#Biblerocks
#PART 1
Sadaka ni kitu cha kiroho sana. Kwa kiingereza tunaita sacrifice ama matoleo na biblia inasema wazi kabisa kuwa pale sadaka yako ilipo ndipo moyo wako ulipo. 
--
Mungu hana shida ya kuangalia DNA yako ili ajue moyo wako au akujue wewe,Sadaka yako inajisemea yenyewe mbele za Mungu.
--
Sadakq
NGUVU YA SADAKA YA DAMU
Maana ya sadaka.
👉Sadaka ina maana nyingi sana hasa tukitaka tuizungumsmzie kidunia. ila tukirudi kiimani yetu basi tutapata maana halisi ya sadaka.

Sadaka ni huduma ya kiroho,haikuanzishwa na wanadamu ila Mungu mwenyewe. Adam na eva walippfanya dhambi,Maandiko yanasema Mungu alitoa kafara ya kwanza ya wanyama kwa ajiri ya adam na eva na kuwafunika na ngozi za wanyama. (mwanzo 3:21).

Kwahiyo sadaka hutolewa kwa Mungu kama upatanisho kati yetu na yeye,kwa ajiri ya makosa fulani ama kwa ajiri ya shukrani.1👇
Sasa hapa tunapata vitu vya aina 2.
👉Matoleo  na kafara 😅

nacheka kwanza. kwa kiingereza zinaitwa offerings na sacrifices ikimaanisha kafara. Wengi tunatambua kuwa kafara lazima ihusishe damu. Katika tamaduni zetu ukisikia neno kafara unakuw na picha halisi kabisa ya Damu damu kuhusika
vivyohivyo..katika maandiko,sacrifice ama kafara mara zote huhusisha damu. Damu lazima ihusishwe kwenye kafara yeyote,iwe damu ya mdudu,wanyama,ndege ama mwanadamu. Na ndipo hapa ambapo familia nyingi zimekamatwa kutokana na sacrifices ambazo zilishawahi kifanywa uko nyuma.
Pia tuna offerings,kama matoleo.Soma Hesabu 28:2 ,na 31:50 utaona aina za matoleo.

Matoleo yanaweza yakawa ya fedha,vitu,mali zingine na hata wanyama. hii ni ishara ya heshima ni sawa na pale mtu anapoenda kwa mfalme,lazima abebe kitu mikononi mwake kama heshima...
So tuna offerings na sacrifices.

Hii imekuwepo tangu kipindi cha torati ambapo YAHWEH alimkabidhi maagizo haya musa. Sadaka nyingi na kafara za aina nyingi zimekuwa zikitumika mpaka lilipo bomolewa hekalu la kwanza miaka ya 70AD. wakristo wengi tumekuwa tukiaminishwa kuwa offerings na sacrifices ziliishia pale..hashaaa


NATEGEMEA UMEPATA KITU KIDOGO

TUKUTANE SEHEMU IJAYO
Axact

Tanzania Worships

Haleluyah! Karibu katika ukurasa wa Tanzania Worships ambao ni maalumu kwa ajili ya kusambaza na kulihubiri Neno la Mungu anayeishi. je kuna maoni na ushauri unataka kuuutoa ili kuhakikisha ukurasa huu unawafikia waamini na wasioamini? basi usione shaka kuwasiliana nasi kwa njia ya mitandao ya kijamii

Post A Comment:

0 comments: