Mwalimu mmoja aliita wanafunzi wake akawaambia''Kesho kila mwanafunzi aje na nyanya kulingana na idadi ya watu anaowachukia, Yaani kama unamchukia mtu mmoja uje na nyanya moja kama ni wawili basi njoo na nyanya mbili vilevile.

Nyanya hizo mtazibeba kwenye mabegi yenu ya kubebea madaftari na vitu vingine vya shule*
"Wanafunzi wakakubali halafu kesho yake wanafunzi wakazibeba zile nyanya vizuri kabisa wengine walibeba moja,wengine mbili na wengine nyingi sana.

Kama mwalimu alivyosema zile nyanya zikapewa majina ya watu ambao wanafunzi wanawachukia
Baada ya kuzipa hizo nyanya majina mwalimu, akawaambia kila mwanafunzi azirudishie nyanya zake kwenye begi lake halafu aziache humo humo ndani ya begi kila siku awe anakuja nazo shuleni na kurudi nazo nyumbani.
Baada ya siku kadhaa wanafunzi wakaanza kulalamika hasa wale waliobeba nyanya nyingi kuwa nyanya ni nzito sana na zinatoa harufu mbaya na zinaharibu vitu vyao vizuri walivyoweka kwenye mabegi yao


Mwalimu akawaambia hivi ndivyo ilivyo mtu unapoweka watu usiowapenda moyoni
kama mtu huwezi kuvumilia kukaa na harufu ya nyanya, kwenye begi vipi kuhusu madhara ambayo moyo wako unayapata kwa kuubebesha mzigo wa chuki dhidi ya watu.?
Moyo unapata madhara makubwa sana unapobebeshwa chuki kila wakati kila siku moyo unakuwa na chuki na hapo ndipo unaharibika, na kusababisha kuharibu hata vitu vingine vizuri vilivyokoko moyoni mwako. Moyo ni kama lile begi la kubebea madaftari unahitaji kubeba vitu vizuri na visivyo na chuki ndani yake
Safisha moyo kwa kusamehe wanaokukosea, jifunze kusamehe maana ni moja ya virutubisho vya moyo wako,Samehe kwa kila anayekukosea na kukukwaza



Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: