HISTORIA YA MAJITU YA KALE YA KUTISHA (NEPHILIM)

LEO TUANGALIE HISTORIA KWA UFUPI..
(maestro).

Unawafahamu Wanefili? Ama watu wakubwa ama majitu ya nyakati hizo? Je goliathi umeshawahi kumsikia? Yule jitu akiyekatwa kichwa na daudi na kulishwa kwa ndege? .... ok sawaa,kuna mtu anaitwa OG ama mfalme OG,King of bashan,umeshawahi kumsikia???
👉Kama hujawahi au umewahi,ngoja nikuelezee historia yao kidogo..


Historia.
Wanefili ni majitu wazamani ambao walikuwa miili mikubwa na wenye nguvu sana kuliko wanadamu wa kawaida,kutokana na nguvu zao,waliweza kutawala wanadamu katika pande zote za dunia....walitoka wapi hawa?

Wanefili hawa ni viumbe ambao Mungu hakutaka wawepo,wametokea kutokana na mmomonyoko wa maadili...

Kuna baadhi ya vitabu kwenye biblia vilitolewa kwa sababu zisizojulikana mpaka sasa..moja ya kitabu hiko ni kitabu cha enock ambacho kimebeba historia kubwa ya asili ya ulimwengu huu.Unaweza ukawaza kuwa labda walivitoa ili binadamu tusijue mambo mengi ya siri,au wanasababu zao wenyewe za kuvitoa,je ni wakina nani hawa waliotoa? Ni maswali mengi ambayo ukiyafikiria sana unaweza ukaumia kichwa,ila siku zijazo nitajitajihidi kukufungulia ukweli wa jambo moja moja kwa kadri Roho wa Mungu atakavyo niwezesha.
------
Sasa tukirudi kwenye kitabu cha enoch, ndicho kitabu pekee kilichoelezea kwa undani juu ya hawa majitu,kinasema hawa majitu ni matokeo ya malaika walioanguka kukutana kimwili na wanadamu wakike na kuzaa wanefili ama majitu. Ndio,ni wanadamu wakike tu,hii ni kwasababu,hakuna ushahidi wowote kimaandiko unaoonyesha kama kuna malaika wa kike. Kwahiyo malaika wa kiume ndio waliohusika kwenye dhahama hii. Na kuzaliwa kwa watu hawa,ndicho kilikuwa chanzo kikuu cha Mungu cha kuleta gharika duniani. Lakini utaweza kujiuliza,mbona baada ya gharika,majitu wanaendelea kuonekana duniani? Mfano mfalme OG mbona anaonekana akiendela kufanya vita na Musa? Ni swali gumu ila nitalijibu siku nyingine...

Tuangalie kidogo ushahidi wa kibiblia..

Mwanzo 6:1-
(Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao, wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini. Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
MWA. 6:1‭-‬4 )

Hapo kuna neno "WANA WA MUNGU" pia "BINTI ZA BINADAMU"

Biblia ya ya kiingereza inawaita SONS OF GOD ikimaanisha wana wa Mungu na DAUGHTERS OF MEN  ikimaanisha binti za wanadamu... hawa binti za wanadamu wanaozungumziwa hapa ni binadamu wa kike na wana wa Mungu wanaotajwa hapa ni hawa malaika,lakini walaika waasi,ambao waliasi mbinguni na kutupwa. Kumbe hawa malaika ndio waliafanya dhambi hii kubwa mpka Mungu akachukia na hasira yake kuwaka.

Unaweza ukawa na maswali mengi kuhusu hawa sons of God,ila naomba nikutoa wasi ya kwamba,kutokana na biblia yenyewe na ushahidi wa kihistoria,hawa sons of God wamethibitika kuwa malaika waasi...

AYUBU 1:6
'Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu(sons of God) walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao.
AYU. 1:6 '

Hapo ni kipindi malaika wameenda mbele za Mungu kwa ajiri ya shughuli zao,biblia imewaita hawa malaika kama wana wa Mungu ama sons of God. Kumbe sons of God ni malaika. 

Na hawa malaika ndio wahusika wakuu wa dhambi hii ya kuzaliana na wanadamu wa kike,na huu ndio ulikuwa mwanzo wa hawa majitu ama wanefili..

Baada ya dhambi hii,Mungu alichukia na ikawa moja ya sababu ya gharika kuu,na nuhu peke yake ndiye aliyepat kibali mbele za Mungu.

Baada ya gharika biblia inasema,ni watu nane tu walisalia duniani,yaanu Nuhu na familia yake...swali je,majitu yanayoonekana baada ya gharika,yalitoka wapi.

KatiKa kipindi kingine cha historia,nitajibu hilo pamoja na kumtazama mfalme wa bashani,OG.

Ahsante.
(Tzworships.blogspot.com)
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: