Sala ya Bwana ni sala ambayo Yesu kristo aliwafundisha wanafunzi pale walipomuuliza jinsi ya kusali..

Sala hii inapatika katika mathayo 6:9-13 na Luka 11:2-4


Mathayo 6:9-13 
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,   Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.  Utupe leo riziki yetu.   Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.   Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.
Watu wengi tunaamini kuwa ,sala ya Bwana ni sala ambayo tunatakiwa tukariri kila neno,na wengine wanaamini kuwa sala hii ina nguvu fulani ambayo inaweza kumshawishi Mungu kufanya jambo

Biblia inaongea tofauti kabisa juu ya jambo hili. Mungu anaangalia zaidi mioyo yetu wakati wa amaombi kuliko maneno yetu.

MATHAYO 6:6-7
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atawajazi.
Mungu anahusika na roho zetu.Sala ya Bwana ni kama formula tu yakuifuata muda wa maombi.

"BABA YETU ULIYE MBINGUNI' inatufundisha kuwa sala zetu zote lazima zielekezwe kwa Mungu baba, "JINA LAKO LITUKUZWE" kuwa ni Mungu pekee ndiye wakuabudiwa. "Ufalme wako uje,   Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni" hii unatukumbusha kuwa katika maombi lazima tuache mapenzi ya Mungu yatimizwe,kile Mungu anataka ndicho kifanyike na sio mawazo yetu sisi tu. 

"Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu." huu ni mstari unaotukumbusha kutubu,lakin sio kutubu tu,kutubu wakati tayari tumeshawasamehe na sisi wale waliotukosea.

 "Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina." mwishoni kabisa ni kifungu cha ulinzi,kumuomba Mungu atulinde na kila hila za adui.

Sala ya Bwana sio ya kukariri.
Je,kuna ubaya kukariri? HAPANA

Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.
FLP. 4:6‭-‬7
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

1 comments:

  1. Barikiwa sana mtumishi wa Mungu alie hai.

    ReplyDelete