EPISODE 1: FAHAMU JINSI YA KUINGIA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO,KUUATHIRI NA JINSI YA KUPIGANA VITA VYA KIROHO
Salamu wapendwa,Leo tunaanza kipengele kipya kinachohusiana na jinsi ya kuingia kwenye ulimwengu wa roho na ukifika ujue jinsi ya kupambama na maadui utakao wakuta.
Ni lazima tufahamu,kuwa ulimwengu wa roho ni ulimwengu halisi kabisa,Ni kama ulimwengu huu tunaoishi sasa hivi,tofauti ni kwamba tu wenyewe hatuwezi kuuona kwa macho ya nyama ndomana mda mwingine inatuwia vigumu kuelewa ulimwengu wa roho kwa sababu hiyo.
Sasa lazima tujue jinsi ya kuuendea huo ulimwengu wa roho na kuuathiri ili kuleta mabadiliko
Kuomba ni namna ya mtu kwenda kwenye ulimwengu wa roho,biblia inasema mungu niroho nao wamwabudua yawapasa kuwa katika roho YOHANA 4:23-24.

WAEBRANIA 11:6 Inasema kila mtu amwendeaye mungu (katika ulimwengu wa roho),inamaana kuomba ni njia yakwenda alipo mungu,yaani rohoni.
Ulimwengu wa roho ni halisi mno,kama unavyoona mtu wa mwili,basi jua kuwa kuna mtu wa rohoni,kama unavyoona Tanzania ya mwilini basi jua kuna Tanzania ya rohoni,Ni kitu halisi mnoo.
2 Wakorintho 4:18
"Tusiangalie vinavyoonekana ni vya muda,Tuangalie vitu visivyoonekana ni vya milele" Kwahiyo vitu vya kiroho vipo,lakn havionekan kwa damu na nyama.Tunakumbuka hadithi ya Elisha na malaika tunaona kuwa malaika hawa hawakuja baadabya elisha kuomba,bali walikuweko muda wote,Maombi ya elisha hayakuwaleta malaika,bali yalifungua tu macho ya yule kijana aliyekuwa haoni.
"2 Wafalme 6:8-17"
Sasa hakuna kitu kinachofanya kazi|kuzaliwa kwenye ulimwengu wa mwili mpaka kianzie rohoni,Tukumbuke kuwa mungu aliumba kwanza ulimwengu wa roho ndipo akaufanya uonekane kimwli yaani kwa macho ya nyama.Kwahiyo kabla ya kitu chochote kifanyika mwilini lazima kwanza kifanyike rohoni na kikamilike.

WAEBRANIA 11:3 "Nasi twajua ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la mungu,hata vitu vya kimwili havikuumbwa  na vitu vinavyoonekana,bali visivyoonekana"
kwahiyo ulimwengu wa roho uliumbwa kwanza,baada ya mungu kukamilisha hiyo kazi ndipo akazalisha ulimwengu wa mwili,Ni sawa na Negative na picha,huwa inaanza negative halafu picha halisia hufuatia,lakini ile negative huwa ndiyo kitu halisi,hata picha ikija kupote,kama bado una negative basi mambo yanakuwa hayajaharibika,na hivyo ndivyo mungu anavyofanya kazi,anaanza rohoni halafu anafuata mwilini.Litambue hilo.
Kumbe basi kila kitu cha kimwili kinachakoroho chake. Katika kitabu cha wakorintho kinasema "ikiwa kuna mwili unaoonekana basi kuna mwili usioonekana"
Kumbe tunajifunza kuwa kama unataka kuutawala ulimwengu wa mwili,Afya,masomo,tabia nk.Lazima uufahamu vizuri ulimwengu wa roho uanzie huko rohoni na ujue namna ya kuuende na kuuathiri ili ulete mabadiliko kwasababu hata maisha yalianzia rohoni.........
Sasa linapotokea lolote mwilini,afya imeyumba,tabia kubadilika,uchumi,usidhani kwamba limeanza leo,Limeshakuweko kwenye ulimwengu wa roho muda mwingi sasa limeamua kujitokeza tu kwenye mwili ili ionekane......
Ayubu 8:9 inasema maisha yetu ni kivuli (photocopy).
Itaendelea,..........
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

3 comments: