Ndoa ni rahisi sana lakini muda mwingine inaweza ikawa ngumu sana. Ndoa ni kitu kikamilifu ambacho kinaundwa na watu wawili ambao sio wakamilifu..instaajabisha e? Unaweza jiuliza ni kivipi ndoa iweze kutengezwa na watu wawili wasio wakamilifu lakini ndoa yenyewe ikawa kamilifu?
Jibu ni rahisi mnoo....Hawa wawili wasio wakamilifu kazi yao kubwa ni kufanya juhudi kufikia ule ukamilifu wa ndoa ambayo Mungu kama fundi wa kwanza wa ndoa,ndivyo alivyoikusudia uwe pale edeni.
-------
Katika ndoa,mwanaume anakuwa na tabia zake,mwenendo wake ,aina yake ya maisha,vile vile kwa mwanamke. KAZI inapokuja ni pale ambapo hizi tabia za watu wawili zinapishana.
------
Leo,nitakueleza mambo 5 ambayo yatakusaidia kuirudisha ndoa yako kwenye mstari.

MAMBO MATANO (5).
 
1.JITAHIDI UMGUSE MWENZAKO (TOUCH THEM).
-Ni kitu rahisi sana si ndio? Ila subiri,mara ya mwisho lini ulimshika mpenzi wako? Simaanishi kile kinachoendelea chini ya shuka (tendo la ndoa),naongelea kushika kama kushika.Nakuhakikishia,kumgusa mpenzi wako kwa mguso wa upendo,kutafanya muwe na muunganiko wa kudumu...Watu tunapenda kupendwa,tunapenda kuguswa....nitakueleza ni kwa namna gani...

Tendo la ndoa pekee halitoshi,mi pale ambapo mpenzi wako ametoka kazini,ukampokea kwa kumkumbatia,ukambusu (kiss),kumbusu mpenzi wako asubuhi au unapomuona,kumfuata akiwa amekaa kwenye kiti na kushika kichwa chake,mabega na kumhug kwa nyuma,hata usipoongea kitu,lazima ajihisi vizuri na kupendwa. Enda ofisini kwa mkeo na bites kama snacks mkiss shavuni mpe bites,ni vitu vidogo sana lakini vimebeba gharama kubwa ua upendo.Kaeni pamoja kanisani,angalien8 tv pamoja nyumbani,mfanyie mpenzi wako massage hata kama hujui....trust me,utafanikiw.

2.KUWA MPOLE
-Hii pia ni rahisi sana. Kuwa mpole maana yake usiwe na hasira za ghafla,usiongee maneno makali kwa mpenzio,usimdhalilishe wala kumkashifu mwenzako mbele ya watu,ongea maneno mazuri kwa sauti na sura ya upole.elewa wanapokuwa wamechoka au wametingwa na kazi. Kuna kitu wengi kinatushindwa,mpenzi wako anapoongea msikilize kwa makini,usifanye mambo mengine kama mpenzi wako anaongea jambo la muhimu,
-------
Kuna siku nilisikia mwanaume anasema "mimi mke wangu nimempa maisha yangu" mwanamke akajibu "maisha yako hata siyataki,ila upike mara moja moja" hahaha...dahh..haya bwanaaa

3. AHSANTE KWENYE MAHUSIANO. 
-Mara ya mwisho kumwambia mpenzi wako ahsante ni lini? Je ni kipindi kile bado wapya wapya? Unaendelea kusema hivyo?.....
Basi ngoja nikwambie,ahsante ni neno lenye nguvu sana,ni neno lenye uwezo wa kugeuza hasira na kuleta tumaini lingine,ni neno ambalo ukitamka,linamaanisha heshima ama respect,linaonyesha unatambua mchango wa mwenzako kwenye hilo jambo. Wengine husema,kwanini nisema ahsante wakati vyombo kuosha ni kazi zake? Haijalishi,kusema ahsante inamaana unatambua mchango wake kwako kupitia kuosha vyombo.Maneno yana nguvu sana,ukumbuke Mungu hakuwa na roli la mchanga wakati anaumba dunia na kila kitu,alitumia neno tu na ndio yeye aliyesema tuwe watu wa shukrani siku zote. Pia usisahau kusema neno zito.... NAKUPENDAA

4.BE PRESENT (UWEPO WAKO WA SASA)
-Hii nitaifupisha lakini utaelewa...tunavyosema uwe present maana yake,uwe mfuatiliaji wa details ndogo ndogo. Kwa mfano,muulize mpenzi wako anaendeleaje,siku yake ikoje,watoto wanaendeleaje,umekula?...muda huu weka simu pembeni,zima tv ongea na mama/baba watoto kwa umakini.

5.MUWEKE MBELE KWA KILA JAMBO (PUT THEM FIRST).
-Mama alishawahu kuniambia,ukiwa na ndoa yako tu,Kila ukiamka muwaze mwenzako,waza utamfanyia nini kipya au utafanya nini afurahi.Na alikuwa sahihi,kwa sababu baada ya mahusiano yetu na Mungu,ndoa zetu zinafuata na wapenzi wetu.Mtume paulo alisema kuwa anashauri watu wasioe au wasiolewa kwa sababu mtu akioa,anakuwa anawaza atamfurahushaje mke wake vile vile kwa mwanamke aliyeolewa. Kwa hiyo,moja ya njia itakayokufanya uwe na mahusiamo mazuri,ni kumuweka mpenzi wako mbele baada ya Mungu.

NINI MAANA YA UPENDO AU MAPENZI.?

Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
1 KOR. 13:4‭-‬8 
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: