kanisa la GRC ubungo kibangu linaloongozwa na mtumishi wa mungu Anthony Lusekelo marufu kama mzee wa upako ambaye naye alikuwa na yabkusemajuu ya afya na Tukio zima la uvamiwaji wa mh Tundu anthipasi Lissu Dodoma wiki iliyopita. Mzee wa upako katika akaunti yake ya instagram aisema haya.
"Tusitumie tatizo la ndugu yetu Tundu lissu kujipatia umaarufu wa kisiasa au wa kidini.Mtu yeyote anayetumia tukio hili kujipatia umaarufu wa kisiasa au wakidini namfananisha na wale wahuni ambao basi likianguka wanaenda kuchukua simu kwanza.Ni jambo ovu sana na wewe unakuwa ni sehemu ya waliompiha risasi Tundu lissu.
Aliendele
" Mwenzako anaumwa wewe unatumia ugonjwa wake kujipatia umaarufu wa kidini au wa kisiasa ni jambo baya sana,mbona sikusikia wakilaani mauaji ya kibiti au kuitisha maombezi ya watu wa kibiti wakipouwawa,mbona hawaja laani utekaji na mauaji ya watoto Arusha na wa marekani,Najua wanatumia matatizo yabTundu lissu kujiongezea daraja la umaarufu la kisiasa ama kidini.Natumia lugha ya kibantu ni Mwiko,Ni mwiko tubaki kuwa wamoja tuviache vyombo vya dola vifanye kazi yake."
Alisema
Post A Comment:
0 comments: