Kuna misemo mingi ya kibinadamu inasemwa juu ya vita,ikiwemo "kumjua adui yako ni nusu ya ushindi wako vitani,au kujua silaha anazotumia adui yako ni sawa au unahesabika kama umeshashinda vita teari"

Hii ni kwa sababu,ukijua silaha za adui yako inakipa wewe muda mzuri wa kujipanga na kuchagua silaha bora ambazo kwazo utakuwa na uhakika wa kumshinda adui yako.

Biblia inamtaja shetani(dhambi) kama adui yetu sisi waamini..Ninasema shetani kwa sababu ndiye Baba wa dhambi
YOHANA 8:44-45

Sasa kumshinda shetani na dhambi inabidi kwanza kumfahamu shetani vizuri pamoja na mipango yake...Katika HOSEA 4:6 Mungu anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa,hajasema wanaangamizwa na shetani,hayo maarifa ambayo mungu anazungumza ni ya kumjua sana mungu na kumfahamu shetani na utendaji kazi wake ili tuweze kumkabiri.

2WAKORINTHO 2:11
"Hatukosi kuzijua fikra za shetani"

Sasa leo tuangalie maeneo au mambo makuu mawili  ambayo shetani anayatumia ili kufanikisha mipango yake ya upotofu:

1.ANAPOFUSHA ZA WAAMINI

-2WAKORINTHO 4:3-4
Hapa tunaona kuwa sehemu kubwa ambayo shetani anaitendea kazi ni fikra au akiri za wanadamu hasa waamini ili ahakikishe zile baraka na neema za yesu Kristo haziwafikii. 

Kazi yake kubwa ni kuhakikisha anawajaza waamini uongo ili wazidi kuwa mbali na utukufu wa mungu
WAEFESO 2:1-3

2.ANAWATESA WAAMINI ILI WATOKE/WAWE MBALI NA NEEMA YA MUNGU

Hii ni moja ya njia kubwa ambayo shetani anaitumia ili kuhakikisha tunaoamini tunamsahau Mungu au tunakuwa mbali na Mungu kwa kuwa bize na matatizo ya kila siku.

Alifanya hivyo kwa Ayubu lakini ashukuriwe Mungu ayubu hakufanya dhambi.
Kwa muda wako pitia haya maandiko chini ili ujue jinsi shetani anavyofanya kazi
WAEFESO 6:12
ZAKARIA 3:1
WAGALATIA 3:1-2
Mungu atusaidie tuweze kupigana vita vya ushindi.
Visit: Tzworships.blogspot.com
@Mwl Nuruel
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: