FAIDA ZA KUWA NA JUHUDI KATIKA MAMBO YA UFALME WA MUNGU,faida za mungu,matunda ya roho,kuwa na Mungu,Faida za yesu
Bwana YESU KRISTO Mwokozi atukuzwe ndugu yangu. Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Unapojibidisha katika mambo ya ufalme wa MUNGU ndipo MUNGU hujishughulisha na mahitaji yako.
Unaweza kujibidisha kwa MUNGU naye MUNGU akajishughulisha na wewe kukuondolea magonjwa, vifungo, matatizo n.k
Ndio maana Biblia iko wazi sana ikisema kwamba utafute kwanza ufalme wa MUNGU maana hayo mengine unayohitaji utapewa.
Mathayo 6:33 "Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa."Image result for african american family praying together
Inawezekana wewe unatafuta sana MUNGU akutoe kwenye tatizo, unasahau kwamba inakupasa kwanza kuutafuta ufalme wa MUNGU.
Watu wengi ukiwauliza wanahitaji nini katika maisha yao inawezekana kabisa katika watu mia moja utakaowauliza watano ndio watasema wao wanauhitaji ufalme wa MUNGU kwanza ila hao 95 waliobaki watasema wanahitaji kwanza pesa, mke mwema,mume mwema, kazi, gari, nyumba, utajiri n.k

Watu hao wamesahau kwamba tumeagizwa na Bwana YESU KRISTO kwamba tuutafute kwanza ufalme wake na hayo mengine tunayohitaji tutapewa.
Ndio maana hata kwa watumishi wa MUNGU inakuwa shida pale ambapo anakuja mtu anataka umuombee apate hitaji lake, ukimwambia aokoke kwanza mnaweza kukosana maana yeye hataki ufalme wa MUNGU ila anataka tu ufalme wa MUNGU umponye kisha arudi kwenye ufalme wa shetani alikokuwa mwanzo.
Mama mmoja alinifuata nimuombee apone kifua ambacho kinamtesa kwa miaka mingi, wakati anasema nilishuhudiwa kwamba anateswa na majini na katika maongezi yeye mwenyewe akasema kwamba anahisi anateswa na majini 20 maana pia huwa yanamtokea na kumtesa. Kwa sababu ya maadui zake hao nikaona nimshauri jambo muhimu zaidi ambalo litahifadhi ushindi wake ili usiwe ushindi wa siku chache tu kisha tatizo linarudi, nilimwambia ampokee YESU KRISTO kama Mwokozi wake hapo ndipo atakuwa ndani ya ufalme wa MUNGU kiasi kwamba akizingatia katika KRISTO majini wale wanaomtesa hawatakuwa na uhalali tena kwake.

Mama yule alinipa jibu ambalo sikuwahi kuambiwa.
Mama yule alisema yeye hamuhitaji YESU KRISTO na Wokovu wake, anahitaji tu kupona ili aendelee na dini yake.
Nilishangaa mno yaani mtu anatangaza kwamba hamhitaji YESU KRISTO na huku anataka watumishi tumuombee ili apone, amesahau kwamba Mimi kama Mtumishi wa MUNGU sina uwezo wa kumponya yeyote hata kama anaumwa ugonjwa mdogo wa mwisho, mponyaji ni YESU KRISTO na sio Mimi Mtumishi wake.
Mama yule alisema anahitaji kupona ila hamtaki YESU anayeponya.
Nikabaki njia panda juu ya kumuombea huyo mama, ila huo ni mfano mmoja tu kati ya mingi sana ya watu wanaohitaji MUNGU awatendee wanachohitaji ila wao hawahitaji ufalme wake.

Kuna watu hufanya hata huduma za maombezi ziwe ngumu sana kwa sababu wao wanataka YESU KRISTO awaponye ila hawamhitaji wala kumwamini.
Ndugu zangu, kwa kusoma kwangu Biblia Mimi Peter Mabula sijawahi kuona mtu hata mmoja aliyeponywa na YESU bila kumwaminiYESU.
YESU KRISTO hakumponya asiyemwamini bali aliponya wakiomwamini.
Mfano hai ni huu.
Mathayo 9:28-30 " Naye alipofika nyumbani, wale vipofu walimwendea; YESU akawaambia, Mnaamini kwamba naweza kufanya hili? Wakamwambia, Naam, Bwana.

Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. Macho yao yakafumbuka. ......."
Watu wengi leo hawamwamini YESU wala kumhitaji ila wanataka watendewe miujiza na yeye, ndugu haiko hivyo.
Tafuta kwanza ufalme wa MUNGU ndipo hayo unayoyahitaji yatakufuata.
Related image
Ndugu, sijui kama unafahamu kwamba kutokumwamini YESU KRISTO kunaweza kupunguza kutendeka miujiza?
Mathayo 13:58 "Wala hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu ya kutokuamini kwao."


Hata kwako miujiza ya YESU KRISTO inaweza kupungua kwako au isiwepo kabisa miujiza kwako kwa sababu tu humwamini YESU KRISTO ambaye ndiye anayeweza kukutoa katika tatizo lako na ndiye anaweza kukupa hitaji lako.
Ndugu utafute kwanza ufalme wa MUNGU na haki yake.
Kumwamini YESU KRISTO ni sehemu kuu ya haki inayopatikana katika ufalme wa MUNGU.
Inawezekana unataka Mume/Mke mwema kutoka kwa MUNGU, ndugu mtumikie Bwana YESU KRISTO maana ukiwa Mtumishi wake sahihi yeye hawezi kukupa mke/mume aliye tanzi kwako, atakupa mke/mume mwema ili wote muendelee kumtumikia katika ufalme wake, labda tu kama hukumsikiliza ROHO MTAKATIFU alipokuwa anakusemesha juu ya Mwenzi wako wa ndoa hivyo ukaongozwa na tamaa zako kumpata mwenzi wako ndio maana ndoa yako imekuwa jaribu la kukurudisha nyuma.
Hata hivyo kwa maombi unayo nafasi hata leo ya kumwambia MUNGU aifinyange upya ndoa yako, ila kama hujaingia katika ndoa usithubutu kutokumsikiliza ROHO MTAKATIFU.
Ndugu, utafute kwanza ufalme wa MUNGU ndipo mengine utapewa,utazidishiwa na kuongezewa.
Luka 12:31" Bali utafuteni ufalme wa MUNGU, na hayo mtaongezewa."
Unapokwenda Kanisani nakuomba jambo la kwanza ni kwenda kuutafuta kwanza ufalme wa MUNGU.
Usiende kufuata baraka zako tu, ukifuata baraka unaweza hata kuangukia kwenye kudanganywa kwa kupewa maji ya upako,mafuta ya upako, sabuni za upako, vitambaa vya upako, juice za upako, barafu za upako, keki za upako n.k na vyote hivyo umetumia pesa nyingi kuvipata na hakuna msaada hata mmoja katika vitu hivyo.
Kwanini wengi wanaibiwa?
Ni kwa sababu wanakosea kanuni ya ki MUNGU.
Kanuni ya ki MUNGU inasema utafute kwanza ufalme wake ndipo baraka zitakufuata lakini wewe kwa kutokujua unatafuta kwanza baraka kisha hata ufalme wa MUNGU huuhitaji.
Kwa kufuata baraka tu ndio maana wengi wanaibiwa.
Ndugu, utafute kwanza ufalme wa MUNGU katika KRISTO YESU.
Kama unautafuta ufalme wa MUNGU Biblia iko wazi sana ikisema kwamba MUNGU atajishughulisha na mambo yako.
1 Petro 5:6-7 " Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa MUNGU ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu."
Naamini umeelewa sasa na utautafuta ufalme wa MUNGU kwanza.
Fanya mambo yaliyo katika ufalme wa MUNGU.
Mtumikie Bwana YESU KRISTO, toa matoleo sahihi mbele za MUNGU, shuhudia watu injili, walete watu kwa YESU KRISTO na fanya kila kilicho ndani ya ufalme wa MUNGU.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU la siku ya leo ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
Bwana YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na Bwana YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee Bwana YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa Bwana YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la Bwana YESU.
0714252292 
0786719090

Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: