JE,YESU ALIONEKANA KWENYE AGANO LA KALE? NA UKWELI KUHUSU MELKIZEDEKI.

Kuna swali moja ambalo watu wengi wanajiulizaga,je Kuna sehemu Yesu alionekana kipindi cha agano la kale? Limekuwa ni swali gumu kidogo ila leo utapata jibu  ambalo na wewe litakupa upana wa kuendelea kutafakari.
---



Kwanza ni vizuri tufahamu ya kuwa Yesu ni yeye yule jana leo na hata milele,hii ikimaanisha hata kabla ya kuzaliwa na bikira mariamu,Yeye alikuwepo na ndio maana kuna sehemu anaitwa mzee wa siku,eh ndio mzee wa siku kwa sababu alikuwako hata kabla ya misingi ua dunia haijawekwa...
(YOHANA 1:1-5)- Ndiye anayehusika na ujenzi wa kila kitu unachokiona na usichokiona.
---
Turudi kwenye swali. 
Katika kitabu cha Yohana sura ya 8,Kuna majibizano  yanaendelea pale kati ya Yesu na wayahudi.Yesu alikuwa anajaribu kuwaambia yeye ni nani na ametoka wapi.Katika sura hii ya nane ndipo unapoweza ukapata mwanga juu ya swali letu ya kwamba Yesu alionekana kwenye agano la kale? Na wapi?.
---
Katika sura hii ya 8,Yesu anawaambia wayahudi kuwa Yeye ametumwa na Mungu baba,na Mungu ni Baba yake. Watu wote walichukia kutokana na maneno ya Yesu kwa sababu alikuwa anamaanisha Yeye ni Mungu,ila kilichokuja kuwachukiza zaidi ni pale Yesu aliposema kuwa AMESHAWAHI KUKUTANA NA BABA IBRAHIMU. Raia walichukia kwa sababu,ibrahimu alikuwa zaidi ya miaka 2000 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu,sasa inawezekanaje Yesu amuone wakati hata miaka 50 hana. Tuangalia kidogo maandiko.

'Ibrahimu, baba yenu,alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe hujapata bado miaka hamsini, nawe umemwona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko.
YN. 8:56‭-‬58 '

Yesu anasema wazi kuwa alikutana na Ibrahim na kabla ya Ibrahim yeye alikuwako tayari. Kumbe huu mstari unatupa mwanga ni wapi Yesu akionekana kwenye agano la kale,kama alikutana na Ibrahimu,basi inabidi turudi kwenye historia ya ibrahimu,tutafute ni wapi ambako ibrahimu alikutana na mtu ambaye anaweza akawa Yesu kristo.
----
Sehemu pekee ambayo Ibrahim anakutana na mtu ambaye anaweza akatupa majibu ni katika MWANZO 14 ambapo ibrahimu anakutana na mtu wa ajabu kipindi anatoka kwenye vita. Anakutana na mtu anayeitwa MELKIZEDEKI ambaye ni MFALME WA SALEM,hakujulikana ametokea wapi,alikutana ghafla tu na ibrahimu.Embu tuangalie vitu vichache.

Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi.
MWA. 14:18‭-‬19 '

Kuna vitu vitatu vya kuangalia hapa.
1. MELKIZEDEKI ALIKUWA MFALME WA SALEM
2. ALIKULA MKATE NA DIVAI PAMOJA NA IBRAHIMU(USHIRIKA NA MUNGU).
3.ALIKUWA KUHANI ( PRIEST OF MOST HIGH).

Kitu cha ajabu ni hiki,katika biblia makuhani wote wa Mungu sio wafalme na hawajawahi kuwa wafalme,ila huyu melkizedeki,anaonekana kuwa kuhani na mfalme...
---
Infact kuna mtu mmoja tu kwenye biblia ambaye anatajwa kama kuhani na mfalme na anatajwa kwenye maagano yote mawili,huyo si mwingine ni kristo.Je hii inamaanisha nini? Tumeanza kupata mwanga kidog?...

Tuangalie hapa...

'BWANA ameapa, Wala hataghairi, Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki.
ZAB. 110:4 '

Huyu ni Yesu anayetajwa hapa kuwa ni kuhani.

Tuangalie pengine.

'Naam, yeye atalijenga hekalu la BWANA; naye atauchukua huo utukufu; ataketi akimiliki katika kiti chake cha enzi; na kutakuwa na kuhani katika kiti chake cha enzi; na shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili.
ZEK. 6:13 '

Kumbe Yesu ndiye mtu pekee ambaye ni kuhani na mfalme.
(ISAYA 9:6-7).

Ndio maana ni kitu cha kushangaza sana kuona Ibrahimu amekutana na huyu mtu ambaye ni kuhani na mfalme,na kufanya ushairika nae(communion).

Pia biblia inasema,Melkizedeki alikuwa mfalme wa salem. Je unajua kuwa sehemu in nayoitwa salem haijawahi kupatikana? Yani hakuna sehemu duniania inayoitwa SALEM. Kiharisia,Salem sio sehemu ila ni maana ya kitu. Salem kutokana na tafsiri ya kiebrania maana yake ni Amani. Kumbe melkizedeki alikuwa mfalme wa Amani. Inashangaza e? Ibrahimu anakutana na mtu ambaye ni kuhani,mfalme na mfalme wa amani..cha kushangaza zaidi ni hiki,kuna mtu mmoja tu kwenye biblia ndiye anayejulikana kama mfalme wa amani,naye ni Yesu kristo.

Unaweza ukawaza kuwa kama kunasehemu Yesu alionekana kwenye agano la kale,basi ni huyu melkizedeki.

Yesu anasema alikutana na ibrahimu,na tunaona hapa kuwa ibrahimu alikutana na mtu ambaye kwanza ni Kuhani mkuu,pili ni mfalme wa amani na tatu wakafanya ushirika(communion).

Tuangalie kitu cha mwisho ambacho kitamaliza mjadala huu.

alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.
EBR. 6:20

Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao wafalme, akambariki; ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote; (tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana yake, mfalme wa amani; hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
EBR. 7:1‭-‬3

Kwa maandiko hayo utagundua vitu vingi sana.kwa mfano.
1.Kumbe hata maana ya neno Melkizedeki ni mfalme wa haki.
2.pia huyu melkizedeki hana baba wala mama.
3.hana mwanzo wala mwisho.
4.ni mfalme wa amani.
5.Adumu kuhani milele.

Ni nani huyu MELKIZEDEKI?

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: