Leo nimeona nikujuze baadhi ya sifa za mapepo ambazo wengi labda hawazijui au hawazijui kwa undani,ila leo itazijua.


Mapepo ni viumbe vilivoasi mbinguni pamoja na baba yao shetani na kutupwa nje mpka nchi. (Mikaeli na malaika zake ndiyo waliopigana vita na shetani na kumtupa nje ya mbingu akiwa na jeshi lake ambao ni mapepo walioasi pamoja naye).

Zifuatazo ni sifa za hawa mapepo.

1. WANACHOKA
2.WANAFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO
3.WANAAKIRI SANA/INTELLIGENCE 
4.WANAKUMBUKUMBU.

Soma kwa makini haya maandiko,utagundua.

Pepo mchafu, amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika, asipate. Halafu husema, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; hata akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa. Mara huenda, akachukua pamoja naye pepo wengine saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kibaya.
MT. 12:43‭-‬45 
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

2 comments:

  1. Bwana Yesu asifiwe.
    Mapepo sio malaika walioasi. Bali mapepo ni kizazi cha wanefili ambao waliangamizwa wakati wa gharika kuu. Baada ya wale malaika waangalizi wa dunia kushuka na kutembea na binti za wanadamu na hatimaye kuzaa nao Mwanzo 6:1-6 Watoto waliozaliwa waliitwa wanefili ambao ndio walikuwa watu hodari sana maana walifundishwa siri nyingi za mbinguni na baba zao hao malaika waliotembea na wanadamu. Kizazi hiki kilikuwa ni viumbe wakubwa na wao walikuwa na tabia mbaya na kuanza kutembea tena wao kwa wao na kuzaa viumbe vya ajabu sana vyenye maumbo tofauti tofauti. Na tabia zao zilikuwa za ajabu maana walianza kula wanadamau na vitu tofauti tofauti. Na kwa sababu ya hawa dunia ilijawa na uasi na uovu mwingi sana. Na hawa ndio sababu ya Mungu kuachia gharika. Viumbe hivi viliteketezwa vyote pamoja na wanadamu wengi wlioasi na kutofuata shria na amri za Mungu, hivyo ilibaki familia ya Nuhu tuu. Ni vyema tukumbuke kuwa ROHO huwa haifi, hivyo roho za hao viumbe ndio leo hii huitwa mapepo na ndio sababu kubwa mtu anapokuwa na mapepo huonyesha tabia za ajabu ajabu maana ndio tabia halisi za wale wanefili na watoto wao.
    Majini hutengenezwa huko kuzimu na shetani mwenyewe, hivyo unavyopambana nae katika vita ya kiroho ni kumtia hasara maana hupukutika na kuisha.

    Ufnunuo 12:7-8

    ReplyDelete
    Replies
    1. Biblia inasema shetani alitupwa na malaika zake? ni wakina nani hawa malaika waliotupwa pamoja na shetani na wanakadiriwa kuwa zaidi ya theluthi moja ya malaika wote wa mbinguni ndio waliofuatana na shetani

      Delete