🌱Tzworships bible study
 #Kitabu cha mwanzo - 2

 Shallooom.

 leo tutaendelea kidogo na kitabu cha mwanzo 1 hasa mistari mitano ya muhimu. MWANZO 1:14 - 19 ambaku kuna habari ya jinsi Mungu alivyoumba jua na mwezi kama mianga mikuu miwili


MIANGA MIKUBWA MIWILI (JUA NA MWEZI)

" Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na siku na miaka; tena iwe ndiyo mianga katika anga la mbingu itie nuru juu ya nchi; ikawa hivyo. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi na kuutawala mchana na usiku na kutenga nuru na giza; Mungu akaona ya kuwa ni vyema. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya nne. MWA. 1:14-19"

 Kuna picha nzuri tunaipata hapa kwenye hiki kifungu.Mungu anaumba mianga mikubwa miwili,mmoja mkubwa utawe mchana,nao ni jua na mwingine mdogo utawale usiku (mwezi). katika tafakari ya hii kitu utagundua kuwa mwezi hautoi mwanga wake wenyewe,mwanga wote wa mwezi unatokna na jua. jua linapowaka,mwezi hunyonya mwanga wa jua na ndipo unapokuwa na uwezo wa kutoa mwanga ikifika usiku. Ile sehemu ya mwezi inayoonekana ,ni kipande ambacho ndicho kilichopata mwanga wa jua wakat wa mchana..

Naamini unajua tunapoelekea hapa.. Jua (the sun) ni mfano wa mwana(son) Yesu kristo.Yesu ni nuru halisi na kamili ya ulimwengu,mwezi ambao ni kitu tu na hakina uzuri wowote mpka jua liuangazie ni mfano wa kanisa ambao ni mm na ww. kuangaza kwetu kunategemea hasa ni kiasi gani cha nuru tumeakisi kutoka kwenye jua ambalo ni kristo yesu. Kuna kitu kimoja ambacho kufanya mwezi usipate mwanga kamili kutoka kwenye jua,nacho ni dunia...

dunia ikikaa katikat ya mwezi tunaita kupatwa kwa mwezi. mwezi unashindwa kupata mwanga kutoka kwenye jua..na huu tunita upagani ama kutomfahanu Yesu kabisa. Na kuna scenario ya pili ambayo dunia inakaa katikat ya jua na mwezi,ukumbuke mwezi ni sawa na kanisa..dunia ikikaa katikati ndipo pale kanisa linakuwa linafundisha habari zake na Yesu hayupo🌚🌚🌚

....... Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu. Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza. YN. 1:4‭-‬5 Hii ndiyo taswira halisi ya jua na mwezi. Ni maombi yangu tuweze kuakisi nuru kamili kutoka kwenye Jua.

Tukutane sehemu ya 3
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: