili hivyo lazima ung'amue andiko ilo unaitaji maarifa ya kuelewa na roho pia akusaidie.

Tutajifunza kanuni chache kama 5 muhimu za kukusaidia kutafsiri mafundisho ili ata ukifundishwa uwe na mwangaza wa kujua kipi ni sawa na lipi si sawa.

@mwl nyahende bright
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: